Paul Pogba: Kiungo wa Manchester United asema 'hana haja' ya kuongea na waandishi


Manchester United celebrate

Mchezaji ghali zaidi kwenye kikosi cha Manchester United Paul Pogba amegoma kuongea na waandishi baada ya timu yake kuifunga Perth Glory ta Australia 2-0.

Mchezo huo ni wa kwanza kwa United katika kampeniyake ya kujiandaa na msimu ujao wa ligi.

Magoli ya ipindi cha pili kutoka kwa Marcus Rashford na James Garner yalitosha kwa Man United kutoka na vicheko kwenye uwanja wa Optus nchini Australia.

Pogba alitoa pasi iliyozaa goli la Rashford.

Huu ulikuwa mchezo wa kwanza kwa Pogba akiwa na United toka alipotangaza nia yake ya kutaka kuondoka kwenye kikosi hicho.

Nia hiyo ya Pogba imesharejelewa mara mbili na wakala wake Mino Raiola katika siku za hivi karibuni.

Kiungo huyo aligoma kuongea na maripota baada ya mchezo akisema “hakuna haja” ya kufanya hivyo.

Vilabu vya Real Madrid na Juventus vinaripotiwa kutaka kumsajili kiungo huyo Mfaransa mwenye miaka 26 japo hakuna kati yao ambaye amepeleka maombi rasmi ya kutaka kumnunua.

Haki miliki ya picha
Getty Images

United inaaminika itataka kulipwa pauni milioni 150 ili kumuachia Pogba aende zake.

Pogba hakupewa kitambaa cha unahodha kwenye mchezo huo na kuvaliwa na Juan Mata, japo kocha wa United Ole Gunnar Solskjaer alisema kabla kuwa mchezaji huyo anaweza kupewa majukumu ya unahodha msimu huu.

“Sidhani kama jambo hilo linahitaji kutolewa maelezo, tutalijadili baadae,” alisema Solskjaer alipoulizwa kuhusu hatima ya unahodha kwa Pogba.

Kuhusu uhamisho, Solskjaer amesema kuwa klabu hiyo haijapokea ofa yoyote ya wanaomtaka Pogba ama mshambuliaji wa Ubelgiji Romelo Lukaku, “tusubiri kuona msimu utakavyoanaza,” alisisitiza Solkjaer.

Huwezi kusikiliza tena

Paul Pogba akishangilia goli lake la kubahatisha na la ‘maumivu’

‘Mzozo’ wa Pogba

Pogba alisema mwezi Juni kuwa ”sasa inaweza kuwa muda mzuri wa kuhamia sehemu nyingine”.

Ni dhahiri kuwa si Solskjaer wala uongozi wa Man United unaotaka mchezaji huyo nyota kuondoka Old Trafford katika dirisha hili la usajili la majira ya joto.

Wiki iliyopita, wakala wa mchezaji huyo Raiola aliliambia gazeti la The times kuwa mchezaji wake anataka kuondoka, na klabu hiyo inajua fika nia ya mteja wake.

“Mchezaji (Pogba) hakufanya kosa lolote,” Raiola aliuambia mtandao wa Talksport.

“Amekuwa na heshima na weledi. Klabu imekuwa ikijua hisia zake kwa muda mrefu.

“Ni aibu kuwa kuna baadhi ya watu wanapenda kukosoa bila ya kuwa na taarifa sahihi, na ninasikitishwa kuwa klabu haichukui hatua yoyote kwa wanaofanya hivyo.”

Hata hivyo, kocha Solskjaer anaamini kuna ajenda dhidi ya mchezaji huyo.

”Ni ajenda dhidi ya Paul, ni mchezaji mzuri, mzuri sana, hakujawahi kuwa na shida, ana moyo wa dhahabu,” alisema kocha huyo.

”Paul hakuwahi kujiweka nje ya timu, mara zote amekuwa akitoa mchango wake mzuri na siwezi kuripoti chochote , isipokuwa maneni ya mawakala ya wakati wote.

”Siwezi kukaa hapa kumzungumzia Paul na kila wanachokisema mawakala, tuna miaka michache iliyobaki kwenye mkataba wake na ni mchezaji mzuri.”Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *