Guterres aisifia Somalia kuanza kujijenga kitaasisi


Hata hivyo, Guterres alisema kuwa inabidi serikali ya Somalia ipambane na watu wenye itikadi kali wanaotumia nguvu, ugaidi, makundi yenye silaha, hali tete ya  kisiasa na rushwa.

Aliyasema hayo katika ripoti iliyowasilishwa katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kusambazwa  siku ya Jumatatu (Mei 21) kwamba changamoto hizo zinaonesha udhaifu wa hatua zilizopigwa hadi sasa na kutishia maendeleo zaidi.

Baada ya miongo mitatu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, mashambulizi ya watu wenye itikadi kali na  njaa, Somalia imeweza kuwa na serikali kamili mwaka 2012 na  hadi sasa imekuwa ikifanyakazi kujenga hali thabiti.Source link

Jumanne Kishimba: Kwanini mbunge huyu anataka bangi kuhalalishwa Tanzania?


Bunge la Tanzania

Mbunge wa Kahama mjini, Jumanne Kishimba anataka serikali kuhalalisha matumizi ya bangi ama marijuana nchini tanzania kwa mautumizi ya dawa.

Aliambia bunge siku ya Jumatatu kwamba mataifa mengine manne ya Afrika tayari yemahalalisha Marijuana kutumiwa kutengeneza dawa.

Kulingana na gazeti la The Citizen nchini Tanzania mbunge huyo anasema kuwa ni vyema kama taifa kuanza kufikiria kuhusu fursa hiyo mapema.

”Tunavyozungumza, Uganda imehalalaisha upanzi wa Marijuana kwa matumizi ya dawa”, alisema akitaja ripoti za hivi majuzi kwamba taifa hilo la Afrika mashariki limenunua mbegu kupanda mmea huo.

”Sijui ni kwa nini kitengo cha chakula na dawa hakijachukua sampuli kuelezea serikali kwamba dawa hizo zina bangi ndani yake”, alihoji.

Kulingana na gazeti hilo ,bangi kama inavyojulikana ni haramu nchini Tanzania na inavutia hukumu kali jela na faini kubwa.

”Tuna bangi lakini kile kinachoonekana kila siku ni maafisa wa usalama kuharibu mmea huo. Bangi imetumika kwa miaka kadhaa kutengeneza dawa”.

Bangi hutumika kutengeneza dawa

Alisema kwamba Lesotho na Zimbabwe zilihalalisha utumizi wake akiongezea kwamba amewahi kuona kiwanda kinachotengeneza dawa kwa kutumia bangi.

Aliongezea kuwa gunia moja la bangi linauzwa kati ya Sh4 million na Sh4.5 millioni huku likiuzwa Sh20 millioni nchini Zimbabwe na Lesotho.

WebMD, Mtandao unaotoa habari za kiafya unasema kuwa ushahidi mkubwa kuhusu mmea wa bangi ni uwezo wake wa kupunguza maumivu, kichefuchefu na kutapika baada ya mgonjwa kupatiwa tiba ya kutumia kemikali {chemotherapy}.

Kulingana na The Citizen Tanzania Uganda inatarajiwa kuuza bangi inayotumika kama dawa yenye thamani ya Shilingi bilioni 600 billion mwezi Juni kwa taifa la Canada na Ujerumani ikilinukuu gazeti la The Daily Monitor nchini Uganda.

Imani ya Rastafari

Imebainika kwamba mnamo tarehe 7 mwezi Disemba Uganda iliuza bangi, na mauwa yenye thamani ya $10,000 kwa kampuni moja ya Afrika kusini.

Muungano wa Rastafari nchini Tanzania ni mojawapo wa mashirika ambayo yanashinikiza wazo la kuhalalishwa kwa bangi katika taifa hilo.

Rasta wanaamini kwamba mmea wa ‘Tree of Life’ uliotajwa katika bibilia ni ule wa bangi.

Mbali na imani za wengi , Rasta hushutumu matumizi ya marijuana kwa lengo la ulevi.

Wale wanaounga mkono wazo la mmea huo kuhalalishwa nchini Tanzania ni pamoja na mbunge wa Geita mashambani muheshimiwa Joseph Msukuma.

Katika kikao cha bunge Msukuma alisema kuwa hajawahi kusikia ama kuona utafiti wowote wa kisayansi uliopata bangi na miraa kuwa na tatizo lolote.

Alisema kuwa hatua ya serikali kuharamisha mimea hiyo haina msingi wowote.

Msimamo wa Serikali

Hatahivyo serikali ya Tanzania imepinga uwezekano wowote wa kuhalalishwa kwa mmea huo katika taifa hilo.

Haki miliki ya picha
Bunge/Tanzania

Mnamo mwezi Februari 2016, naibu waziri wa afya Dkt. Hamis Kigwangalla alipinga kuhalalishwa kwa bangi na miraa ahihusisha utumizi wake na matatizo ya kiakili .

”Tafiti kadhaa zimethibitisha kwamba matumizi ya marijuana yanasababisha matatizo ya kiakili na hivyobasi serikali haiwezi kuhalalisha matumizi yake”, alisisitiza Kigwangalla.

Lakini mwenyekiti wa Rastafari United Front Thau-Thau Haramamba anasema kuwa matatizo ya kiakili yanayowakabili watumizi wa bangi hayatokani na matumizi ya bangi badala yake uchanganyaji wa bangi na vitu vileo vingine.

Anahoji kwamba hakuna utafiti umewahi kupata matumizi ya mmea huo kushirikishwa na tatizo la Kiakili.Source link

Kwanini DRC Mashariki ni eneo hatari?


Wanajeshi wa DRC

Haki miliki ya picha
Getty Images

Watu 19 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya mtu mwenye silaha kusahambulia soko la samaki nchini Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC).

Tukio hilo limetokea karibia na mji wa Ituri uliopo kwenye pwani ya ziwa Albert.

“Maiti 19 ziligunduliwa katika kijiji cha Tara, na watu wengine wanane kujeruhiwa,” Pilo Mulindo, kiongozi wa jadi wa eneo hilo amenukuliwa na shirika la habari la kimataifa la AFP.

Maiti hizo zimegundulika Jumapili na tukio lilitokea Jumatano ya wiki iliyopita.

Hakuna kundi la waasi ambalo limejitokeza kukiri kuhusika kwenye mauaji hayo. Lakini eneo hilo linafahamika kwa vita ya kikabila baina jamii za Hema na Lundu.

Mapigano ya makabila hayo mawili yameshapelekea vifo vya watu zaidi ya 100 na wengine zaidi ya 300,000 kuvuka ziwa Albert na kutafuta hifadhi kama wakimbizi nchini Uganda.

Amani mashariki ya DRC

Ingawa maeneo karibu yote ya DRC yamekuwa yakikumbwa na changamoto za usalama kama vita ama kushambuliwa na waasi mara kwa mara, eneo la mashariki ya nchi hiyo ndiyo lililoathirika zaidi.

Akiongea na BBC siku chache kabla ya kuondoka madarakani mwishoni mwa maka 2018, rais mataafu wa nchi hiyo, Joseph Kabila amesema katika mambo ambayo angekuwa na muda zaidi kuyashughulikia ni kurudisha amani kwa taifa hilo.

Mashariki mwa DRC kuna makundi ya kijeshi ya waasi na kikabila mengi kupindukia.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Baadhi ya makundi yanaondwa na raia wa nchi hiyo, lakini kuna amakundi mengine makubwa ambayo yanafadhiliwa ama kupambana za serikali za nchi jirani.

Baadhi ya makundi ya waasi yanayotokea nchi jinani ni FDLR ambalo lilitekeleza mauaji ya kimbari nchini Rwanda mwaka 1994 na wapiganaji wake kukimbilia DRC.

Waasi wa ADF wanatokea nchini Uganda.

Makundi hayo ya waasi yanatumia misitu mizito iliyopo kwenye eneo hilo kujificha na kuendesha shughuli zao huku wakitangaza nia ya kushambulia nchi zao walizozikimbia.

Uganda na Rwanda zimeshavamia DRC mara mbili kwa lengo la kusambaratisha makundi hayo na vita hizo kupelekea mamilioni ya watu kufariki.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Vikosi vya kulinda amani chini ya Umoja wa Mataifa (UN) vipo mashariki ya DRC

Eneo hilo la Mashariki ya DRC pia linakabiliwa na ugonjwa hatari wa Ebola ambapo moja ya sababu za kushindikana kushughulikiwa kikamilifu ni uwepo wa makundi ya waasi hao.

Mwezi Machi mwaka huu shirika la habari la kimataifa la Reuters liliripoti kuwa, kundi la waasi la Mai Mai lilishambulia kambi ya matibabu ya Ebola na kuua polisi na kufurusha wagonjwa na wahudumu wote wa afya.

Makundi hayo pia yamekuwa pia yakishutumiwa kwa ubakaji wa wanawake katika maeneo wanayoyashambulia, na kufanya ubakaji kuwa ni moja ya matatizo makubwa yanayolikumba eneo hilo.

Uwepo wa makundi hayo ya waasi yamefanya Umoja wa Mataifa kupeleka kikosi maalumu (MONUSCO) kulinda amani. Hata hivyo, wachambuzi wengi wamekuwa wakilaumu vikosi hivyo kwa kushindwa kutekeleza wajibu wake ipasavyo.Source link

Widodo achaguliwa tena rais wa Indonesia


Kulingana na tume ya uchaguzi Widodo ameshinda kwenye majimbo 21 kati ya 34, kwa jumla ya kura milioni 85.6, dhidi ya Subianto aliyepata kura milioni 68.5.

Zoezi la kuhesabu kura lilimalizika rasmi usiku wa jana na tume ya uchaguzi nchini humo ikatangaza matokeo mapema hii leo. Matokeo hayo yalimuonyesha rais Widodo kuongoza kwa asilimia 55.5 ya kura zote, akifuatiwa na Generali huyo wa zamani Subianto na anayejifungamanisha na Waislamu wenye itikadi kali aliyepata asilimia 45.5.

Indonesien Yogyakarta - Präsidentschaftswahl (picture-alliance/NurPhoto/R. Hamiid)

Vituo vya kupigia kura vikiwa vimenakshiwa kwa rangi za kuvutia

Maelfu ya polisi na wanajeshi walikuwa katika tahadhari kubwa katika mji mkuu Jakarta, wakitarajia kuzuka kwa maandamano ya wafuasi wa Subianto. Ofisi za makao makuu ya tume ya uchaguzi zilizoko katikati ya mji wa Jakarta zimezungushiwa nyaya za umeme na ulinzi mkali.

Alipozungumzia ushindi huo, Widodo amesema yeye pamoja na mgombea mwenza wake, kiongozi wa dini mhafidhina, Ma’ruf Amin watakuwa rais na makamu wa rais wa watu wote wa Indonesia.

Indonesien wählt neuen Präsidenten und Parlament | Joko Widodo und Prabowo Subianto (picture-alliance/AP Photo)

Prabowo Subianto(pichani kulia) ameahidi kupinga matokeo hayo mahakamani

Subianto ambaye pia alishindwa kwenye uchaguzi wa 2014 dhidi ya Widodo na kujaribu bila mafanikio kupinga matokeo mahakamani amedai kuwepo kwa udanganyifu mkubwa kwenye uchaguzi lakini hajatoa kithibitisho chochote cha msingi.

Wakaazi wa Jakarta nao wameyapokea matokeo hayo kwa hisia tofauti, hasa kufuatia madai hayo ya Subianto. Ahmad Djunaedi alisema “Nadhani wanatakiwa kwenda mahakama ya katiba, kama wana mashaka na matokeo hayo, kwa sababu mahakama ya katiba ipo kwa ajili ya kusuhisha madai yoyote ya uchaguzi. Waende mahakamani kwanza, kisha sisi raia tutasubiri maamuzi ya mahakama”.

Afisa wa kampeni za Subianto Sufmi Dasco Ahmad amesema watawasilisha kesi hiyo kwenye mahakama ya katiba katika kipindi cha siku tatu. Widodo ameeleza kuridhishwa na namna mpinzani wake huyo anavyochukua hatua za kupinga matokeo hayo kwa kuzingatia katiba na sheria.

Awali Subianto na wafuasi wake walitishia kuingia mitaani kupinga matokeo hayo kwa kutumia nguvu ya umma badala ya kwenda mahakamani kwa sababu hawana imani kama mahakama hiyo itatenda haki.

Waangalizi huru na wachambuzi wamesema uchaguzi huo ulikuwa huru na wa haki, ingawa Prabowo na timu yake ya kampeni wanaibua madai hayo ya udanganyifu.

Iwapo mahakama itapata vithibitisho vya kutosha kufungua kesi hiyo, inatakiwa kutoa uamuzi katika kipindi cha siku 14 baada ya nyaraka zote kuwasilishwa na wadai. Uamuzi wa mahakama hiyo ni wa mwisho na haukatiwi rufaa.

 Source link

Margeret Nyairera Wambui: Mwanariadha wa kike wa Kenya asema hawezi kupunguza homoni za kiume


Caster Semenya (katikati) alishinda dhahabu katika mashindano ya madaola 2018 , Mkenya Margaret Nyairera Wambui (kushoto) na Natoya Goule wa Jamaica Jamaica (kulia)

Haki miliki ya picha
AFP

Image caption

Caster Semenya (katikati) alishinda dhahabu katika mashindano ya madaola 2018 , Mkenya Margaret Nyairera Wambui (kushoto) na Natoya Goule wa Jamaica Jamaica (kulia)

Bingwa wa mbio za mita 800 nchini Kenya kwa upande wa akina dada Margeret Nyairera Wambui amesema kuwa hatotumia dawa za kupunguza homoni za kiume ili kushiriki katika mbio hizo.

Akihojiwa na BBC mwanariadha huyo amesema kuwa dawa hizo zina kemikali ambazo huenda zikakuathiri katika maisha ya baadaye.

”Mimi siwezi kutumia dawa kwa lengo la kutaka kupata fedha,Mungu aliniumba niwe hivi nilivyo – kumbuka dawa hizi zina kemikali ambazo madhara yake baadaye huenda yakawa mabaya katika mwili wako. Wakati huo wote IAAF haitakuwa hapo”.

Mwanadada huyo mwenye umri wa miaka 24 ni miongoni mwa wanariadha walioathiriwa na sheria mpya ya shirikisho la riadha duniani IAAF inayowataka wanawake walio na viwango vya juu vya homoni za kiume testosterone kutumia dawa ili kuzipunguza mwilini.

IAAF inasisitiza kuwa sheria hiyo ni nzuri katika kuleta usawa katika mashindano , ikihoji kwamba wanariadha wenye homoni za kiume wanafaidika kutokana na ongezeko la nguvu katika mifupa yao na misuli sawa na wanaume walio balehe.

Lakini mwanadada huyo wa Kenya analalamika kwamba tangu Shirikisho la riadha duniani IAAF liidhinishe sheria hiyo maisha yake yamebadilika na kuwa magumu.

”Kwa sasa unajipata umeketi kitandani hujui ufanye nini, ukiamka hujui uende wapi kufanya mazoezi na hata ukifanya mazoezi hujui utakwenda wapi. Hii ndio biashara tunayofanya, ndio inatupatia kila kitu cha kunywa, mahitaji yote, inatusaidia kuwekeza halafu unaamka siku moja unaambiwa sasa kuanzia leo huezi kuendelea na bishara hiyo-lazima maisha yako yataathirika kidogo”, alisema bingwa huyo wa mita 800.

Alitarajiwa kushiriki katika mbio za IAAF World Challenge mjini Nanjing wiki ijayo lakini sasa maisha yake yamegubikwa na swali gumu.

”Usiku usingizi unapotea unajua ni kitu inahusisha maisha yako kwa sababu tayari ulikuwa na malengo yako lakini sasa malengo hayo yamekatizwa”,aliongezea.

Sheria hiyo mpya inaathiri kuanzia mbio za mita 400 hadi maili moja na inashirikisha mbio za Heptathlone zenye vitengo saba ambapo mshindi hukamilisha mbio hizo kwa kushiriki mbio za mita 800.

Nyairera anasema kuwa hawezi kuhamia katika mbio za mita 5000 akisema kwamba hajawahi kushiriki mbio yoyote mbali na ile ya mita 800 ambapo ujuzi na mafunzo tofauti yatahitajika ili kufikia kiwango hicho.

”Sasa kuanza kukimbia mita 5000 kutoka 800 ni kitu hakiwezekani. Sijawahi kukimbia 5000m nikipitia laini ya utepe mara ya kwanza najua kwamba mara ya pili nimemaliza sijawahi kupita Utepe mara hizo zote”.alisema

Chini ya sheria ya IAAF, wanariadha wa kike walio na viwango vya juu vya homoni za kiume watalazimika kushindana na wanaume la sivyo wahamie katika mbio nyengine iwapo hawawezi kutumia dawa kupunguzi viwango vya homoni hizo.

Sheria hiyo mpya itaathiri kuanzia mbio za mita 400 hadoi zile za maili moja na mahitaji yake ni kwamba wanariadha ni sharti wapunguze viwango vyao vya homoni za kiume chini ya kiwango kinachohitajika kwa zaidi ya miezi sita kabla hawajaanza kushindana.

Hatahivyo sheria hiyo mpya imepata wakosoaji huku baraza la haki za binaadamu katika shirika la Umoja wa mataifa likisema kwamba hatua ya kuwaorodheshwa wanariadha wa kike kulingana na viwango vyao vya homoni za kiume inakiuka haki za kibinaadamu.

Hivi majuzi mahakama ya kutatua mizozo katika michezo CAS ilipinga rufaa iliokatwa dhidi ya Mwanariadha wa Afrika Kusini Caster Semenya ambaye ni miongoni mwa wale walioathiriwa na sheria hiyo.

Lakini mahakama hiyo ilisema kuwa ina wasiwasi mkubwa kuhusu matumizi ya sheria hiyo katika siku za baadaye.

Haki miliki ya picha
AFP

Semenya ambaye ni bingwa duniani katika mbio za mita 800 alijibu kwamba sheria hiyo ilikuwa ikimlenga yeye binafsi.

”Kwa muongo mmoja sasa IAAF imejaribu kunikata makali, lakini hatua hiyo imenifanya kuwa na nguvu”, alisema Semeyna

Uamuzi huo wa mahakama ya kutatua mizozo hautanizuia, alisema Semeynya katika taarifa.Source link

Je, Dk. Bashiru Ally 'anajiandaa' kuitosa CCM?


Dkt Bashiru akihutubia mkutano wa hadhara

Haki miliki ya picha
CCM

Mei 31 mwaka huu mwanazuoni, Dk. Bashiru Ally, atatimiza mwaka mmoja tangu alipoteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa chama tawala nchini Tanzania CCM akichukua nafasi ya Kanali Abdulrahman Kinana.

Uteuzi wake katika nafasi hiyo, Mei 31, 2018 ulikuja muda mfupi baada ya kuwa Mwenyekiti wa Kamati iliyoundwa kufuatilia mali za chama hicho. Majukumu yote hayo yalishangaza wengi, na hakika ni wachache tu ambao walikuwa wakijua kuwa mhadhiri huyo alikuwa ni kada wa CCM.

Bashiru alijijengea sifa na heshima miongoni mwa jamii ya Watanzania kwa kuwa mchambuzi huru wa masuala ya kisiasa na kijamii, na mara kadhaa alichukua msimamo mkali wa mawazo dhidi ya serikali na CCM yenyewe.

Katika kipindi cha mwaka mmoja wa majukumu yake katika nafa kuu ya utendaji wa chama, Dk. Bashiru ameonyesha namna gani anataka kuendana na kasi ya Mwenyekiti wake, Rais Dk. John Pombe Magufuli.

Makala haya yanaangazia matamko au kauli ambazo Dk. Bashiru amekuwa akizitoa kwa kipindi chote tangu akabidhiwe madaraka hayo. Aidha, makala haya hayatajibu kila jambo bali yanaangalia mwelekeo wa Katibu mkuu huyo wa chama tawala.

Hivi karibuni Dk. Bashiru amezungumzia hatima yake iwapo atamaliza muda wa kuwa Katibu mkuu wa CCM. Upesi alieleza kuwa atarudi kufundisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Tafsiri tunayopata kwa mwaka mmoja huu bado Dk. Bashiru Ali haonekani kuwa na mipango ya muda mrefu katika siasa. Kwamba haonekani kuwa anahitaji kuendelea kubaki kwenye siasa za utendaji mkuu na majukwaani. Kwa tafsiri nyingine Katibu huyo anaonesha hana mpango wa kuendelea kukitumikia CCM, kana kwamba amejiandaa kukitosa muda ukifika au kabla haujafika muda wake wa kung’atuka.

Kulalamikia viongozi vijana

Dk Bashiru Ally ameonekana ‘kukilalamikia’ chama chake kwa kushindwa kufanya kazi ya kuandaa viongozi bora kupitia jumuiya zake, hali inayosababisha kuwa na wanasiasa vijana ambao hawana maadili, hawana unyenyekevu, hawajali hisia za watu wala kuzingatia muktadha na masilahi ya chama hicho.

Akizungumza wakati wa misa ya mazishi ya Mwenyekiti wa kampuni za IPP, Reginald Mengi iliyofanyika katika kanisa la KKKT Usharika wa Moshi mjini, mkoani Kilimanjaro na kuoneshwa moja kwa moja kwa njia ya Televisheni.

Haki miliki ya picha
Ikulu, Tanzania

Image caption

Bashiru aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM baada ya kuchunguza mali za chama hicho

Ikikumbukwe Katibu huyo amelalamikia mwenendo wa Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe, ambaye hadi sasa anamtaja kama mwanasiasa aliyepitia Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wakati mfumo wa kuandaa viongozi ukiwa umekufa. Jambo hilo pia alililifanya septemba mwaka 2018 akielezea mwenendo wa kisiasa wa Mbunge huyo na wengine wa kariba yake.

Aidha, amemlalamikia Mbunge wa Mtama mkoani Lindi, Nape Nnauye, ambaye amesema anahitaji kusikilizwa, kupikwa na kuongozwa zaidi katika siasa na uongozi ndani ya CCM na taifa kwa ujumla. Kurudiwa kwa matamshi ya Dk. Bashiru dhidi ya wabunge hao na CCM kwa ujumla wake kunaonesha anajaribu kujitenga na siasa za CCM pamoja na mwenendo wake uliokuwapo na unaoendelea sasa.

Dk. Bashiru amekuwa akilalamikia viongozi wasiofundishwa uongozi, hali ambayo inaonesha wazi Katibu huyo ni kama vile anatengeneza mlango wa kutokea CCM. Ni kama vile anawakebehi kwa kushindwa kukijenga chama au kukosa dira ya kuzalisha vongozi mahiri miongoni mwa wanasiasa vijana kutoka jumuiya zake.

Mwanachama mmoja mkongwe wa chama hicho amemwambia mwandishi wa makala haya kuwa, “Katibu wetu anaonekana kama vile hahusiki na anajitenga na makosa ya viongozi ambao anaamini hawajapitia Chuo cha Diplomasia.”

Kumsema ‘Mkuu wa Mkoa Kipenzi cha Rais’

Tangu aingie madarakani Rais Dk. John Magufuli ameonekana dhahiri kumpenda Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda na mara kadhaa amemsifu hadharani.

Ikumbukwe mwaka 2017, rais John Magufuli alimtetea hadharani mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa barabara za juu katika makutano ya Ubungo jijini Dar es Salaam.

Haki miliki ya picha
MAKONDA INSTAGRAM

Utetezi huo ulikuja ikiwa ni muda mfupi tangu kutokea tukio la kuvamia ofisi za chombo cha habari, hatua ambayo ilimlazimu aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye kuunda kamati ya uchunguzi chini ya Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Deodatus Balile.

Dk. Bashiru Ally amemsema hadharani mara tatu mkuu wa mkoa kipenzi cha rais Magufuli, Paul Makonda. Mwaka 2019 akiwa kwenye ziara ya kichama mkoani Simiyu na pili akiwa kwenye Misa ya mazishi ya bilionea wa kitanzania, Dk. Reginald Mengi mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Septemba 2018 katika mahojiano na gazeti la kila wiki la Raia Mwema, Dk. Bashiru alimuonya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam juu ya tabia yake ya kuwaita wakazi wa Dar es Salaam, wananchi (Mkoa) wangu. Bashiru alisema “Na hii habari ya Dar es Salaam ya Makonda, hakuna Dar es Salaam ya Makonda, ni Dar es Salaam chini ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Makonda. Kuna wakati namsikia anasema wananchi wangu, nani kamwambia anao wananchi wake? Hakuna wananchi wako. Hakuna kiongozi anamiliki wananchi, ni wananchi wenzangu.”

Mara ya tatu ni kwenye Misa ya mazishi ya Reginald Mengi mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro, Dk. Bashiru alisema, “Kuwa viongozi bora, watiifu, wanyenyekevu na wenye heshima, naomba nitumie fursa hii kumuombea msamaha kijana wangu Makonda mimi namfahamu na hii ni mara yangu ya pili namsema hadharani,”

“Mara yangu ya kwanza nilimsema Simiyu akaja analia ofisini nikasema ubadilike na kwa kweli ameanza kubadilika, bado ni kijana mzuri, shupavu lakini tunahitaji kuwasaidia vijana wetu,” amesema Dk. Bashiru Ally.

Image caption

Bashiru alimkosoa na kumuombea radhi Makonda kwenye msiba wa bilionea Reginald Mengi

Matamshi haya yanaonesha wazi Dk. Bashiru Ally si kama viongozi wengine ambao wanaogopa kumsema vibaya Mkuu huyo wa Mkoa wakitambua kuwa ni kiongozi kipenzi cha rais ambaye alikuwa chanzo cha kutimuliwa kwa aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye. Wanachama wa CCM wanatambua kuwa ni vigumu kwa sasa kumsema vibaya Paul Makonda kisha wakaendelea kubaki kwenye wadhifa wao. Kwahiyo hatua ya Dk. Bashiru inawashangaza wengi na kuamini kuwa Katibu huyo ni kama vile ‘hana cha kupoteza’ hivyo yupo tayari ‘kukitosa’ chama hicho.

Chama na jumuiya ‘kukosa nguvu’

Bashiru akiwa mtendaji mkuu wa CCM amepitia vipindi vya kawaida mno, huku chama chenyewe na Jumuiya zake nguvu zikiwa zimefifia mno katika siasa kwa ujumla wake.

CCM hakuna matamko ya kisiasa. Hakuna mihemko ya kisiasa wala pilika zozote ambazo zimezoeleka kuchangamsha siasa za nchi kati ya chama tawala na wapinzani wake. Pilika zote kisiasa ‘zimeporwa’ na serikali jambo ambalo linadhoofisha taasisi yenyewe ya chama na jumuiya zake.

Hakuna umahiri wa vijana katika anga za kisiasa dhidi ya wapinzani wa CCM, badala yake kila jambo limekuwa likijibiwa na Msemaji wa Serikali badala ya chama chenyewe ‘kujibu mapigo’.

Mwandishi wa makala haya amewahi kumwuliza Katibu wa Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole kuwa kulikoni chama kimekuwa bubu kwenye masuala ambayo yanahitaji majibu ya kisiasa kama sehemu ya siasa zenyewe? Hakukuwa na majibu halisi, angalau baadaye Katibu huyo alianza mabadiliko kwa ‘kujibu mapigo’ katika matamko ya kisiasa.

Hasara ya serikali ‘kupora’ shughuli za kisiasa za chama ni kuvunja nguvu, uimara na utamaduni wa kisiasa ambao ndiyo huibua umahiri wa wanasiasa kutoka ndani ya chama na kuleta ugumu kwenye zoezi zima la uchaguzi wa serikali za mitaa, uchaguzi mdogo au uchaguzi mkuu. Hayo yote yanatokea wakati Dk. Bashiru Ally ndiye mtendaji mkuu, kana kwamba hayaoni au amekubali kuwa nguvu ya wanasiasa wa serikali ndiyo imekua kubwa kuliko ya wanasiasa wa siasa.

Anafuata nyayo za Kinana ?

Image caption

Abdulrahman Kinana alikuwa akiikosoa serikali wakati akuhudumu kama Katibu Mkuu wa CCM

Tafsiri nyingine ya matamshi ya Dk. Bashiru Ally yanaonesha kufuata nyayo za mtangulizi wake, Abdulrahman Kinana, ambaye aliingia kwa gia ya kuonekana kama vile mtu ambaye hahusiki na ubovu wa viongozi wa chama na serikali. Kinana alifanya ziara ya kukagua utekelezaji Ilani ya CCM kama ambavyo Dk. Bashiru Ally afanyavyo sasa.

Ziara za Kinana akiwa sambamba na aliyekuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye zilianzia katika mikoa ya Tabora, Singida na Manyara ambapo inadaiwa kuwa iliongeza kasi ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama hicho kati ya mwaka 2010-2015.

Nape na Kinana wamekuwa wakitajwa kurudisha matumaini ya wananchi kwa CCM, ambapo waliwataka mawaziri wanaohusika kwenda kutoa majibu ya malalamiko ya wananchi waliotoa tuhuma mbalimbali mbele yake.Source link

Justin Amash amejitetea dhidi ya matamshi yake makali kwa Trump


Mbunge wa jimbo la Michigan nchini Marekani aliyekuwa m-Republican wa kwanza kutoa wito kwa Rais Donald Trump afunguliwe mashtaka alijitetea siku ya Jumatatu japokuwa msimamo wake ulimsababisha kushambuliwa na warepublican wengine wanaomuunga mkono Trump.

Mbunge Justin Amash anayehudumu kwa muhula wa tano bungeni aliwaeleza wakosoaji wake kwamba walieleza matamshi kadhaa ya uongo katika kudai kwamba Trump hakuzuia mkondo wa sheria kufanya kazi kwa kujaribu kusitisha uchunguzi wa muda mrefu uliofanywa na mwendesha mashtaka maalumu Robert Mueller kuhusiana na Russia kuingilia kati uchaguzi mkuu wa urais Marekani 2016.

Rais Donald Trump

Rais Donald Trump

Wakosoaji wa uchunguzi wa Mueller akiwemo rais mwenyewe wanadai kwamba Trump hakuweza kuzuia mkondo wa sheria kufanya kazi kwa sababu hakukuwa na uhalifu wa kuzuia sheria kufanya kazi kwa kuwa Mueller aligundua kuwa sio Trump wala kampeni yake ilishirikiana na Russia kumsaidia Trump ashinde kuingia White House.

Lakini Amash alieleza kuwa wachambuzi wa sheria wa Marekani wanakubaliana kwamba kizuizi cha sheria hakihitaji hatua ya kuelezea uhalifu wenyewe.Source link

Jamhuri ya Congo imepigia kura marekebisho ya ulipaji deni lake kwa ChinaBaraza la seneti la Jamhuri ya Congo siku ya jumatatu lilipiga kura ili kufanya marekebisho ya baadhi ya utaratibu wa ulipaji madeni yake kwa China hatua ambayo shirika la kimataifa la fedha-IMF lilisema ilikuwa muhimu ili kuwezesha msaada wa kifedha kutolewa kwa nchi hiyo.

Mashauriano juu ya kutolewa msaada wa kifedha kuokowa uchumi wa taifa hilo linalotegemea mafuta yalikuwa yanadorora tangu mwaka 2017 wakati maafisa wa Congo waliposhindwa kuishawishi IMF kwamba walikuwa wakifanya vya kutosha kudhibiti deni la kitaifa au kukabiliana na rushwa.

Kutokana na juhudi hizo ujumbe wa IMF ulieleza mwezi huu wa Mei kwamba ulikubaliana na serikali ya Congo juu ya mpango wa miaka mitatu wa kutoka mkopo ikiwa mageuzi yatatekelezwa na kuidhinishwa na bodi ya wakurugenzi wa IMF.Source link

Yemen: Kuponea kifo katika mji 'unaoshambuliwa' na wadunguaji


Taiz ni mji wa tatu kwa ukubwa nchini Yemen. Wakati mmoja ulisifika kwa maendeleo lakini sasa umebakia mahame na magofu ya majumba yaliyoporomoka- baada ya kuathiriwa vibaya na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Watu ambao bado wanaishi katika mji huo wamejipata katikati ya mashambulio kati ya waasi wa Kihouthi na vikosi vinavyounga mkono serikali ya Yemen. Hakuna hata mtu mmoja aliyesalama.Source link