Sean Connery: Muigizaji wa filamu ya James Bond afariki dunia akiwa na miaka 90


Sir Sean Connery

Sir Sean Connery, muigizajiwa sinema ya James Bond amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 90, familia yake imethibitisha.

Muigizaji huyo wa Uskochi alifahamika sana kwa kuwa mhusika wa katika sinema ya James Bond, na alikuwa wa kwanza kuleta sinema hiyo katika ukumbi wa sinema..

Sir Sean alifariki akiwa usingizini, akiwa Bahamas ambako amekuwa “akiugua kwa muda”, mwanawe wa kiume alisema.

Kazi yake ya uigizaji wa miongo mitano ilimwezesha kushinda tuzo ya Oscar mwaka 1988 kutokana na jukumu lake katika ‘The Untouchable’.

Filamu zingine alizoigiza Sir Sean ni pamoja na The Hunt for Red October, Highlander, Indiana Jones na the Last Crusade and The Rock.

Jason Connery alisema baba yake “alikuwa na sehemu kubwa ya familia yake Bahamas ambayo ilikuwa naye” alipofariki usiku mjini Nassau.

Alisema: “Sote tunajaribu kukubaliana na msiba huu mkubwa kwani limetokea sasa, ingawa baba yangu amekuwa mgonjwa kwa muda.

“Ni siku ya huzuni kwa watu wate waliomfahamu baba yetu mpendwa na watu wote waliovutiiwa na uigizaji wake kote duniani .”

Maelezo ya video,

Highlights of Sir Sean Connery’s acting career

Sir Sean, anayetokea Fountainbridge, Edinburgh aliigiza filamu ya first James Bond mwaka 1962 na kuendelea mbele na kuigiza filamu zingine tano rasmi – na zingine ambayo sio rasmi kama vile Never Say Never Again mwaka 1983.

Aliamminiwa na watu wengi kuwa muigizaji mahiri ambaye ailiigiza 007 kwa muda mrefu, akiitwa majina hayo.

Alikabidhiwa tuzo ya knigh na Malikia Queen katika Holyrood Palace mwaka 2000. Mwezi Augosti, alisherehekea mwaka wa 90 wa siku yake ya kuzaliwa.

Aliunga mkono kwa muda mrefu uhuru wa Uskochi, akisema hayo katika mahojiano kuelekea kura ya maoni ya mwaka 2014 na kugusia kwamba huenda akarejea nyumbani kutoka Bahamas na kuishi Scotland inadapo itapiga kura kujitenga na Uingereza.

Waziri wa Kwanza wa Scotland Nicola Sturgeon amesema: “Nimevunjika moyo kupokea taarifa za kifo cha Sir Sean Connery. taifa letu linaomboleza kwa kumpoteza mpendwa wetu.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *