Sex for Grades: Nigeria kuanzisha sheria ya kupinga unyanyasaji wa ngono


Boniface Igbeneghu on undercover film

Image caption

Mhadhiri Boniface Igbeneghu alipigwa picha BBC’s investigation

Seneta wa Nigeria ameanzisha sheria yenye lengo la kuzuia unyanyasaji wa ngono katika vyuo vikuu.

Mapendekezo ya kuanzishwa kwa sheria hiyo yamekuja baada ya kipindi cha uchunguzi cha BBC kubaini unyanyasaji wa kingono unaofanywa na wahadhiri dhidi ya wanafunzi wa chuo kikuu nchini Nigeria na Ghana.

Seneta huyo amesema kuwa ana matumaini kuwa uchunguzi wa BBC utasaidia kuunga mkono uanzishwaji wa sheria hiyo.

Seneta Ovie Omo-Agege anasema kwamba hata kama sheria haipo lakini unyanyanyasaji wa kingono hauruhusiwi katika vyuo vikuu.

Kama mapendekezo hayo yataweza kuwa sheria basi jambo hilo litakuwa kosa la jinai kwa walimu wa chuo kikuu kutoa rushwa yeyote ya ngono kwa wanafunzi.

Katika mapendekezo hayo ambayo seneta aliyasoma hapo jana jumatano, inaweza kuwahukumu wwalimu kifungo cha miaka 14 kwa kuhusika na mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi.

Harakati za kuanzisha sheria inayopinga unyanyasaji wa ngono ilianzishwa mwaka 2016 lakini haikupitishwa na bunge.

Sheria hiyo ilikosolewa kwa sababu haikugusia unyanyasaji wa kingono katika eneo la kazi na ilijumuisha usalama wa mhusika

Utetezi wa mhusika umetolewa katika mswada wa mwisho.

Huwezi kusikiliza tena

BBC Africa Eye: Unyanyasaji wa kingono wa wanafunzi katika Chuo kikuu cha Lagos na Ghana.

Video inayoonyesha waadhiri wa chuo kikuu cha Nigeria na Ghana iliruka

Makala ya Africa Eye kuhusu unyanyasaji wa kingono katika vyuo vikuu au maarufu mtandaoni kama #sexforgrades kufuatia uchunguzi wa vyuo Vikuu vya Lagos na Ghana.

Wahadhiri wawili waliotuhumiwa Ghana wamesimamishwa kazi, huku wahadhiri wengine wawili walisimamishwa kazi katika Chuo Kikuu cha Lagos japo wote wamekanusha madai dhidi yao.

Kitu gani kingine kimeoneshwa katika Makala?

Wahadhiri wanne walipigwa picha za video kwa siri zikiwaonesha wakimrubuni kimapenzi mwandishi wa uchunguzi wa BBC aliyejifanya mwanafunzi.

Mhadhiri wa chuo kikuu cha Lagos, Dkt. Boniface Igbeneghu ambae pia ni mchungaji wa kanisa amesimamishwa kazi na chuo na kanisa lake.

Yeye ni miongoni mwa wahadhiri walionekana katika makala ya siri iliyofanyika kwa zaidi ya mwaka mmoja na kitengo cha BBC Africa Eye.

Makala hii ya urefu wa saa moja imeonesha pia wahadhiri wawili kutoka chuo kikuu cha Ghana wakihusika na vitendo vya unyanyasaji wa kingono kwa wanafunzi.

Wote wawili Profesa Ransford Gyampo na Dr Paul Kwame Butakor wamekanusha kuhusika na kuomba rushwa kwa kutoa alama za darasani.

Profesa Gyampo amesema kwa vyombo vya ndani vya habari kuwa ana mpango wa kuchukua hatua za kisheria dhidi ya BBC.

Chuo kikuu cha Ghana kimetoa taarifa kuwa watafanya uchunguzi kwa wahadhiri hao na kusisitiza kuwa hawahusiki na kumtetea mhadhiri yoyote ambae ameshukiwa kujihusisha na rushwa ya ngono chuoni.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *