Rusty Hutson: Mwanamume aliyekuwa milionea kwa kununua visima 60,000 vya mafuta na gesi


Rusty Hutson

Haki miliki ya picha
Billy Brown

Image caption

Rusty Hutson awali hakutaka kufanya kazi katika sekta ya kawi

Rusty Hutson awali hakupendelea kufanya kazi katika sekta ya kawi.

Hatahivyo mwishowe Hutson hakuweza kukaidi wito wa kibiashara wa familia yake.

Akiwa mzaliwa katika mtaa wa vibarua katika visima vya mafuta vya West Virginia , babake , babu yake na babake mkubwa wote walijipatia kipato chao katika sekta ya kawi.

Walifanya kazi katika visima vya mafuta, na katika mabomba ya kusafirishia mafuta wakifanya kazi ngumu , siku baada ya siku , mwaka baada ya mwaka ili kukuza familia zao.

Wakati wa likizo ya msimu wa joto alipotoka shule na katika taasisi , Hutson alikuwa akienda kazini na babake.

lakini alipokuwa wa kwanza kufuzu katika chuo kikuu 1991, aliamua alitaka kufanya kitu tofauti kabisa na maisha yake.

Haki miliki ya picha
DGO

Image caption

Rusty, wa tatu kushoto, sasa anawaajiri watu 925

”Nimeamua kwenda katika kisima cha mafuta na gesi ndio kitu cha mwisho nilichotaka kufanya”,anasema.

”Sikutaka hata chembe cha kazi hiyo nilipotoka shule. Ni kazi ngumu sana”.

Hivyobasi akiwa na shahada yake kutoka chuo kikuu cha Virginia fairmont State University alienda kufanya kazi ya benki kwa muongo mmoja akimalizia Birmingham, Alabama.

lakini huku miaka ikisonga mbele , Hutson anasema kwamba alianza kutekwa na mawazoi ya kutosikiza ushauri wa babake wa kuingia katika kiwanda cha familia.

West Virgia ilikuwa jimbo gumu wakati nilipokuwa kijana.

Na kulikuwa na watu aina mbili- wafanyakazi wa mkaa ama wafanyakazi wa sekta ya mafuta na gesi.

lilikuwa jambo la jumla – iwapo babako na babu yako walifanya kazi ili kujipatia kipato basi kulikuwa hakuna sababu ya wewe kutofanya kazi kama hiyo.

Na huku miaka ikisonga mbele , nilizidi kuhisi kuvutiwa na sekta hiyo ya kazi. Pia nilikuwa na hamu ya kujenga kitu na kufanya kitu cha kibiashara.

Hivyobasi ilipofikia mwaka 2001, nikiwa na umri wa miaka 32, Hutson alinunua kisima kimoja cha zamani cha gesi katika eneo la West Virginia kwa $250,000.

Alichangisha fedha hizo kwa kuuza nyumba yake.

”Kilikuwa kisima kidogo na cha zamani , kilikuwa kikizalisha mafuta kwa miaka mitano, lakini kilikuwa kama dhahabu kwangu mie”, alisema.

Nilihudumu miaka minne iliofuata nikiwa mfanyakazi wa benki, lakini nilipokuwa na muda wa kupumzika nilisafiri hadi West Virginia kufanyakazi pamoja na kisima hicho kimoja nilichokuwa nacho.

Haki miliki ya picha
DGO

Image caption

Rusty anasema kisima cha kwanza kwake kilikuwa kama kupata dhahabu

Na kufikia hii leo kampuni ya Hutson DGO inamiliki zaidi ya visima 60,000 vya gesi na mafuta katika jimbo la West Virginia, Pennsylvania , Ohio Kentucky na Tenesee, eneo linaloitwa Appalachia.

Akiwa na wafanyakazi 925 kampuni hiyo ina mapato ya zaidi ya $500m . Asilimia 90 ya operesheni zake ni gesi asilia huku asilimia 10 ikiwa mafuta.

Biashara ya kampuni hiyo ni maalum- haichimbi mafuta na hifadhi za gesi.

Badala yake inanunua visima vya mafuta na vile vya gesi ambavyo wazilishaji mafuta wakuu hawavitaki kwa kuwa viwango vya uzalishaji vimepungua sana.

Hutson anasema kwamba DGO imesaidiwa sana na kile kinachojulikana kama ‘dash for shale’ nchini Marekani katika kipindi cha muongo mmoja uliopita, ambapo kampuni za gesi na mafuta ziliacha mafuta ya kawaida na kufanya kazi ya kuvunja mwamba ili kutafuta mafuta au gesi.

Kwa urahisi ni kwamba ukilinganisha na visima vya kawaida ,ambapo gesi na mafuta hufyonzwa , mbinu hii inashirikisha uvunjaji wa mwamba ili kupata mafuta na gesi ambayo haikuwa rahisi kupata.

Hutson anasema kwamba sekta hiyo kwa kiwango kikubwa imeanza kuelekea katika mtindo huo mpya, na uwezo wake wa kuzalisha mafuta mengi ,unamaanisha kwamba DGO imeweza kununua maelfu ya visima vya zamani, ambavyo bado ni visima vya mafuta vya kawaida na kuendelea kupanua biashara yake.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Japo bishara yake kwa 90% ni ya gesi pia “hajachelea” kuimarisha visima vyake vya mafuta

Huku akiweza kuchangisha fedha za upanuzi wa kampuni yake, mwaka 2017 , kamapuni hiyo iliamua kwenda katika soko la hisa na kuuza hisa zake .

Katika tukio lisilo la kawaida kwa kampuni ya Marekani , Hutson alichagua soko la hisa la London kama soko mbadala la uwekezaji.

“Kampuni haikuwa kubwa sana kuweza kuuza hisa zetu nchini Marekani” , anasema.

”Na sikutaka kwenda katika njia ya kibinafsi kwasababu sikutaka kumfanyia kazi mtu mwengine yeyote .”

DGO sasa inakaribia kuelekea katika soko kuu la hisa mjini London LSE.

Chini ya usimamizi wa Hutson DGO imekuwa kwa haraka tangu iuze hisa zake mwezi Februari ikiongeza uzalishaji mara 20 zaidi na hifadhi zake mara 23 zaidi.

Lengo kuu la DGO ni kuendelea kununua visima vya mafuta ili kuchukua mahala pa visima ambavyo vitakuwa vimefiki mwisho wake katika uzalishaji.

Haki miliki ya picha
Gaylon Wampler

Image caption

Baba yake Rusty, pchaniu, ana jukumu la hadhi y ajuu katika kampuni hiyo

Hutson anasema kwamba kampuni hiyo inatarajiwa kupanuka katika maeneo mengine kama vile Texas.

Kwa sasa anasema kwamba amepumzika kutokana na kaunguka kwa bei ya mafuta na gesi tangu kuanza kwa mlipuko wa virusi vya corona, kwa kuwa ana malengo ya muda mrefu kwa kuwa biashara yake inafanya kazi mara kwa mara ikilinganishwa na washindani wake wakuu.

Pia anaweza kutafuta usaidizi na ushauri kutoka kwa babake.

Babake, Hutson ni msimamizi wa operesheni za kampuni hiyo katika eneo la West Virginia.

”Ana umri wa miaka 72 na anapenda kufanya kazi hiyo”, anasema Htson .

Je yeye hunishauri kuhusu ni nini ninachopaswa kufanya? ndio.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *