Wilfred Bungei: Ni heri kujihusisha na biashara unayoipenda


Baadhi ya wanariadha hujitosa kwenye biashara baada ya kustaafu. Je, ushindi uwanjani unamaanisha kuwa pia watafaulu wanapowekeza?

BBC Mitikasi walizungumza na Wilfred Bungei ambaye ni bingwa wa Olimpiki wa mbio za mita mia nane katika makala ya mwaka elfu mbili na nane, na ambaye sasa anafanya biashara kadhaa magharibi mwa Kenya.

Je, amejifunza nini kuhusu biashara?Source link

Wanawake 100 wa BBC: Wanawake wanaouawa siku moja maeneo tofauti duniani


An average of 137 women across the world are killed by a partner or family member every day

Image caption

Wanawake 137 huuawa kila siku kote duniani

Takriban wanawake 137 kote duniani huuawa na waume na pia wapenzi wao au watu wa familia kila siku, kwa mujibu wa data mpya zilizotolewa na ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na madawa na uhalifu (UNODC).

Wanasema nyumbani ndilo eneo ambapo kuna uwezekano mkubwa zaidi kwa mwanamke kuuawa.

Zaidi ya nusu ya wanawake 87,000 waliuawa mwaka 2017 waliripotiwa kufa mikononi mwa watu walio karibu nao.

Kati ya idadi hiyo takriban wanawake 30,000 waliuawa na wapenzi wao na wengine 20,000 waliuawa na watu wa familia.

BBC 100 walitaka kujua zaidi wanawake waliojipata kwenye takwimu hizi. Tunakupa hadithi kuhusu baadhi ya mauaji haya na jinsi yaliripiotiwa.

More than half of women killed were victims of relatives or partners

Image caption

Zaidi ya nusu ya wanawake waliuawa na wapenzi au jamaa

Idadi ya wanaume wanaouawa bado ni ya juu

Data iliyokusanywa na UNODC ilionyesha kuwa wanaume kote duniani wako na uwezekano mara nne zaidi kuliko wanawake kupoteza maisha kutokana na kuuliwa makusudi

Umoja wa Mataifa unasema kuwa wanaume wanachangia vifo 8 kati ya 10 kote duniani.

Pia ripoti hiyo hiyo inasema kuwa zaidi ya vifo 8 kati ya 10 vya muaji yaliyofanywa na wapenzi ni dhidi ya wanawake.

Women are much more likely to be killed by someone close to them

Image caption

Wanawe wako katika hatari zaidi ya kuuliwa na mtu aliye karibu nao

Wanawake arobaini na saba, nchi 21, siku moja

Takwimu za Umoja wa Mataifa zinachambua matokeo ya mwaka 2017 yanayotokana na takwimu za mauaji kutoka kwa serikali.

BBC 100 Women na BBC Monitoring walichukua hatua ya kufahamu zaidi kuhusu wanawake walioathiriwa.

Tulifuatilia wanawake waliouawa na watu wengine Oktoba mosi mwaka 2018 kote duniani. Wanawake 47 walihesabiwa kuuliwa kwa sababu zinazohusu jinsia kwenye nchi 21 tofauti na mengi ya mauaji haya bado yanachunguzwa.

Hivi ni visa vitano vilivyoripotiwa na vyombo vya habari na kisha kuidhinishwa na mamlaka mabzo BBC iliwasiliana nazo.

Judith Chesang

Haki miliki ya picha
Family handout

Image caption

Judith Chesang

Judith Chesang, 22, Kenya

Jumatatu 1 Oktoba Judith Chesang na dada yake Nancy walikuwa shambani wakivuna mtama.

Judith, mama wa watoto watatu alikuwa ametengana na mume wake Laban Kamuren na kuamua kurudi kwa wazazi wake katika kiji kilicho kaskazini mwa nchi.

Mara dada hao walianza kufanya kazi, aliwasili katika shamba la familia akashambulia na kumuua Judith.

Polisi wanasema Laban aliuawa na wanakijiji.

Women in Africa most at risk

Image caption

Wanawake barani Afrika ndio walio kwenye hatari zaidi

Afrika ndilo eneo wanawake wako kwenye hatari kubwa zaidi ya kuuawa na wapenzi wao au na mtu wa familia kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa. Ilifanyika kwa watu 3.1 kati ya watu 100,000.

Asia ilikuwa na idadi ya juu zaidi ya wanawake waliouwa na wapinzani au watu wa familia mwaka 2017, kwa jumla wanawake 20,000.

Neha Chaudhary

Haki miliki ya picha
Manohar Shewale

Image caption

Neha Chaudhary

Neha Sharad Chaudury, 18, India

Neha Sharad Chaudury aliuawa wakati siku yake ya kuhitimiza miaka 18. Alikuwa ameenda kusherehekea na mpenzi wake. Polisi waliiambia BBC kuwa wazazi wake hawakukubaliana na uhusiano huo.

Wazazi wake na mwanamume mmoja wa familia wanalaumiwa kwa kumuua akiwa nyumbani usiku huo.

Uchunguzi unafanywa na watatu hao wako kuzuizini wakisubiri kushtakiwa.

BBC iligundua kutoka kwa wakili anayewakilisha wazazi wa Neha na mwanamume wa familia kuwa wanataka kukana mashtaka hayo.

Zeinab Sekaanvand

Haki miliki ya picha
Private via Amnesty International

Image caption

Zeinab Sekaanvand

Zeinab Sekaanvan, 24, Iran

Zeinab Sekaanvan alinyongwa na mamlaka za Iran kwa kumuua mume mwake.

Zeinab alizaliwa kaskazini magharibi mwa Iran kwenye familia moja maskini eneo la Kurdi. Alikimbia nyumbani akiwa msichana kuolewa akiwa na matumaini ya kupata maisha mazuri.

Amnesty International inasema mume wake alikuwa anadhulumu na alikataa kumpa talaka na kwamba malalamiko yake yalipuuzwa na polisi.

Alikamtwa kwa kumuua mume wake akiwa na umri wa miaka 17.

Waliomuunga mkono wakiwemo Amnesty wanasema aliteswa ili akiri kumuua mume wake, akapigwa na polisi na hakupata hukumu yenye haki.

Sandra Lucia Hammer Moura

Haki miliki ya picha
Reproduction / Facebook

Image caption

Sandra Lucia Hammer Moura

Sandra Lucia Hammer Moura, 39, Brazil

Sandra Lucia Hammer Moura aliolewa na Augusto Aguiar Ribeiro akiwa na miaka 16.

Wanandoa hao walikuwa wametengana kwa miezi mitano wakati mume wake alimuua.

Polis huko Jardim Taquari waliiambia BBC kuwa alichomwa kisu shingoni.

Walipata video ya mume wakae kwenye simu yake. Kwenye video hiyo alisema Sandra alikuwa na urafiki na mwamamume mwingine na alihisi kuhujumiwa.

Pia alisema kuwa hawezi kukamatwa kwa sababu wote watanda kwa Mungu pamoja. Kisha akajinyonga kwenye chumba chao cha kulala.

Marie-Amélie Vaillat

Haki miliki ya picha
PHOTOPQR/LE PROGRES/Photo Jean-Pierre BALFIN

Image caption

Marie-Amélie Vaillat

Marie-Amélie Vaillat, 36, Ufaransa

Marie-Amélie alichomwa kisu na kuuawa na mume wake, Sébastien Vaillat.

Wanandoa hao walikuwa wametengana baada ya miaka minne ya ndoa.

Alimshambulia kwa kisu kabala ya kukiri kwa polisi. Siku chache baadaye alijiua akiwa gerezani.

Nje ya mlango wa duka la Marie-Amélie Vaillat eneo la Rue Bichat, wenyeji waliacha maua na kupanga kufanya matembezi kwa heshima kwake.

A march in memory of Marie-Amélie Vaillat

Haki miliki ya picha
PHOTOPQR/LE PROGRES/Photo Jean-Pierre BALFIN

Image caption

Makumbusho ya Marie-Amélie Vaillat

Inagharimu nini kisa cha kuuliwa mwanamke kuripotiwa?

Kukusanya ripoti hizi, mtandao ya waandishi wa habari wa BBC Monitoring na watafiti walichambua televisheni, radio, magazeti na mitadao ya kijamii kote duniani, wakiangalia ripoti za wanawake waliouawa tarehe 1 Oktoba mwaka 2018.

Walipata jumla ya ripoti 47 za wanawake walioauawa kote dudiani. Tumechapisha baadhi ya visa hivi. Kuna vingine vingi ambavyo nia yao haijulikani au waliotekeleza hawajatambuliwa.

BBC 100 Women logo

Je wanawake 100 ni nini?

BBC 100 Women huwataja wanawake 100 wenye ushawishi na wenye kutia moyo kote duniani kila mwaka na tunaangazia hadithi zao.

Umekuwa mwaka wenye umuhimu katika masuala ya haki za wanawake kote duniani, kwa hivyo mwaka 2018 msimu wa Wanawake bora 100 wa BBC, utaangazia wanawake waasisi wanaotumia ari, hasira na ghadhabu kushinikiza mageuzi halisi duniani.

Jumuika nasi kwenye Facebook, Instagram na Twitter na tumia #100WomenSource link

Mikoko inavyoimarisha maisha pwani ya Kenya


Kongamano la kwanza duniani la uchumi wa maji linafanyika mjini Nairobi Kenya. Maelfu ya wajumbe wanakutana kuzungumzia namna ya kunufaika kutokana na raslimali za bahari, mito na ziwa bila ya kuziharibu. Katika kijiji cha Gazi pwani ya Kenya, jamii hii imejuwa namna ya kunufaika kwa kilimo cha mikoko.

Mpiga picha: Kenneth MungaiSource link

Ndoto yake ni kuwa mkufunzi wa walimbwende wenye ualbino


Elizabeth James mshiriki wa shindano la mr na miss Albino Afrika Mashariki. Ndoto yake ni kuwa mkufunzi wa walimbwende hasa wenye ualbino. Mlimbwende huyu kutoka Tanzania anasema licha ya kudhihakiwa na kuitwa majina ya kuvunja moyo hana hofu na uwezo wake katika Sanaa na ulimbwende na ana uwezo wa kutumia vyema talanta yake. Mlimbwende huyu alizungumza na mwanahabari wetu Eagan SallaSource link

Kumekuwa na dhana potofu kuhusiana na jinsi mtu anavyoweza kuambukizwa HIV


Disemba mosi ni siku ya kimataifa ya UKIMWI Duniani

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Disemba mosi ni siku ya kimataifa ya UKIMWI Duniani

Suala la maambukizi ya virusi vya HIV vinavyosababisa ugonjwa wa Ukimwi bado linaendelea kuwakosesha usingizi wataalamu wa afya kote duniani.

Kwa mujibu wa shirika la Afya Duniani (WHO) ugonjwa huo umewaangamiza zaidi ya watu milioni 35 kufikia sasa.

Mwaka jana pekee, karibu watu milioni moja walifariki kutokana na magonjwa yanayohusishwa na virusi vya HIV.

Kuna karibu watu milioni 37 ambao wanaishi na virusi hivyo – 70% kati yao wanapatikana barani Afrika – huku watu milioni 1.8 wakiambukizwa umpya mwaka 2017.

Tangu ugonjwa wa Ukimwi ulipogunduliwa miaka ya 1980, kumekuwa na gumzo kuhusiana na jinsi virusi vyake vinavyoweza kusambazwa.

Je maisha ya waathiriwa wa ugonjwa huo katika jamii yamekuaje?

Leo Ulimwengu unapoadhimisha siku ya Ukimwi Duniani, tunaangazia baadhi ya dhana potofu zinazosababisha kunyanyapaliwa kwa waathiriwa.

Dhana: Naweza kuambukizwa virusi vya HIV kwa kutangamana na watu waliyoathirika

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Uchunguzi wa damu ni muhimu ili kubaini kama una virusi vya HIV

Dhana hizi zimesababisha unyanyapaa dhidi ya waathiriwa wa ugonjwa wa UKIMWI kwa muda mrefu.

Licha ya kuendeshwa kwa kampeini ya mwaka 2016 ya kuhamasisha watu nchini Uingereza kuhusiana na suala hilo 20% ya watu nchini humo wanaamini HIV inaweza kusambazwa kupitia mate au kumgusa mtu aliyeambukizwa virusi hivyo.

Huwezi kuambukizwa virusi vya HIV kupitia:

  • Kwa kuvuta hewa moja
  • Kukumbatiana, kubusiana, au kusalimiana
  • Kutumia pamoja vyombo vya kula chakula
  • Kutumia maji pamoja
  • Kutumia pamoja vitu vya kibinasi
  • Kutumia pamoja vifaa vya mazoezi
  • Kugusa kiti cha msalani, komeo la mlango na kadhalika

Haki miliki ya picha
Ronald Grant

Image caption

Mwaka 1991, Princess Diana wa Wales alikutana na waathiriwa wa Ukimwi mjini London katika juhudi za kukabiliana na dhana kuhusu njia za maambukizi ya virusi vya HIV

Virusi vya HIV huambukizwa kupitia damu, kunyonyesha au kufanya ngono bila kinga na mtu aliye na virusi hivyo.

Dhana: Dawa za kienyeji zinaweza kuzuia maambukizi ya HIV

Huu si ukweli hata kidogo . Dawa za kienyeji, kuoga baada ya kufanya tendo la ndoa au kufanya ngono ya mdomo haina athari yoyote dhidi ya HIV.

Utamaduni wa utakaso ambao ulipata umaarufu katika mataifa ya jangwa la sahara , na maeneo ya India na Thailand, umetajwa kuwa hatari sana.

Umesababisha wasichana kubakwa na watoto wadogo kunajisiwa hali ambayo inawaeka katika hatari ya kuambukizwa virusi vya HIV.

Chimbuko la utamaduni huo linaaminiwa kuwa barani Ulaya katika karne ya 16 ambapo watu walianza kuambukizwa magonjwa ya zinaa kama vile kisonono na kaswende.

Utamaduni huo hata vyo haukuwahi kutibu magonjwa hayo pia.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

HIV haiambukizwi kwa kumgusa mtu aliyeathiriwa au kwa kuumwa na mbu

Dhana: Mbu wanaweza kusambaza virusi vya HIV

Japo maambukizi hupitia damu, tafiti kadhaa zinaonyesha kuwa mtu hawezi kupata maambukizi kutoka kwa wadudu wanaofyonza damu kwa sababu hizi mbili.

1) Mbu hamuongezei mtu damu mwilini kabla ya kumuuma mtu.

2) Virusi vya HIV huishi ndani yao kwa kwa muda mchache.

Kwa hivyo hata mtu akiishi katika eneo lililo na mbu wengi, maambukizi ya HIV hayahusiani kwa vyovyote na mbu hao.

Dhana: Siwezi kupata virusi vya HIVkwa kufanya ngono ya mdomo

Ni kweli ngono ya mdomo huenda si hatari sana ikilinganishwa na aina nyingine ya ngono.

Viwango vya maambukizi ni chini ya nne katika visa 10,000.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Mipira ya kondomu husaidia kumkinga mtu dhidi ya virusi vya HIV na magonjwa mengine ya zinaa

Lakini mtu anaweza kupata maambukizi ya virusi vya kufanya ngono ya mdomo na mwanamume au mwanamke aliye na virusi hivyo.

Ndio maana madaktari wanapendekeza matumizi ya mpiria wa kondomu wakati wa kufanya gono ya mdomo.

Dhana: siwezi kuambukizwa virusi vya HIV nikivaa mpira wa kondomu

Mipira ya Kondomu inaweza kupasuka, kutoka au kuvuja wakati wa tendo la ndoa hali ambayo huenda ikawaeka katika hatari ya maambukizi ya virusi wapenzi wote wawili

Hii ndio maana kufanikiwa kwa kampeini dhidi ya UKIMWI hakukomei katika muktadha wa kuwaambia watu kutumia kinga pekee, bali bia kuna haja ya wale waliyeambukizwa virusi vya HIV kupata matibabu.

Kwa mujibu wa shirika la Afya Duniani WHO, mmoja kati ya kila watu wanne ana virusi vya HIV na mtu huyo hana habari – hii inamaanisha watu milioni 9.4 – wako katika hatari kubwa ya kuambukizwa ugonjwa huo hatari.

Dhana: Kama huna dalili huna virusi vya

Mtu anaweza kuwa na virusi vya ukimwi na asiwe na habari.

Hata hivyo huenda akapatikana na magonjwa kama vile homa inayofanana na influenza-ikiwa ni pamoja na kuumwa na kichwa,kushikwa na homa, harara mwilini au kuumwa na koo katika wiki chache za kwanza baada ya kuambukizwa viini vinavyosababisha ugonjwa wa UKIMWI.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Mmoja kati ya kila watu wanne ana virusi vya HIV na mtu huyo hana habari

Dalili zingine kama vile kupungua uzani, kuharisha na kukohoa hujitokeza kadiri kinga ya mwili inavyoendelea kupungua.

Muathiriwa asipopata matibabu huenda akapatikana na magonjwa kama vile kifua kikuu, homa ya utandu wa ubongo miongoni mwa zingine

Dhana: Mtu aliyepatikana na virusi vya HIV atafariki akiwa na umri mdogo

Watu wanaojua hali yao ya HIV na kuzingatia matibabu na lishe bora huishi kwa muda mrefu.

Shirika la UNAids linasema 47% ya watu wote wanaoishi na virusi vya HIV huwa wamedhibiti kiwango cha virusi hivyo mwilini kwa kutumia dawa.

Hii inamaanisha watu hao hawawezi kusambaza virusi hivyo hata wakijamiana na mtu ambaye hana virusi hivyo.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Hata hivyo wakisitisha matibabu viwango vya virusi vinaongezeka na vinaweza kuonekana katika damu yake.

Kwa mujibu wa WHO, watu milioni 21.7 waliyo na virusi vya HIV wamekuwa wakitumia dawa za kukabiliana na virusi hivyo mwaka 2017.

Idadi hiyo imeongezeka kutoka watu milioni 8 mwaka 2010 – hii inamaanisha 78% ya watu waliyo na virusi vya HIV wanajua hali yao.

Dhana: Kunamama waliyoathirika watawaambukiza watoto wao

Suala hilo lina mjadala lakini uwezekano wa akina mama ambao wamedhibiti kabisa kiwango cha virusi vya HIV katika miili yao wanaweza kuwanyonyesha watoto wao bila kuwaambukiza virusi hivyoSource link

Kenya: Mashindano ya ulimbwende ya Albino Afrika Mashariki 2018


Haki miliki ya picha
George Okurut

Image caption

Mr na Miss Albino

Mr Albino Afrika Mashariki ni Emmanuel Silas kutoka Tanzania ambaye pia ni mshindi wa vipaji.

Wakati Miss Albino ni Maryanne Mungai kutoka Kenya ambaye alishinda kwa kuwa na vazi la kibunifu.

Haki miliki ya picha
George Okurut

Haki miliki ya picha
George Okurut

Mr Albino Uganda- Paul WakibonaMs Albino Uganda- Olive Auma

Haki miliki ya picha
George Okurut

Haki miliki ya picha
George Okurut

Image caption

Mr Albino Tanzania-Emmanuel Silas

Mr Albino Tanzania-Emmanuel Silas

Miss Albino Tanzania- Chevawe Kasure

Haki miliki ya picha
George Okurut

Mr Albino Kenya- Oreen Wakhulunya

Ms Albino Kenya- Maryanne Mungai

Haki miliki ya picha
George Okurut

Image caption

Mr na Miss Albino

Haki miliki ya picha
George OkurutSource link

Je! Utawapeleka wazazi wako katika Makao ya Wazee?


Kwa wakongwe kupelekwa katika nyumba ya wazee, maisha yao yanaweza kuwa bora au wakati mwengine kuwa

yenye shida. Mpiga picha mmoja aliyeangazia maisha ya wakongwe katika nyumba hizo za malezi, amesema hangependa kuwasumbua watoto pindi anapokuwa na umri mkubwa.

Je! wewe unaweza kuwapeleka wazazi wako wakongwe katika makao hayo?

Tuwasiliane kwenye facebook BBCSwahili.comSource link