Shule inayotoza karo kupitia taka za plastiki


Akshar Forum katika Jimbo la Assam Mashariki mwa India imebuni njia ya kipekee ya wanafunzi kulipa karo ya shule. Wanahitajika kuleta taka ya plastiki kila wiki. Mradi huo ulianza kutekelezwa mwezi Oktoba mwaka 2018 baada ya waanzilishi wake kugundua kuwa plastiki zinachomwa nje ya nyumba zao. Kampeni hiyo ya kulinda mazingira ni moja ya miradi inayoendeshwa katika shule hiyo ambapo wanafunzi wanapewa mafunzo ya kawaida na nyingine ya ziada itakayowawezesha kujitegemea baada ya kukamilisha elimu yao ya msingi.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *