Sudan: Kesi inayomkabili rais wa zamani Omar el Bashir ina uzito gani?


Bashir

Haki miliki ya picha
AFP

Image caption

Omar al-Bashir kizimbani Sudan

Afisa wa uchunguzi ameiambia mahakama nchni Sudan kwamba rais wa zamani Omar al-Bashir amekiri kupokea mamilioni ya dola kutoka Saudi Arabia.

Bashir alifika mbele ya mahakama leo Jumatatu kukabiliwa na mashtaka ya ufisadi , ambayomawakili wake wanasema hayana msingi.

Alitumuliwa Aprili baada ya maandamano ya miezi kadhaa, yaliofikisha kikomo utawal awake wa takriban miaka 30.

Mnamo Juni, waendesha mashtaka wamesema kiwango kikubwa che fedha za kigeni zilizohodhiwa ziligunduliwa katika magunia ya nafaka nyumbani kwake.

Siku ya Jumapili, wanaharakti wa kutetea demokrasia na viongozi wa jeshi nchini humo waliomtimua madarakani Bashir, walisaini makubaliano yanayotoa fursa kufanyika uchaguzi mkuu nchini.

Kiongozi huyo wa zamani, aliyefika mahakamani na kusimama kizimbani alikuwa amevaa nguo nyeupe na kilemba. Hakujibu tuhuma zinazomkabili, Shirika la habari la Reuters linaripoti.

Kumekuwa na maafisa wengi wa usalama walioshika doria nje ya mahakama katika mji mkuu Khartoum, wakati Bashi alipowasili.

Haki miliki ya picha
Reuters

Image caption

Bashir alionekana kwa mara ya kwanza hadharani mnamo Juni mjini Khartoum

Anakabiliwa na mashtaka gani ya ufisadi?

kiongozi huyo wa zamani anakabiliwa na mashtaka yanayohusiana na “kumiliki fedha za kigeni, ufisadi, na kupokea zawadi kinyume cha sheria”.

Mnamo April, kiongozi wa jeshi Sudan Abdel Fattah al-Burhan alisema zaidi ya milioni $113 ya fedha katika sarafu ya pauni ya Sudan na sarafu za kigeni ziligunduliwa numbani kwake Bashir.

Mawakili wanaomtetea Bashir wanapinga mashtaka hayo.

Kiongozi huyo aliyetimuliwa alitarajiwa mahakamani mnamo Julai – lakini kesi iliahirishwa kutokana na sababu za usalama.

Bashir anakabiliwa na mashtaka gani mengine Sudan?

Mnamo Mei, nwendesha mashtaka nchini Sudan alimshtaki Bashir kwa uchochezi na kuhusika katika mauaji ya waandamanaji.

Mashtaka hayo yanatokana na uchunguzi wa kifo cha daktari aliyeuawa wakati wa maandamano yaliochangia kutimuliwa kwa Bashir madarakani mnamo Aprili.

Haki miliki ya picha
EPA

Image caption

Kumeshuhudiwa maandamano ya miezi kadhaa Sudan

Shahidi mmoja ameieleza BBC kwamba daktari huo aliyekuwa akiwatibu majeruhi alitoka nje ya jengo akiinua mikono juu, na kuarifu polisi kwamba yeye ni daktari, na papo hapo akapigwa bunduki.

Kesi ya Omar el Bashir ina uzito gani?

Kesi ya Bashir inaonekana kama mtihani ya iwapo utawala mpya unaweza kukabiliana na uhalifu unaotuhumiw akutekelezwana utawala uliokuwepo.

Siku ya Jumamosi, baraza la utawala wa kijeshi nchini ulioingia madarakani baada ya kuondoka kwa Bashir, lilisaini makubaliano muhimu ya ugavi wa mamlaka na muungano wa kiraia wa upinzani.

Makubaliano hayo yanatoa fursa ya kuidhinishwa baraza jipya la utawala linalowajumuisha raia na majenerali wa jeshi , na kutoa fursa ya kufanyika uchaguzi mkuu na hatimaye utawala wa kiraia.

Mohamed Hamdan “Hemeti” Dagolo, anayetazamwa na wengi kama mtu mwenye nguvu Sudan, ameahidi kutii makubaliano hayo.

wanachama wapya wa baraza huru jipya walitarajiwa kuapishwa leo Jumatatu, lakini hafla hiyo imeahirishwa kwa siku mbili kutokana na ombi la wanaharakati wa kuunga mkono demokrasia, Reuters linamnukuu msemaji wa jeshi.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *