
Shakira amekuwa msanii wa hivi karibuni kuuza haki za muziki wake kwa kitita cha mamilioni ya dola. Nyimbo zake zote 145, pamoja na Hips dont Lie, Whenever, Wherever, na She Wolf, zimejumuishwa kwenye mpango huo. Nyimbo hizo zilimfanya msanii wa kike wa Kilatini aliyeuza rekodi nyigi zaidi ulimwenguni. Mkataba huo ni baina na kampuni ya Hipgnosis, ambao pia hivi karibuni walipata haki za muziki za mwanamziki Blondie na Neil Young.