Ole Gunnar Solskjaer: Je kocha huyu atapona kufuatia msururu wa matokeo mabaya Man United?


Mkufunzi wa Man United Ole Gunnar Solskjaer

Ni msimu mwengine ambao wakufunzi walioshindwa kuzisaidia timu zao kuvuka viwango fulani wamepata shinikizo kali kutoka kwa bodi simamizi za timu wanazofunza mbali na mashabiki wa timu hizo.

Shinikizo katika baadhi ya timu zimesababisha kufutiliwa mbali kwa wakufunzi hao ama hata kupewa onyo la kufutwa iwapo misururu ya matokeo mabaya itaendelea kushuhudiwa.

Hivi majuzi klabu ya AC Milan ilimteua Stefano Pioli kama meneja wake mpya, kufuatia kufutwa kwa Marco Giampaolo siku ya Jumanne baada ya miezi mitatu akiifunza timu hiyo.

Hatua hiyo ilichukuliwa kufuatia msururu mbaya wa matokeo. Lakini sio timu hiyo pekee ambapo meneja alikabiliwa na shinikizo kali na hatimaye kufutwa.

Kabu ya Olympique Lyonnais ya Ufaransa wiki hii imemfuta kazi kocha wake Sylvinho baada ya kuwa na matokeo mabovu toka walipompa kazi miezi michache iliyopita.

Ijapokuwa hawajapigwa kalamu wakufunzi kama vile Zinedine Zidane wa Real Madrid ,Pochettino wa Tottenham na Marcos Silva wa Everton pia wapo chini ya shinikizo kufuatia matokeo mabaya.

Katika klabu ya Everton , aliyekuwa kocha wa timu hiyo David Moyes anapigiwa upatu kuchukua mahala pake Silva huku Jose Mourinho akitarajiwa kumrithi Zinedine Zidane iwapo atapigwa kalamu.

Silva huenda akaachishwa kazi baada ya timu yake kushindwa kupata ushindi wa ligi tangu siku ya kwanza ya mwezi Septemba licha ya kununua wachezaji wapya.

Klabu hiyo ilimuunga mkono na zaidi ya £100m msimu uliokwisha lakini kumekuwa na ishara chache za timu hiyo kuimarika uwanjani.

Mourinho ni miongoni mwa wakufunzi waliokumbwa na kipindi kigumu katika klabu ya Man United kufuatia matokeo mabaya yanayodaiwa kusababishwa na mbinu yake ya uchezaji, uhusiano mbaya kati yake na wasimamizi wa bodi ya timu hiyo pamoja na wachezaji na kadhalika.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Ni nini kilichojiri? alipigwa shoka na mahala pake kuchukuliwa naye mkufunzi wa sasa Ole Gunnar Solskjaer ambaye ni mmojawapo wa wachezaji wa kikosi cha United kilichoshinda kombe la mabingwa Ulaya 2008.

Je ni wakati kwa Ole Gunnar kuiaga Man United?

Baada mkufunzi huyo kuanza na mguu mzuri, kwa kushinda mechi 14 kati ya 19 akiwa kaimu mkufunzi aliandikisha kandarasi ya miaka mitatu.

Lakini tangu hapo kocha huyo ameshindwa kuinoa timu hiyo licha ya kupewa fursa ya kusajili wachezaji wakati wa dirisha la uhamisho lililopita.

Na kufikia sasa timu hiyo ipo katika nafasi ya 12 na pointi 9 baada ya kucheza mechi nane huku ikishinda mara mbili kushindwa mara tatu na kutoka sare mara tatu.

Wachanganuzi wanatabiri kwamba timu hiyo itajipata katika eneo la kushushwa daraja baada ya mechi dhidi ya Liverpool na Norwich hatua ambayo huenda ikaamua hatma ya kocha Olegunnar Solskjaer.

Matumaini pekee ya United kujizolea pointi ni kucheza katika uwanja wa Old Trafford, lakini hilo pia halijaizuia United kupoteza mechi kufikia sasa,

Kocha huyo ameshinda mechi mbili pekee kati ya 13 na hivyobasi kuwa mara ya kwanza kwa United kuanza vibaya katika ligi ya England katika kipindi cha miaka 30.

Amedaiwa kuwaambia wachezaji wake kwamba kazi yake ipo hatarini baada ya klabu hiyo kushindwa na Newcastle mbali na kuwasisitizia wachezaji hao kwamba hatma zao hazijulikani iwapo hawataimarika , huku meneja mpya akitarajiwa kuchukua mahala pake.

”Ningependa kuomba msamaha kwa mashabiki kwa sababu hatushindi mechi , lakini hilo litanatokana na kuanza upya kujijenga, hivyobasi tumejipatia jukumu kubwa la kuweza kufaulu katika timu sita bora, bila kujali timu nne bora. Hivi sasa tunahitaji matokeo ili tuweze kwenda mbele”, alinukuliwa akisema.

Je anahitaji muda zaidi

Kocha huyo amekuwa akiomba kupewa muda zaidi na usimamizi wa timu hiyo kuwa na subra naye.

Man United imejikuta imewekeza pakubwa na sio tu kwa kandarasi ya miaka mitatu aliyopewa kocha huyo.

Mabadiliko ya kuwanunua Harry Maguire na hususan Aaron wan Bissaka pamoja na Dan James yamepokelewa vyema.

Ukweli kwamba wachezaji hao watatu wameanza vyema ni swala ambalo limemshawishi Ed Woodward kwamba klabu hiyo ipo katika mwelekeo mwema.

Tatizo ni kwamba Woodward na Man United wataendelea kulimbikiziwa lawama iwapo watahisi kuendelea kumuunga mkono Solskjaer.

Hatahivyo baada ya kuruka kutoka mkufunzi mmoja hadi mwengine tangu alipostaafu Sir Alex Furguson kuna kiu cha mkufunzi ambaye ataendelea kuifunza timu hiyo .

Ufutaji wa David Moyes, Louis Van Gaal hadi Jose Mourinho haukuwa mzuri na athari zake zilikuwa ghali mno.

Lakini mapendekezo yoyote kwamba hilo pekee ni sababu kwa Solskjaer kusalia katika wadhfa huo – baada ya msururu wa matokeo ambayo yameleta ushindi mara 2 katika mechi 13 za ligi ya England – ni kutoeleweka kwa jukumu la mkufunzi katika klabu ya kisasa.

Solskjaer anazungumzia kuhusu kuimarisha utamaduni wa klabu hiyo na ni swala linalovutia kwa kweli ,lakini Sera kama hizo zinawezekana bila yeye kuwepo.

United haimuhitaji mkufunzi huyo kutilia mkazo sera ya kuleta wachezaji vijana na wale walio na kiu katika kikosi hicho.

Lengo lake ni kuimarisha timu hiyo uwanjani na kutumia raslimali zilizopo kwa lengo la kupata matokeo mazuri – kupitia mbinu nzuri ya mchezo.

Lakini hali ilivyo ni kwamba ameshindwa na hana rekodi yoyote ya kumshawishi mtu yeyote kwamba atafanya lolote isipokuwa kuendelea kufeli katika siku za usoni.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *