Syridio Dusabumuremyi: Kiongozi wa upinzani Rwanda 'auawa kwa kudungwa kisu'


Syridio Dusabumuremyi was at work when he was attacked

Haki miliki ya picha
©FDU-Inking

Image caption

Syridio Dusabumuremyi alikuwa kazini aliposhambuliwa

Mwanasiasa maarufu wa upinzani nchini Rwanda amedunguwa kisu na kuuawa, chama chake cha FDU-Inkingi kinasema.

Syridio Dusabumuremyi, mratibu wa chama hicho cha upinzani FDU-Inkingi, alikuwa kazini wakati aliposhambuliwa na wanaume wawili, kiongozi wa chama hicho Victoire Ingabire ameieleza BBC.

Mwanamume huyo ambaye ni baba ya watoto wawili alikuwana duka la kuuza chakula katika kituo cha afya katika wilaya ya kati ya Muhanga.

Polisi bado haijatoa tamko kuhusu taarifa za mauaji hayo.

Bi Ingabire anasema mauaji ya Dusabumuremyi ni ya hivi karibuni kufuatia msururu wa mashambulio dhidi ya wafuasi wa chama chake kwa lengo la kuwatishia.

Miezi miwili iliyopita, Eugène Ndereyimana, mwakilishi wa chama cha FDU-Inkingi kutoka eneo la mashariki mwa Rwanda alitoweka. Mpaka sasa hajapatikana.

Mnamo Machi, Anselme Mutuyimana, msemaji wa chama hicho alitekwa na baadaye kukutikana amefariki msituni magharibi mwa nchi hiyo.

Mnamo 2016, mwanachama wa FDU-Inkingi Jean Damascène Habarugira aliuawa.

Bi Ingabire, ambaye ni mkosoaji mkubwa wa rais Paul Kagame, amesema chama chake kinalengwa kwasababu kinapania kutetea haki za raia wa Rwanda na uhuru wao.

“Lengo letu ni zuri na hatutaacha kulipigania hata wakafanya lolote,” amesema.

Image caption

Kiongozi wa upinzani Rwanda Victoire Ingabire amesema chama chake kinalengwa kwasababu kinapania kutetea haki za raia wa Rwanda na uhuru wao

Victoire Ingabire ni nani?

Victoire Ingabire Umuhoza alizaliwa oktoba tarehe tatu mwaka 1968.

Ni mke na mama wa watoto wa tatu.

Amesomea Sheria na masuala ya uhasibu na hatimaye kufuzu kwa shahada ya uchumi na biashara nchini Uholanzi.

Tangu mwaka 1997, Ingabire amejihusisha na harakati za upinzani nchini Rwanda akiwa mafichoni Uholanzi.

Aliteuliwa na muungano wa kundi la viongozi wa upinzani ambao una wanachama nchini Rwanda, barani Ulaya, Marekani na Canada.

Mnamo mwezi Januari mwaka 2010 Bi Ingabire alirejea Rwanda kutoka mafichoni nchini Uholanzi baada ya kutajwa kuhusika kwenye mauaji ya kimbari ya mwaka 1994, ili kugombea uchaguzi wa urais.

Alikamatwa na kuzuiliwa kuwania urais.

Bi Ingabire, ni mwanachama wa jamii ya Wahutu na alihoji kwa nini makumbusho rasmi ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda hayakujumuisha Mhutu yeyote

Bi Ingabire alikamatwa na hatimae kufungwa jela mwaka 15 kwa makosa ya ugaidi pamoja na kuhatarisha usalama wa kitaifa.

Hata hivyo sasa yuko huru baada ya kupewa msamaha na Rais Kagame.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *