Serikali ya kenya yaondoa vibali ya makampuni ya kubeti


Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

SportPesa ni moja ya makampuni yaliyoathiriwa naagizo la serikali la kufutwa la leseni ya kifanyia kazi nchini Kenya

Serikali ya Kenya imefuta kwa muda vibali vya makampuni takriban 27 ya mchezo wa bahati nasibu hadi yatakapolipa ushuru.

Katika taarifa iliyotolewa Jumatano na Mkurugenzi wa Bodi ya Udhibiti na utoaji wa Leseni ya michezo ya Bahati nasibu nchini Kenya, Liti Wambua pia imeagiza makampuni yote ya simu za mkononi yenye huduma za huduma za kutuma na kupokea pesa kubatilisha nambari za makampuni hayo za pay bill zinazotumiwa na kampuni zilizoathiriwa na hatua hiyo.

Tayari wachezaji wa michezo ya bahati nasibu wameanza kupokea ujumbe unaoonyesha kuwa kuna tatizo kwenye mtandao wa mchezo mfano ni ujumbe huu:

Kamapuni ya mawasiliano ya simu za mkononi -Safaricom ambayo imekuwa ikitumiwa makampuni ya michezo ya bahati nasibu na kamari tangu yalipoanzisha michezo hiyo nchini Kenya, imesema kuwa agizo hilo la serikali ambalo litaathiri akaunti milioni 12 za kubeti , limeiacha njia panda kwasababu baadhi ya akaunti hizo zina pesa na makampuni kama vile SportPesa na Betin zimepata agizo la mahakama la kuendelea kufanya kazi.

Hata hivyo kupitia mawakili wa Safaricom pia imeomba iruhusiwe kubaki na alama za siri (codes) ili kuwaruhusu watu kutoa pesa zao kwenye simu za mkononi, na imeomba kutoa taarifa kwa umma juu ya uamuzi wa mahakama kuhusu leseni.

Makampuni hayo ambao ni pamoja na SportPesa, Betin na Betway, pia yanakabiliwa na tisho la kushuhudia mameneja wake wa kigeni wa ngazi ya juu wakirudishwa makwao.

Makampuni ambayo tayari yamefutiwa vibali vya kufanyanyia kazi nchini Kenya ni pamoja, SportPesa, Betin, Betway, Betpawa, PremierBet, Lucky2u, 1xBet, MozzartBet, Dafabet, World Sports Betting, Atari Gaming, Palms Bet na Betboss miongoni mwa makampuni mengine.

Imeripotiwa kuwa makampuni hayo ya bahati nasibu yalishindwa kuthibitisha kuwa yanalipa ushuru kulinga na maagizo ya Bodi ya Udhibiti na utoaji wa wa michezo ya bahari nasibu- Betting Control and Licensing Board (BCLB).

Image caption

Asilimia 76 ya vijana wa Kenya hushiriki michezo ya bahati nasibu pamoja na kamari

Miongoni mwa mambo yaliyobainiwa na Bodi wakati wa uchunguzi wake ni kwamba makampuni hayo yalipata faida ya shilingi bilioni 204 za Kenya mwaka jana, lakini yalilipa ushuru wa shilingi bilioni 4 pekee.

Hata hivyo Kampuni ya Betin tayari imekwenda mahakamani kudai irudishiwe leseni yake.

Makampuni yote ya bahatinasibu yalitakiwa kupata leseni mpya za kuendesha shughuli zao tarehe Mosi Julai.

Image caption

Mchezo bahati nasibu ni biashara yenye thamani ya mabilioni ya dola kwa kampuni zinazoendesha biashara hii

Awali Waziri wa mambo ya ndani Fred Matiang alielezea haja ya kufanya mabadiliko katika kudhibiti sekta michezo ya bahati nasibu.

“Tunapaswa kufanya mabadiliko ili kufanya michezo ya bahati nasibu na kamali kuwa yenye mwongozo. Pamoja na kwamba sekta hii inaweza kutoa fursa za kimaisha kwa baadhi ya watu na, labda kuchangia katika ukuaji wa uchumi, ina changamoto ,”alisema Bwana Matiang’i.

Aliongeza kuwa asilimia 76 ya vijana wa Kenya hushiriki michezo ya bahati bahati nasibu pamoja na kamari huku asilimia 54 ya wale wanaoshiriki michezo hiyo wakitoka katika kundi la wenye kipato cha chini. Mchezo wa kamari unaendelea kuenea barani Afrika haswa miongoni mwa mashabiki wa soka. Ni biashara sasa iliyo na thamani ya mabilioni ya dola kwa kampuni zinazoendesha biashara hii.

Makampuni yaliyoathiriwa na agizo:

 • SportPesa
 • Betin
 • Betway
 • Betpawa
 • Elitebet
 • PremierBet
 • Lucky2u
 • 1xBet
 • MozzartBet
 • Dafabet
 • World Sports Betting
 • Atari Gaming
 • Palms Bet
 • Betboss
 • Kick-Off
 • Millionaire Sports Bet
 • Cheza Cash
 • Betyetu
 • Bungabet
 • Cysabet
 • Saharabet
 • Easibet
 • Easleighbet
 • Sportybet
 • AGB lottery and gaming
 • Atari
 • Kickoff

Unaweza pia kutazama:

Huwezi kusikiliza tena

Je michezo ya kamare inaleta hofu gani katika mataifa ya Afrika mashariki?Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *