Rais Biden ameomboleza vifo vya wamarekani Laki tano kutokana na CoronaRais wa Marekani Joe Biden, Jumatatu jioni alitembea kwenye upande wa pili wa jengo la White House uliopambwa kwa bendera nyeusi pamoja na mishumaa 500 ikiwa ishara wakati taifa linaomboleza vifo laki tano kwa sababu ya COVID-19.

Pembeni ya Rais Biden alikuwepo mkewe Jill Biden na Makamu Rais Kamala Harris pamoja na mumewe Doug Emhoff. Wote walisimama kimya wakati bendi ya Marine Corps ikipiga wimbo wa “Amazing Grace”.

Muziki ulipomalizika Rais Biden ambaye ni mkatoliki muumini mwenye kawaida ya kwenda kanisani alitoa ishara ya msalaba. Dakika chache kabla, kwenye ukumbi wa Cross Hall ghorofa ya kwanza ya White House, Rais Biden alitoa wito kwa taifa kuungana nae katika wakati wa ukimya katika sauti ya chini sana alielekeza matamshi kwa wale ambao wamepoteza wapendwa wao kutokana na virusi vya COVID-19.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *