Ripoti: Iran inashinda mapambano ya kimikakati ya ushawishi katika Mashariki ya Kati dhidi ya mpinzani wake – Saudi Arabia


Jeshi kuu la Iran [Islamic Revolution Guard Corps] IRGC linakadiriwa kuwa zaidi ya 150,000 ambao wanahudimia taifa

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Jeshi kuu la Iran [Islamic Revolution Guard Corps] IRGC linakadiriwa kuwa na maafisa zaidi ya 150,000 ambao wanahudimia taifa

Iran inashinda mapambano ya kimikakati ya ushawishi katika Mashariki ya Kati dhidi ya mpinzani wake, Saudi Arabia, kwa mujibu wa ripoti mpya ya taasisi ya kimataifa ya mafunzo ya kimikakati iliyo na makao yake mjini London.

Mahasimu wa kikanda wa Iran wametumia mabilioni ya dola kununua silaha katika mataifa ya magharibi hususan kutoka Uingereza.

Japo Iran inakabiliwa na vikwazo, imetumia sehemu ndogo ya fedha hizo kujiimarisha ushawishi wake katika eneo la mashariki ya kati.

Ina ushawishi mkubwa – kwa kudhibiti mzozo unaoendelea katika mataifa ya- Syria, Lebanon, Iraq na Yemen.

‘Kuongeza mkondo wa usawa

Hatua ya Iran kubuni mtandao wa ushirikiano usiokuwa ya serikali kote Mashariki ya Kati, ambayo mara nyingi huitwa “wanamgambo wakala”, sio jambo geni.

Kupitia matandao wa Hezbollah nchini Lebanon, taifa hilo la Kiislamu limekuwa likieneza falsafa ya mageuzi na kutanua wigo wake nje ya mipaka yake tangu kiongozi wa kidini Ayatollah Ruhollah Khomeini aliporejea mjini Tehran mwaka 1979.

Lakini ripoti hiyo ya IISS ya kurasa 217 inayofahamika kama “Mitandao ya Ushawishi ya Irani Mashariki ya Kati”, inaangazia kwa kina ushawishi wa Iran katika eneo la mashariki ya kati.

“Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran,” inasema ripoti hiyo, “imedhihirisha utenda kazi wa kikosi chakeMashariki ya kati.” Imefikia hilo, waandaji wa ripoti hiyo wanasema.

Kiungo muhimu katika mapambano ya kimikakati ya ushawishi huo ni vikosi vya Kikurdi, ambavyo vinaendesha oparesheni yake kwa ushirikiano na jeshi la ulinzi la Iran.

Vikosi vya Kikurdi na kiongozi wake, Maj Gen Qasem Soleimani, vinafanya kazi chini ya kiongozi mkuu wa kidini, Ayatollah Ali Khamanei, badala ya kufuata muundo wa kawaida wa kijeshi wa Iran.

Haki miliki ya picha
AFP

Image caption

Maj Gen Qasem Soleimani akiongoza vikosi vya Kikurdi

Tangu Marekani ilipovamiwa kijeshi Iran na kuung’oa madarakani utawala wa Saddam Hussein mwaka 2003, vikosi vya kikurdi vimeimarisha oparesheni yake katika eneo karibu lote la mashariki ya kati, kwa kutoa mafunzo, kufadhili ununuzi wa silaha kwa mataifa yaliyo na ufungamano na Tehran.

Mwezi April, rais wa Marekani Donald Trump aliorodhesha jeshi la IRGC, ikiwemo vikosi vya Kikurdi kuwa “shirika la kigaidi la kigeni” (FTO).

Ilikuwa mara ya kwanza Marekani kutaja sehemu ya serikali nyingine kama shirika la kigaidi la kigeni.

Iran ilijibu madai hayo ya Trump kwa kutaja vikosi vya Marekani katika eneo la Ghuba kuwa kundi la kigaidi kama hatua ya kulipiza kisasi.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Wafuasi wa Hezbollah mjini Beirut wakionesha picha ya kiongozi mkuu wa kidini Ayatollah Ali Khamenei

Jack Straw, ambaye alikuwa waziri mambo ya nje wa Uingereza kutoka 2001 hadi 2006 na ambaye alizuru Iran mara kadhaa, anaamini kuwa jukumu la Jenerali Soleimani ni zaidi ya kamanda wa jeshi.

“Qasem Soleimani amekuwa akiendesha sera zao za katika kanda hiyo kigeni kupitia ushirikiano unaungwa mkono na vikosi vyake,” anasema.

Kujibu yalioibuka katika ripoti ya IISS, msemaji wa ubalozi wa Iran mjini London aliambia BBC: “Ikiwa ripoti imesema hivyo basi jukumu la Iran katika kanda ya mashariki ya kati lazima liheshimiwe, tamko ambalo linaashiria imeunga mkono ripoti hiyo.

“Sera ya kuipuuza Iran haikufanya kazi. Iran ilikataa. Iran pia ilidhibiti vikwazo vya kiuchumi vya Marekani. Kwa hivyo ni kweli kwamba ni taifa lenye nguvu, na ambalo linashirikiana na mataifa mengine katika miradi inayolenga kuboresha ushirikiano

Hezbollah – ‘washirika wadogo

Vuguvugu la waislamu wa dhehebu la kishia nchini Lebanon, Hezbollah, ambalo ni chama cha kisiasa na wanamgambo waliojihami, “limejenga hadhi yake na kupata uungwaji mkono kutoka kwa washirika wa Iran”, inasema ripoti hiyo, ambayo imeangazia kwa kina ushawishi wa Iran nchini Syria na Iraq.

Hezbollah ilitekeleza jukumu muhimu katika machafuko ya nchi hizo zote mbili, ikipigana na vikosi vya Syria vilivyoaminifu kwa Rais Bashar al-Assad na kusaidia wanamgambo wa Shia ya Iraq.

Japo ripoti hiyo imeiorodhesha Hezbollah kama “washirika wadogo ambao ni washirika waaminifu na ndugu wa dhati katika vita vya chini kwa chini vya Iran “. wa kikanda.”

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Kitengo maarufu cha Popular Mobilisation Units (PMU) kilishirikiana na vikosi vya Iraqi kupambana na kundi la kigaidi la Islamic State

Kuingilia Iraq na Syria

Uvamizi wa kijeshi wa Marekani nchini Iraq na baadae kung’olewa mamlakani kwa utawala wa Saddam Hussein ulibadilisha kabisa mtizamo wa Mashariki ya kati dhidi ya Marekani.

Kabla ya hatua hiyo, mataifa ya kiarabu katika eneo la Ghuba yalichukulia utawala wa Waarabu wa dhehebu la Kisuni kama kiungo kinachohujumu sera ya Iran ya kujiimarikasha kama Jumuia ya nchi za Kiarabu.

Baada ya suala hilo kutoweka, Iran ilifanikiwa ilitumia uhusiano wake wa kitamaduni na kidini ndani ya Iraq – ambayo ina idadi kubwa ya waumini wa Kiislamu wa dhehebu la Kishia – kumarisha ushawishi wake nchini humo.

Iran ingependa sana kama Marekani, kuwa na nguvu ya kijeshi katika eneo la Mashariki ya kati.

Mataifa ya Saudi Arabia, Bahrain na Falme ya Milki za Kiarabu (UAE), hayana nia ya kuruhusu jambo hilo lifanyike.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *