Pompeii: Wanaakiolojia wavumbua miili ya mtu tajiri na maskini ya miaka 2,000 iliyopita


Two bodies discovered in Pompeii, Italy

Maelezo ya picha,

Uvumbuzi huo ulibainika katika eneo kubwa la kifahari viungani nwa mji wa kale wa Roma

Wanaakiolojia au wachimbuzi wa vitu vya kale wamebaini mabaki ya wanaume wawili waliofariki dunia katika mlipuko wa volkeno ulioharibu mji wa kale wa Roma wa Pompeii karibu miaka 2,000 iliyopita.

Bila shaka alikuwa mwanaume wa ngazi ya juu huku mwingine akiwa mtumwa, maafisa katika bustani ya akiolojia ya Pompeii wamesema.

Pengine “walikuwa wanatafuta hifadhi” kutoka eneo la mlipuko” walipolipuliwa na mlipuko huo”, mkurugenzi Massimo Osanna aliongeza.

Mji wa Pompeii ulikumbwa na mlipuko wa volkeni kutoka Mlima Vesuvius katika mwaka AD 79.

Mlipuko huo ulifunika mji wa Pompeii kwa jivu, ukasitisha shughuli za mji na wakazi wake na kuufanya kuwa chanzo muhimu cha wanaakiolojia.

Uvumbuzi wa hivi karibuni ulibainika mwezi huu wakati wa shughuli ya uchimbaji katika eneo kubwa la kifahari viungani nwa mji wa kale.

Maafisa wamesema mwanaume tajiri alikuwa na umri katika 30 na 40 ambaye alipatikana akiwa na nguo ya kifahari ya kujikinga baridi chini ya shingo yake.

Mwanaume mwingine aalisemekana kuwa kati ya umri wa miaka 18 na 23. Maafisa katika eneo la akiolojia walisema mfupa uliokuwa umevunjika katika mwili wa kijana huyo uliashiria kwamba alikuwa mtumwa aliyefanya kazi za mkono.

Miili yao ilikuwa imefanya kama matabaka na kuonesha kuwa miili hiyo ilikuwa imeingia kwenye jivu.

Aidha, maafisa wameelezea uvumbuzi huo kuwa wa kipekee wa wakati mlipuko unaotekea.

Shughuli ya uchimbaji katika eneo la akiolojia unaendelea ingawa bado limefungwa kwa ajili ya watalii kwasababu ya virusi vya corona.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *