Ralf Rangnick: Manchester United inajiandaa kumteua Mjerumani huyu kuwa kocha wa mpito


Ralf Rangnick:

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Ralf Rangnick:

Manchester United inakaribia kumteua Ralf Rangnick kuwa meneja wao wa muda mfupi kwa mkataba wa miezi sita.

Mjerumani huyo mwenye umri wa miaka 63 anatarajiwa kujiunga na United lakini hataiongoza timu hiyo katika mchezo wa mwishoni mwa wiki dhidi ya Chelsea, wakati huu akisubiri kibali chake cha kazi.

United wameshamalizana na Rangnick, lakini hawajamalizana na Lokomotiv Moscow, ambako Mjerumani huyo anafanya kazi kama Mkuu wa masuala ya michezo na maendeleo.

Rangnick anatua baada ya United kumfukuza kazi Ole Gunnar Solskjaer Jumapili iliyopita kufuatia kuiongoza timu hiyo miaka mitatu bila kombe.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *