Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 21.05.2019: Sane, Pogba, Conte, Batistuta, Giroud


Leroy Sane

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Leroy Sane

Bayern Munich wanaamini kuwa watamsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Ujarumani Leroy Sane, 23, kutoka Manchester City msimu huu wa joto. (Mirror)

Manchester United wanatarajiwa kuitisha euro milioni 160 (£138m) kumuuza kiungo wa kati wa kimataifa wa Ufaransa Paul Pogba, 26. (Star)

Mlinzi wa Leicester na nyota wa kimataifa wa England Harry Maguire, 26, ni mmoja wa walinzi wa kati wanaolengwa na Manchester City kuchukua nafasi ya Vincent Kompany. (Sky Sports)

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Paul Pogba

Meneja mpya wa Anderlecht, Kompany anamfuatilia kwa karibu kocha wa chuo mpira cha Manchester City, Simon Davies na mkuu wa sayansi ya michezo Sam Erith, kuungana nae mjini Brussels. (Telegraph)

Meneja wa zamani wa Chelsea Antonio Conte ameafiki masharti ya kujiunga na Inter Milan kama kocha wao mpya msimu ujao. (Guardian)

Juventus wameachana na Conte na sasa wanamlenga meneja wa sasa wa Chelsea, Maurizio Sarri. (Sun)

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Antonio Conte

Arsenal wametoa ofa ya kumnunua kipa wa valencia Mbrazilia Norberto Murara, baada ya kuzungumzana wawakilishi wa mchezaji huyo wa miaka 29. (Star)

Nyota wa zamani wa kimataifa wa Argentina Gabriel Batistuta, 50, bado hajafikia kiwango cha ukufunzi wa timu kubwa lakini sasa inaaminiwa kuwa ameonesha nia ya kuchukua nafasi ya usimamizi iliyoachwa wazi katika klabu ya Middlesbrough. (Hartlepool Mail)

Chelsea wanatarajiwa kuthibitisha kuwa mshambuliaji wa kimataifa Ufaransa Olivier Giroud, 32, amekubali kusalia katika klabu hiyo kwa mwaka mmoja mwingine. (London Evening Standard)

Meneja wa Ireland Kaskazini Michael O’Neill amaeibuka moja wa watu wanaopigiwa upatu kuchukua nafasi ya umeneja iliyoachwa wazi West Brom. (Express and Star)

Haki miliki ya picha
EPA

Meneja mkuu wa Hertha Berlin Michael Preetz amefanya mazungumzo na mwenzake wa Liverpool Jurgen Klopp katika juhudi za kutafuta huduma za kiungo wa kati wa kimataifa wa Serbia Marko Grujic, 23, kwa mkopo wa mwaka mwingine tena. (Liverpool Echo)

Mlinzi mahiri wa zamani wa Brighton Bruno, 38, anasomea kozi ya ukufunzi wa Uefa mjini Belfast. (Argus)

Tetesi bora Jumatatu

Streka wa PSG na Ufaransa Kylian Mbappe, 20, amebainisha kuwa anaweza kuihama klabu yake katika kipindi hiki cha usajili. Kauli hiyo inatarajiwa kuziamsha klabu kongwe na tajiri kama Real Madrid, Barcelona na Manchester City kumgombea. (Express)

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Kylian Mbappe

Kiungo raia wa Ujerumani Ilkay Gundogan, 28, anataka kurudi mezani na klabu yake ya Manchester City kwa malengo ya kusalia klabuni hapo zaidi ya mwezi Juni 2020 ambapo mkataba wake wa sasa unaishia. (Mail)

Kocha Pep Guardiola atapewa fursa ya kusalia klabuni Manchester City walau kwa miaka mitano ijayo huku kipato chake kikifikia pauni milioni 100, baada ya mshahara wake kwa mwaka kuchupa toka pauni milioni 15 mpaka milioni 20. (Sun)

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola

Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane amemwonesha dalili za wazi winga raia wa Wales Gareth Bale, 29, kuwa muda wake katika klabu hiyo umefikia tamati, baada ya kusema kuwa asingemuingiza mchezoni kutoka benchi walipofungwa Jumapili na Real Betis hata kama kungekuwa na fursa ya kuingiza wachezaji wanne. (Eurosport)

Bale hata hivyo amewaambia wachezaji wenzake kuwa anapanga kusalia klabuni hapo mpaka kwisha kwa mkataba wake na takuwa mwenye furaha kucheza gofu endapo hatapangwa kucheza. (Radioestadio, via Mail)

Kiungo wa Chelsea na Ufaransa N’Golo Kante, 28, anapiga hessabu za kuikacha klabu yake na kujiunga na miamba ya Ligi ya Ufaransa PSG. (Talksport)Source link

Sudan yashindwa tena kuafikiana


Baraza la mpito la kijeshi na wawakilishi wa makundi ya upinzani nchini Sudan wameshindwa tena kuafikiana kuhusu kuundwa kwa chombo kipya kitakachotawala taifa hilo, wakati mazungumzo baina yao yakikabiliwa na mkwamo kuhusu watawala wa chombo hicho, kati ya wanajeshi ama raia. 

Baraza hilo le kijeshi na wawakilishi hao wa makundi ya upinzani walikutana tena kwenye kasri la rais kuanzia Jumatatu jioni kuhitimisha mapendekezo ya muundo wa chombo hicho, lakini hawakufanikiwa kufikia makubaliano.

Hakuna upande uliozungumzia kuhusu kurejea kwa mazungumzo hayo, lakini mmoja wa viongozi wa waandamanaji Siddiq Yousef aliwaambia waandishi wa habari kwamba mazungumzo yalisitishwa tena hadi kutakapopatikana suluhu kati yao na baraza na kijeshi.

Afrika | Protests im Sudan (picture-alliance/dpa/AA/M. Hjaj)

Waandamanaji nchini Suda wanataka serikali ya mpito ya kiraia.

Hata hivyo baraza hilo halitoa tamko lolote kuhusu kuahirishwa kwa mazungumzo hayo. Lakini kulingana na taarifa ya pamoja iliyotolewa na wawakilishi wa jeshi na makundi hayo usiku wa jana baada ya majadiliano hayo kusitishwa ilisema suala moja kubwa ambalo bado linazozaniwa linahusiana na mgawanyo wa wawakilishi wa kijeshi na raia kwenye baraza hilo, na nani atakuwa kiongozi wa baraza hilo jipya. 

Kiongozi maarufu wa Muungano wa Freedom and Change Satea al-Haj amesema baraza la kijeshi linasisitiza kwamba rais wa baraza hilo huru anatakiwa kutoka jeshini, na kukataa kiongozi wa kiraia. Awali al-Haj alisema, wanahalalisha hilo kwa kudai kwamba taifa hilo linakabiliwa na vitisho vya kiusalama. Kulingana na al-Haj, jumuiya ya kimataifa haitakuwa tayari kushirikiana na serikali ya kijeshi.
    
Pande hizo mbili zilianzisha raundi ya pili ya mazungumzo Jumapili jioni kuhusu baraza litakalotawala Sudan katika miaka mitatu ya mpito, kufuatia kuondolewa kwa aliyekuwa rais Omar al-Bashir. 
 
 Source link

Muhindi wa tabaka la chini la Dalit auawa kwa 'kukalia kiti na kula' mbele ya watu wa tabaka la juu


Jitendra

Image caption

Jitendra alikuwa akifanya kazi seremali kuikimu familia yake

Jamii ya wahindi wa tabaka la chini linalojukina kama Dalit linaomboleza kifo cha mmoja wao aliyeuawa kwa kosa la ”kukalia kiti na kula” mbele ya watu wa tabaka la juu katika kijiji cha Kot nchini India.

Mwezi uliyopita kundi la wanaume wa jamii ya wahindi wa tabaka la juu lilidaiwa kumpiga vibaya mtu aliyefahamika kama Jitendra mwenye umri wa miaka 21 ili kumuadhibu lakini alifariki siku 9 baadae.

Hakuna hata mmoja kati ya mamia ya wageni waliohudhuria harusi hiyo aliyejitokeza kuelezea masaibu yaliyomkuta Jitendra siku ya April 26.

Lakini polisi imesema wazi nini kilichotokea.

Chakula katika harusi hiyo kilipikwa na watu wa jamii ya tabaka la juu kwasababu watu katika kijiji hicho hawagusi chakula kilichopikwa na Dalit ambao zamani waliitwa “wasio guswa”.

“Mzozo uliibuka wakati chakula kilipokua kikipakuliwa kuhusu nani aliyekalia kiti,” afisa wa polisi Ashok Kumar alisema.

Image caption

Geeta Devi anasema alimpata mwanawe akiwa amejeruhiwa nje ya nyumba yao

Ameongeza kuwa kisa hicho kimerekodiwa chini ya sheria (kupinga udhalimu) – iliyotungwa kuzilinda jamii zilizobaguliwa kihistoria nchini India.

Watu wa jamii ya Dalits, wamekuwa wakibaguliwa kwa muda mrefu nchini humo na jamii za matabaka ya juu.

Wakazi wa kijiji hicho kutoka jamii ya Dalit wanadai kuwa Jitendra alipigwa na kudhalilishwa harusini.

Wanasema aliondoka katika sherehe hiyo akilia machozi, lakini aliviziwa na kushambuliawa tena hatua chache kutoka mahali hapo na kupigwa vibaya sana.

Mma yake Jitendra, Geeta Devi, alimpata akiwa amejeruhiwa karimu saa za asuhuhi.

“Huenda alilala hapo usiku kucha,” alisema huku akionesha mahali alipomkuta. “alikuwa na majeraha na alama kila mahali mwilini mwake. Nilijaribu kusema nae lakini hakuweza kunijibu.”

Image caption

Dalit ni wachache wakilinganishwa na familia zingine katika kijiji cha Kot katika jimbo la Uttarakhand

Bi Geeta Devi, hajui ni nani aliyemuacha mwanawe nje ya nyumba yao. Alifariki dunia siku tisa baadae akipokea matibabu hospitali

Kifo cha Jitendra ni pigo kwa mama yake ambaye alimpoteza mume wake karibu miaka mitano iliyopita.

Kati ya familia 50 zinazoishi katika kijiji cha kina Jitendra, ni familia 12 ama 13 ndio wa tabaka la chini la Dalit.

Polisi imewakamata watu saba wanaoshukiwa kuhusika na kifo cha Jitendra lakini wote wamekanusha kuhusika na kisa hicho.

“Hii ni hujuma dhidi ya familia yetu,” alisema mmoja wa mwanamke ambaye baba yake, ndugu zake na wajomba zake wanatuhumiwa kutekeleza uovu huo.

“Kwanini baba yangu atumie suala l matabaka katika harusi ya Dalit ?” aliuliza mwanamke huyo.

Lakini jamii ya Dalit katika kijiji hicho ambao walishuhudia kifo cha Jitendra, wanapinga vikali madai hayo.

Image caption

Watu wa tabaka la juu katika kijiji hicho wamekanusha madai ya kuwabagua watu wa jamii ya Dalit

Wanasema Jitendra alipatikana na ugonjwa wa kifafa, lakini wanapinga uwezekano kuwa alitumia dawa kupita kiwango alichoshauriwa na daktari.

Licha ya machungo waliyo nayo, familia za wadalit katika kijiji hicho wamekuwa watulivu.

“Hii ni kwasababu wanategemea familia ya watu wa tabaka la juu kiuchumi,” mwanaharakati Daulat Kunwar alisema.

“Dalit wengi hawana ardhi na wao huwafanyia kazi majirani zao wa tabaka la juu. wanajua athari ya kupaza sauti kuhusu kisa hicho.”

Familia ya Jitendra tayari imeshuhudia athari hizo- Geeta Devi anasema kuwa wanashinikizwa kutosema ukweli kuhusu kile kilichotendeka.

“Wanaume fulani walikuja nyumbani kwetu kututisha,” alisema “Hakuna wa kutusaidia lakini haturudi nyuma hadi tupate haki yetu.”Source link

Kylian Mbappe: PSG inasama mshambuliaji wa Ufaransa atasalia Klabu hiyo msimu ujao


Kylian Mbappe

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Mbappe alishinda tuzo ya mchezaji bora wa Ligue 1msimu

Kylian Mbappe”ataendeleza historia ya uhusiano wake” na Paris St-Germain kwa kutuwakilisha msimu ujao, wanasema mabingwa hao wa Ufaransa.

Mbappe ambaye pia aliisaidia Ufaransa kushinda kombe la Dunia alishinda taji la mchezaji bora wa mwaka katika Ligue 1 siku ya Jumapili.

Katika hotuba yake ya kupokea tuzo hiyo aligusia kuhusu “mradi wake mpya kwingine”.

Alipoambiwa afafanue tamko hilo, nyota huyo wa miaka 20 alisema: “Nimesema kile nilichotaka kusema.”

Katika taarifa kwa, PSG ilisema”Ushirikiano thabiti unaunganisha klabu hii na Mbappe”, ambaye alijiunga nayo kutoka Monaco mwaka 2017.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Kabla ya hapo aliichezea klabu hiyo kwa mkopo na baadae akapewa mkataba wa kudumu wa kima cha karibu euro milioni 166, kitita ambacho kilimfanya kuwa mchezaji wa pili ghali zaidi baada ya Neymar.

Ameifungia PSG mabao 59 katika mechi 86, kushinda ligi mara mbili na kombe moja la Ufaransa, lakini waliondolewa katika kinyang’anyiro cha Champion League na Manchester United.

Mbappe ni mfungaji bora wa mabaolatilaLigue 1 msimu huu akiwa na mabao 32.Source link

Sylvestre Ilukamba Waziri Mkuu mpya DRCIlukamba anachukuwa nafasi ya Bruno Tshibala aliyetumikia nafasi ya waziri mkuu tangu April 7 mwaka 2007, chini ya utawala wa rais mstaafu Joseph Kabila.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Reuters Ilukamba kabla ya uteuzi huu alikuwa Mkuu wa Kampuni ya Reli ya Taifa nchini Congo inayojulikana kama SNCC. Pia aliwahi kuwa Waziri wa Fedha wakati wa utawala wa Mobutu Sese Seko.

Wakati huo huo, maelfu ya watu Jumatatu wamemlaki kwa shangwe na vigelegele Moise Katumbi, mpinzani mkuu wa Rais mstaafu Joseph Kabila, alipowasili leo kwenye uwanja wa ndege mjini Lubumbabshi, akirejea nyumbani kutoka uhamishoni.

Katumbi mwenye umri wa miaka 54, mwanasiasa pia mfanyabiashara alikuwa gavana wa jimbo la Katanga kwa muda mrefu. Katumbi alikataliwa kushiriki kwenye uchaguzi wa Disemba mwaka 2018, baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 3 jela akiwa nje ya nchi.

Alikuwa anatuhumiwa kumiliki aridhi kinyume cha sheria, shutma ambazo alizikana. Lakini hukumu hiyo ilifutiliwa mbali na vyombo vya sheria vya DRC.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Washington, DC.Source link

Sylvestre Ilunga Ilunkamba achaguliwa waziri mkuu mpya DRC


HABARI ZA HIVI PUNDE

Rais Felix Tshisekedi amemteua Profesa Sylvestre Ilunga Ilunkamba kuwa waziri mkuu mpya katika Jamhuri ya Kidmeokrasi ya Congo.

Uteuzi huo umefanyika muda mfupi uliopita baada ya hapo awali waziri mkuu aliyekuwepo Bruno Tshibala, kujiuzulu.

Sylvestre amewahi kushikila nyadhifa tofuati serikalini.

Yeye ni mfuasi wa chama cha rais wa zamani nchini Congo Joseph Kabila – PPRD.

Raia wa Congo wamesubiri zaidi ya miezi mitatu, pasi kuwa na waziri mkuu mpya.

Mwanasisia huyu mwenye umri wa miaka 78 ambae pia ni miongini mwa viongizi wa chama cha Joseph Kabila, alikuwa mkurugenzi wa kampuni ya reli Congo.

Aliwahi kutumika chini ya utawala wa Mobutu Seseko kama mshauri wake wa maswali ya uchumi,

Tutakufahamisha zaidi kadri tunavyoendelea kuipokea taarifa hii.Source link

Uchaguzi Malawi: Mauaji ya Albino na taarifa za uongo za kifo cha rais Mutharika na mengineyo 5


Three main candidates

Haki miliki ya picha
AFP

Image caption

Rais Peter Mutharika (kulia) inakabiliwa na upinzani kutoka kwa Lazarus Chakwera (kushoto) na Saulos Chilima (kati)

Takriban raia milioni 7 nchini Malawi watapata fursa ya kumpigia kura rais mpya kesho Jumanne mei 21 katika uchaguzi ambao hauwezi kutabirika katika historia ya nchi hiyo.

1. Makamu wa rais asimama dhidi ya Rais

Maswali mengi kuhusu iwapo afya ya rais Peter Mutharika inamruhusu kugombea muhula mwingine umezusha mgawanyiko na makamu wake wa rais, Saulos Chilima.

Chilima aliteuliwa na rais Mutharika kama mgombea mwenza wake katika uchaguzi uliopita mnamo 2014. Lakini mwaka uliopita shemegi yake rais, Callista Mutharika, alipendekeza kwamba umri wa kiongozi huyo , miaka 78, ni mkubwa kwa yeye kuchagulia tena na kwamba sasa atoe fursa kwa makamu wake aliye na umri wa miaka 46.

Pendekezo hilo lilipingwa na wafuasi wenye ushawishi katika chama taala cha Democratic Progressive Party (DPP).

Kulizuka mgawanyiko wa chama hicho katika pande mbili na hatimaye Chilimaaliishia kuanzisha chama cha UTM, huku akisalia kuwa makamu wa rais nchini.

Haki miliki ya picha
AFP

Image caption

Inadhaniwa makamu wa rais Saulos Chilima ana umaarufu mkubwa miongoni mwa wapiga kura vijana nchini

haijulikani wazi iwapo Bi Mutharika wana sikizana na shemegi yake – hivi karibuni hakuhudhuria uzinduzi wa sanamu la marehemu mumewe Bingu wa Mutharika. Anagombea ubunge kupitia chama hicho cha makamu wa rais UTM.

Chilima anaonekana kama ishara ya mabadiliko kwa raia nchini Malawi wanaotamani mageuzi.

Umri mdogo wa Chilima huenda ukawana manufaa kwake, wakati raia walio na umri wa katiya miaka 18 na 34 wakiwa wanajumlisha 54% ya wapiga kura nchini.

2. Mke wa makamu wa rais ‘afoka’ kumtafutia mumewe kura

Mkewe Chilima, Mary, ameingia uwanjani akitafuta ushindi wa vijana kwa kuanza kuimba nyimbo za kufoka foka au rapa.

Katika kanda ya video, kando na kufoka, anadensi na kutumia mistari inayofahamika kwa vijana huku akionekana kuvaa nguo kama wao.

Amewasilisha pia matangazo ya biashara yanayowalenga wapiga kura wanawake.

Wagombea ni kina nani?

Wagombea saba wapo kwenye debe kaika uchaguzi wa urais Malawi, lakini watatu ndio wanaopigiwa upatu kuwa na nafasi ya kushinda:

  • Peter Mutharika – Democratic Progressive Party – rais wa sasa anayegombea muhula wa pili
  • Lazarus Chakwera – Malawi Congress Party – Anatumai kufufua utajiri wa chama tawala cha zamani
  • Saulos Chilima – UTM Party – makamu wa rais hivi sasa anayewania kiti dhidi ya mku wake

3. Hakuna wagombea wanawake wa urais

Licha ya kwamba wanawake ni 56% ya wpaiga kura nchini, hakuna mwanamke anayegombea urais nchini.

Haki miliki ya picha
AFP

Image caption

Wanawake ni zaidi ya nusu ya idadi ya wapiga kura nchini lakini hakuna mwanamke anayegombea katika uchaguzi mkuu

Rais wa zamani Joyce Banda, aliyeshndwa na Mutharika mnamo 2014, alijitoa katika kinyang’anyiro hicho kumuunga mkono Lazarus Chakwera wa chama cha Malawi Congress Party (MCP).

Uchaguzi wa ubunge na udiwani pia unafanyika kwa pamoja katika uchaguzi huuu. zaidi ya wanawake 300 wanagombea viti katika bunge la uwakilishi wa viti 153. Huku mamia wengine wakigombea katika viti vya serikali za mitaa.

‘Chanjo ya kwanza ya malaria’ kufanyiwa majaribio

Tanzania yawasaidia waathiriwa wa Kimbunga Idai

‘Anusurika kunyongwa mara tatu’

4. ‘Sijakufa’ asema Rais Mutharika

Takriban wiki moja ikiwa imesalia kwa uchaguzi mkuu kufanyika, kumekuwa na uvumi uliosabaa kwamba rais Mutharika huenda ni mgonjwa mahututi au amefariki. Hili lilifuatwa kwa taarifa kwa vyombo vya habari kutoka ofisini mwake iliosema kwamba anakatiza mikutano mingine ya kampeni ili “kushughulikia mambomengine muhimu zaidi”.

Picha ya ndege ya ambulensi ya Afrika kusini, iliyokuwa katika uwanja mkuu wandege wa nchi hiyo, ilianza kusamba aktika mitandao ya kijamii iliyoongeza chumvi uvumi huo.

Mutharika alizuka upya katika kampeni siku mbili baadaye na kuwakejeli upinzani.

Alisema kwamba badala ya yeye kufa, ni wapinzani ake watakaoteseka kwa kifo cha kisiasa uchaguzi utakapofika.

“Je nimekaa kama maiti kwenu?” aliwauliza wafuasi wake.

Kumeshuhudiwa ghasia kwa kiasi fulani lakini kwa ukubwa kampeni zimekuwa za amani.

Hakuna duru ya pili ya uchaguzi katika uchaguzi huo wa rais Malawi – mgombea atakayejinyakulia kura nyingi ndiye mshindi.

5. Mauaji ya walemavu wa ngozi – Albino

Suala jingine lililogubika kampeni nchin ini mfululizo wa mauajai ya watu wenye ulemavu wa ngozi – Albino- kufuatia kuwadia kwa uchaguzi mkuu.

Kuna wasiwasi kwamba huenda suala hilo likaharabu nafasi ya makamu wa rais.

Ripoti ya Umoja wa matiafa imeashiria kwamba mashambulio na mauaji ya walemavu wa ngozi huongezeka wakati wa uchaguzi “kutokanana imani potofu kwamba viungo vya walemavu vinaweza kuleta bahati nzuri na nguvu za kisiasa na hutumika katika visa vya uchawi”.

Vyama vya upinzan vinautuhumu utawala wa Mutharika kwa kutowajibika ipasavyo kusitisha mashambulio hayo.

Rais analikana hilo na ameunda tume ya uchunguzi, kuchunguza mauaji hayo.Source link

Meli ya Saudia iliyozuiliwa kupakia silaha Ufaransa yawasili ItaliaKundi dogo la waandamanaji limekusanyika bandarini, wakiwa wamebeba mabango yaliyo na ujumbe wa kulaani vita inayoendelea nchini Yemen.

Ijumaa (Mei 10, 2019) makundi ya kutetea haki za binadamu yalikusanyika wakishinikiza meli ya Bahri – Yanbu izuiliwe kupakia silaha katika bandari ya La Havre, ya Ufaransa.

Makundi hayo yamejitokeza kupinga usafirishaji wa silaha hizo kutokana na wasiwasi uliokuwepo hivi sasa kwamba silaha hizo zitatumika na Saudi Arabia dhidi ya raia wasio kuwa na hatia katika vita inayoendelea nchini Yemen.

Meli hiyo ya Bahri-Yanbu, ambayo imebeba shehena nyingine ya silaha iliyopakiwa Antwerp, inatarajiwa kuondoka Italia, kuelekea Jeddah, Saudi Arabia, baadaye Jumatatu.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Washington, DC.Source link

Massimiliano Allegri aihama Juventus


Lakini wanampoteza kocha wao Massimiliano Allegri ambaye anaondoka baada ya kuhudumu kama mkufunzi kwa kipindi cha miaka mitano.

Allegri mwenye umri wa miaka hamsini na moja anasema lakini kuwa anaondoka ila hana kinyongo na yeyote.

“Tumezungumza na wakuu wa klabu na tukaelezana kile kilicho bora kwa Juventus na mustakabali wake. Baada ya hapo wakuu wakaitathmini hali nzima na ikaamuliwa ni vyema kwamba nisiwe kocha wa klabu hii msimu ujao. Hili halibadilishi chochote kwasababu hali ya maelewani na Rais Agnelli, wakurugenzi Pavel Nedved na Fabio paratici bado yanasalia kuwa mazuri kabisa,” alisema Allgeri.Source link

Mbappe adokeza huenda akaihama PSG


Mbappe alishinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka na mchezaji bora mwenye umri mdogo.

Lakini ameonyesha mashaka iwapo ataendelea kuwa mchezaji wa PSG msimu ujao licha ya kuthibitisha mwezi Machi kwamba hataihama klabu hiyo ya Ufaransa.

Mbappe amesema amefikia sehemu katika taaluma yake ya soka sasa ambapo anaanza kupata ufanisi na anatarajia kuendelea hivyo iwe ni hapo PSG au katika klabu nyengine Ulaya.Source link