Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Felix Tshisekedi na wa Uganda Yoweri Museveni waweka mifumo madhubuti ya ushirikiano


Wizara ya mambo ya nje Uganda

Haki miliki ya picha
Wizara ya mambo ya nje Uganda

Image caption

Rais Felix Tshisekedi amekuwa kwenye ziara ya siku mbili nchini Uganda kujadili ushirkiano wa miongoni mwa mengine kibiashara na usalama

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Felix Tshisekedi yuko kwenye ziara ya siku mbili nchini Uganda kwa ajili ya kuhudhulia mkutano wa kibiashara wa mwaka 2019.

Wizara ya mambo ya nje nchini Uganda imetoa maelezo kuwa wakuu wa mataifa hayo mawili wamekutana ili kukamilisha mkakati wa kushirikiana katika masuala ya afya, amani na usalama, nishani ,biashara na uwekezaji pamoja na masuala mengine ya maendeleo.

Katika suala la usalama na amani ambayo ni changamoto kubwa kwa mataifa hayo mawili, viongozi hao wameazimia kutafuta suluhu ya kuyangamiza makundi ya wapiganaji na waasi mashariki mwa Kongo.

Marais hao wanamini kuwa hiyo ndiyo itakuwa hatua ya kwanza kuleta maendeleo ya viwanda, biashara na uwekezaji eneo hilo.

Viongozi hao wametoa mwito kwa wenzao katika kanda ya maziwa makuu kuunga mkono juhudi zao.

Baada ya kukutana kwa siku nne, ujumbe wa DRC uliojumuisha maafisa wa ngazi za juu pamoja na wawakilishi 110 wa wafanyabiashara, waliorodhesha na wenzao wa Uganda masuala ambayo waliyataka viongozi wayazingatia ili kuimarisha biashara kati ya nchi hizo mbili.

Masuala mawili yaliyosisitizwa ni usalama na miundobinu ya barabara.

Haki miliki ya picha
Wizara ya mambo ya nje Uganda

Walipopokea masuala hayo, marais Museveni na Tshishekedi waliahidi kuanzisha operesheni kabambe kuangamiza makundi ya wapiganaji Mashariki mwa Congo.

Hii wameeleza viongozi hao itatoa fursa kwa wafanyabiashara kutoka pande zote mbili kuendesha shughuli zao na kwa hiyo kuchangia kwa amani, usalama na uthabiti eneo hilo.

Kadhalika Rais wa Congo amefichua azimio lake la kuligeuza eneo la mashariki mwa nchi yake kuwa ndicho kitovu cha viwanda.

Amebaini maeneo sita ambayo yanalengwa ili kulifanikisha hilo na pia katika biashara na uwekezaji sambamba na kujenga barabara za moja kwa moja kutoka Uganda badala ya kutegemea tu zile zinazopitia Rwanda.

Kulingana na takwimu za serikali, Uganda iliuza bidhaa za thamani ya dola milioni 538 kwa nchi ya Congo huku nchi hiyo yenye utajiri mkubwa wa madini na mbao iliuzia Uganda dola milioni 117.

Baadhi ya wafanyabiashara wametaja ushuru, michakato ya uhamiaji ikiwemo ada za Viza za usafiri na pia barabara kuwa changamoto zinazostahili kupewa kipaumbele ili kuboresha biashara kati ya Uganda na DRC.

Biashara ambazo zinatarajiwa kufanywa na mataifa hayo mawili zinakadiriwa kuwa milioni 532 kwa mujibu wa ofisi ya taifa ya takwimu Uganda.

Waziri wa mambo ya nje wa Uganda anasema kuwa ushirikiano huo ni mzuri kwa kuwa unazipa nchi hizo mbili wigo mkubwa wa kukua kimaendeleo na kufanya kazi pamoja.

Amani mashariki ya DRC

Ingawa maeneo karibu yote ya DRC yamekuwa yakikumbwa na changamoto za usalama kama vita ama kushambuliwa na waasi mara kwa mara, eneo la mashariki ya nchi hiyo ndiyo lililoathirika zaidi.

Akiongea na BBC siku chache kabla ya kuondoka madarakani mwishoni mwa maka 2018, rais mataafu wa nchi hiyo, Joseph Kabila amesema katika mambo ambayo angekuwa na muda zaidi kuyashughulikia ni kurudisha amani kwa taifa hilo.

Mashariki mwa DRC kuna makundi ya kijeshi ya waasi na kikabila mengi kupindukia.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Baadhi ya makundi yanaundwa na raia wa nchi hiyo, lakini kuna makundi mengine makubwa ambayo yanafadhiliwa ama kupambana za serikali za nchi jirani.

Baadhi ya makundi ya waasi yanayotokea nchi jirani ni FDLR ambalo lilitekeleza mauaji ya kimbari nchini Rwanda mwaka 1994 na wapiganaji wake kukimbilia DRC.

Waasi wa ADF wanatokea nchini Uganda.

Makundi hayo ya waasi yanatumia misitu mizito iliyopo kwenye eneo hilo kujificha na kuendesha shughuli zao huku wakitangaza nia ya kushambulia nchi zao walizozikimbia.

Uganda na Rwanda zimeshavamia DRC mara mbili kwa lengo la kusambaratisha makundi hayo na vita hivyo kupelekea mamilioni ya watu kufariki.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Vikosi vya kulinda amani chini ya Umoja wa Mataifa (UN) vipo mashariki ya DRC

Eneo hilo la Mashariki ya DRC pia linakabiliwa na ugonjwa hatari wa Ebola ambapo moja ya sababu za kushindikana kushughulikiwa kikamilifu ni uwepo wa makundi ya waasi hao.

Mwezi Machi mwaka huu shirika la habari la kimataifa la Reuters liliripoti kuwa, kundi la waasi la Mai Mai lilishambulia kambi ya matibabu ya Ebola na kuua polisi na kufurusha wagonjwa na wahudumu wote wa afya.

Makundi hayo pia yamekuwa pia yakishutumiwa kwa ubakaji wa wanawake katika maeneo wanayoyashambulia, na kufanya ubakaji kuwa ni moja ya matatizo makubwa yanayolikumba eneo hilo.

Uwepo wa makundi hayo ya waasi yamefanya Umoja wa Mataifa kupeleka kikosi maalumu (MONUSCO) kulinda amani. Hata hivyo, wachambuzi wengi wamekuwa wakilaumu vikosi hivyo kwa kushindwa kutekeleza wajibu wake ipasavyo.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *