Richard Tongi: Mbunge wa Kenya aliyerejea India kulipa deni alilokopeshwa miaka 30 iliyopita akiwa mwanafunzi


Haki miliki ya picha
RICHARD TONGI / RAVIKANT GAVLI

Image caption

Richard Tongi na Kashinath Gawali

Kashinath Gavali, 75, makaazi wa Wankhedenagar katika mji wa Aurangabad nchi India alipata umaarufu miongoni mwa wanafunzi kutokana na biashara yake ambayo ilikuwa mkombozi kwa baadhi ya wanafunzi waliokuwa wakiishi karibu.

Richard Nyagka Tongi alikuwa mmoja wa wanafunzi kama hao.

Richard alikuja alitembelea Aurangabad kutoka Kenya mwaka 1985 na alikuwa akiishi katika nyumba ya kukodisha karibu na duka la Gavali.

Mara nyingi hakupokea pesa alizotumiwa na familia yake kutyoka Kenya kwa muda aliyotarajia. Kutokana na hilo wakati mwingine alilazimika kukopa vitu vya matumizi kutoka kwa duka la Gavali.

Kashinath Gavali pia alimkopesha Richard na vitu kama maziwa, mkate, siagi na bidhaa zingine bila hofu yoyote.

Richard alirejea Kenya mwaka 1989 baada ya kukamilisha masomo yake lakini kila akifanya hesabu ya vitu vyake vya matumizi alikuwa akilikumbuka deni la Rupee 200 la Gavali na muda wote amekuwa akitamani kulilipa.

Lakini mambo yalibadilika na Richard akajiunga na siasa za Kenya ambapo alichaguliwa kuwa mwakilishi katika mbunge la nchi hiyo.

Hata baada ya hadi yake kupanda katika jamii alikumbuka deni la Gavali.

Wakati mwingine angelimwambia mke wake, ‘Nitakutana vipi na Mungu wangu kama siwezi kulipa deni.’ Pia aliomba apate nafasi ya kurudi tena India.

Haki miliki ya picha
RAVIKANT GAVALI

Image caption

Richard Tongi na fami,lia ya Kashinath Gawali

Kurejea India, baada ya miaka 30

Hatimae miaka 30 baadae, Richard alipata fursa hiyo wiki iliyopita.

Richard ambaye ni naibu mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na masuala ya kigeni katika bunge la Kenya hivi karibuni alizuru taifa hilo kama sehemu ya ujumbe wa Kenya.

Baada ya kukamililisha kazi yake rasmi mjini Delhi alitembelea eneo la Aurangabad siku ya Jumapili akiwqa ameandamana ma mke wake ambaye ni daktari kutafuta nyumba ya Bw Gavali katika mtaa wa Wankhedenagar.

Mtaa huo ulikuwa umebadilika kabisa na kile alichokumbuka kuhmhusu muhisani wake ni jina la- ‘Gavali’.

Na jina lenyewe alilitamka visivyo ‘Gavaya’, badala ya ‘Gavali’ kwa hivyo watu hawakufahamu anamtafuta nani haswa.

Lakini alipoelezea jinsi Gavali alivyopenda kuvaa vazi la fulana iliyofahamika kama ‘banyan’ kila mmoja alimtambua.

Kwa bahati nzuri mmoja wa watu Richard aliyekuwa akisema nao alikuwa Kashinath binamu wa Gavali, na alikubali kumpeleka hadi nyumbani kwake.

Haki miliki ya picha
RAVIKANT GAVALI

Jumapili moja kama mwendo wa saa moja jioni, Kashinatha alirejea nyumbani kujiandaa kwa chakula cha jioni kama ada yake, mwanawe wa kiume Nandkumar alimuita na kumfahamisha kuna mtu anaomba kukutana nae.

Lakini, Kashinath aliamua kukutana na wageni hao baada ya kula, kwa hiyo alishuka chini dukani baada ya kama dakika 15-20.

Alipofika alimuona mtu raia wa Kigeni wa mri wa makamo akimsubiri katika duka lake.

Mtu huyo alikuwa ameandamana na mwanamka na Kashinath alishangaa na kujiuliza ni kina nani.

Wote wawili walianza kububujikwa na machozi walipomuona Kashinath na kwa karibu dakika saba hawakuweza kusema lolote bali walilia kila walipomuangalia Bw. Gavali.

Gavali hakuweza kumkumbuka mtu huyo na alionekana kuchanganyikiwa japo tukio hilo lilimgusa sana

Na mtu huyo wa umri wa makamo aliyejitambulisha kama, Kashinath Gavali alikumbuka kila kitu.

Haki miliki ya picha
RAVIKANT GAVALI

Richard na Kashinath walifurahi kukutana tena baada ya miaka mingi.

Wawili hao walijumuika pamoja kwa karibu saa tatu na katikati mazungumzo yao Richard alimfahamisha Kashinath kuwa anadeni lake la Rupee. 200.

Kisha akamkabidhi euro 250, Lakini Kashinath alikataa kuzipokea pesa hizo na kuongeza kuwa amefurahishwa sana na hatua ya Richard kumtembelea. Lakini, Richard alimsisitizia kuzipokea .

Richard alisema, “Ulinisaidia nikiwa katika hali ngumu zama hizo. Siwezi kusahau wema wako. Mimi ni mwana wa mkulima. Siwezi kuishi bila kulipa deni la mtu. Natawezaje kukutana na Mola wangu kama sitaweza kulipa deni lako?”

Kashinath alibubujikwa na machozi aliposikia manenoi hayo. Na baadae kupokea pesa hizo. Richard hatimae aliialika familia ya Kashinath Kenya na kuondoka.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *