Tanzania yapiga marufuku safari za ndege za Kenya kuingia kwenye anga lake


Ndege ya Dreamliner ilipowasili Tanzania Julai

Tanzania imepiga marufuku Shirika la ndege la Kenya Airways kufanya safiri nchini humo hadi wakati usiojulikana.

Taarifa iliyotolewa na mamlaka ya usafiri wa anga nchini humo (TCAA) imeondoa idhini iliyopewa Shirika la ndege la Kenya Airways kuanza tena safari za kimataifa nchini Tanzania ikijubu hatua iliyochukuliwa na Kenya.

”Mamlaka inasikitika kuwatangazia kwamba kama hatua ya kujibu, serikali ya Tanzania imeamua kutupilia mbali idhini iliyokuwa imetoa kwa safari za ndege za Kenya Airways kati ya Nairobi na Dar es Salaam, Kilimanjaro na Zanzibar kuanzia Agosti 1, 2020 hadi muda usiojulikana” taarifa iliyotolewa na Jenerali Hamza Johari.

Hili limetokana na hatua iliyochukuliwa na Kenya baada ya Waziri wa uchukuzi nchini humo James Macharia kusema kuwa anga la Kenya halitafunguliwa kwa kila mtu na orodha ya nchi zilizoruhusiwa kuingia Kenya ikionesha wazi Tanzania si mmoja wa nchi inayokaribishwa kwenye anga lake.

Hatua iliyochukuliwa na Kenya

Nchi zilizoruhusiwa katika anga la Kenya ni China, Korea Kusini, Japan, Canada, Zimbabwe, Ethiopia, Switzerland, Uganda, Rwanda, Namibia na Morocco.

Waziri wa uchukuzi James Macharia alisema nchi hizo zimedhibiti janga la Covid- 19 kwa kiasi cha kuridhisha.

Na kuwa nchi hizo zimepunguza maambukizi ya ugonjwa huo na raia wake wamekuwa wakipata dalili za kawaida za ugonjwa wa mfumo wa upumuaji.

”Tutaendelea kuboresha orodha yetu kwa kutegemea na hali ilivyo na mazingira. Hii ni orodha yetu kwa leo tutaipitia tena kesho na siku zinazokuja.”

”Abiria wote watakaowasili kwa ndege za kimataifa wakiwa na hati zinazoonesha kuwa hawana dalili za Covid-19 na wale waliopima saa 96 kabla ya safari hawatakaa karantini,” alisema.

Siku ya Jumatatu tarehe 27 mwezi Julai, Rais Uhuru Kenyatta alitoa kauli ambayo haikuilenga Tanzania moja kwa moja kuwa Kenya haifichi idadi ya watu wenye maambukizi ya Covid-19.

”Sisi tuko wazi na tunajua fika kuwa ugonjwa huu upo tofauti na majirani zetu ambao wanauficha ukweli huu,” alisema Rais Kenyatta.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *