Ramadhan: Kanisa moja Ujerumani limefungua milango kwa Waislamu kusali


Haki miliki ya picha
Reuters

Kanisa moja kubwa mjini Berlin limefungua milango kwa ajili ya Waislamu kusali kwasababu hawawezi kutosha msikitini wakifuata utaratibu mpya wa kutokaribiana.

Ujerumani iliruhusu sehemu za kuabudiwa kufunguliwa Mei 4, lakini kwa masharti kuwa watu wakae kwa umbali wa mita 1.5 (5ft).

Na hii kupelekea msikiti wa Dar Assalam uliopo mjini Neuk├Âlln kushindwa kumudu vigezo hivyo kwa sababu hauwezi kutosha.

Lakini kanisa la Kilutheri la Martha katika mji wa Kreuzberg lilitoa ruhusa kwa Waislamu kufanya ibada zao Ijumaa na katika wiki ya mwisho ya mfungo wa Ramadhani.

Kwa kipindi cha mwezi mzima wa Ramadhan, Waislamu wamekuwa wakijinyima kula, kunywa, kuvuta sigara na ngono kuanzia alfajiri hadi jioni.

Kwa kawaida familia na marafiki huwa wanajumuika kwa pamoja kuhitimisha mfungo kwa kusheherekea na kujumuika katika sala za pamoja, lakini kwa mjini Berlin – na hata maeneo mengi duniani sherehe hizo bado zimeathirika.

Haki miliki ya picha
Reuters

“Ni ishara njema na inaleta furaha kwa wakati huu wa Ramadhan na inaleta furaha katikati ya janga,” Imamu mmoja aameliambia shirikala habari la Reuters. “Mlipuko huu umetufanya kuwa jumuiya moja. Majanga yamewafanya watu wawe kitu kimoja.”

“Ni hisia ya ajabu kwa sababu ya ala za muziki na picha za ukutani ni kitu tofauti,” alisema muumini mmoja, Samer Hamdoun, hakuna kitu ambacho kinawakilisha swala za kiislamu.”

“Lakini unapoangalia, unaposahau kidogo. Hii ni nyumba ya Mungu.”

Haki miliki ya picha
Reuters

Hata wachungaji wa kanisa wamehudhuria swala hizo.

“Nilitoa hotuba Ujerumani,” alisema Monika Matthias. “wakati wa maombi, nilikuwa naweza kusema ndio, ndio, ndio kwasababu tunamatatzio ya kufanan na tunataka kujifunza kutoka kwenu. Na hisia hiyo ni nzuri kati yetu.”

Haki miliki ya picha
Reuters

Pia unaweza kutazama:

Huwezi kusikiliza tena

Je, utasali vipi sala ya Idi ukiwa nyumbani?Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *