Raia wa Korea Kaskazini aingia eneo la kijeshi la Korea Kusini mfumo wao wa kiusalama ukionesha hitilafu


DMZ file image

Maelezo ya picha,

Kupita kwenye eneo lisilo na shughuli za kijeshi (DMZ) kutoroka ni nadra na ni hatari

Vikosi vya Korea Kusini vimeshindwa kumgundua mwanamume wa Korea Kaskazini aliyevuka mpaka na kuingia upende wa Korea Kusini unaolindwa vikali mwezi huu hata baada ya kuonekana kwenye kamera za televisheni mara nane na kuzua taharuki.

Jeshi la Korea Kusini limesema litachukulia tukio hilo kama hitaji la kufanyika mabadiliko ya kiusalama haraka iwezekanavyo.

Mwanamume huyo aliogelea na kutoka baharini akiwa na suti yenye maji, na kutembea umbali wa kilomita 5 na kuwa katika eneo hilo kwa saa tatu bila kugundulika kabla ya wanajeshi hatimaye kuchukua hatua alipojitokeza kwa mara ya 9.

Bado haijafahamika kwanini aliamua kuvuka katika eneo hatari namna hiyo.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *