Safari za ndege zaanza uwanja wa ndege wa kimataifa Hong KongMamlaka ya viwanja vya ndege ya Hong Kong imetangaza Jumatano kuwa jaji ametoa amri ya muda ya kudhibiti maandamano ya kuipinga serikali, katika moja ya uwanja wa ndege mkubwa duniani, ambapo kwa siku mbili waandamanaji walikuwa wameleta ghasia kwa kupambana na polisi.

Amri hiyo inawataka waandamanaji kuwepo katika maeneo maalumu, ikiwa ni juhudi za kuzuia msongamano ambao ulisababisha wafanyakazi wa serikali na mashirika ya ndege kurudishwa majumbani ikiwa pamoja na kusitisha safari zote za ndege za kutoka na kuingia katika himaya hiyo ya China.

Hatua hiyo ilisababisha wasafiri wa ndege kutojua la kufanya na kutokuwa na uhakika wa lini wata-endelea na safari zao huku wakishindwa kununua chakula na kukokosa mahala pa kulala.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *