Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 03.06.2020: Griezmann, Silva, Partey, Aurier, Koeman, Salah


Mshambuliaji wa Barcelona Antoine Griezmann mshambuliaji wa Barcelona Antoine Griezmann

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa Barcelona Antoine Griezmann mshambuliaji wa Barcelona Antoine Griezmann

Changamoto zinazomkabili mshambuliaji wa Barcelona Antoine Griezmann zinaweza kufanya Arsenal au Inter Milan kupata nafasi ya kumsajili mchezaji huyo mwenye miaka 29. (Express)

Arsenal wana matumaini kuwa beki wa kati David Luiz 33, anaweza kujaribu kumshawishi Mbrazili mwenzake Thiago Silva,35, kujiunga na klabu baada ya kuondoka Paris St-Germain msimu huu. (Le 10 Sport, via Mail)

Maelezo ya picha,

Washika bunduki wameongeza juhudi za kumuwinda kiungo wa Atletico Madrid, Thomas Partey lakini hawako tayari kufikia dau

Washika bunduki wameongeza juhudi za kumuwinda kiungo wa Atletico Madrid, Thomas Partey lakini hawako tayari kufikia dau linalotakiwa la pauni milioni 45. (Athletic, via Mirror)

Mchezaji wa nafasi ya ulinzi anayekipiga katika klabu ya Chelsea Andreas Christensen, 24, amesema hana nia ya kuondoka kwenye klabu na yuko tayari kwa mkataba mpya ndani ya Stamford Bridge. (Goal.com)

Maelezo ya picha,

Kiungo wa kati wa Arsenal Henrikh Mkhitaryan huenda akajiunga na Roma

Kiungo wa kati wa Arsenal Henrikh Mkhitaryan, 31, anaonekana kujiandaa kujiunga na Roma kwa mkataba wa kudumu baada ya mkataba wa kucheza kwa mkopo katika klabu ya ligi ya Serie A kuongezwa. (Mail)

Winga wa Liverpool Mohamed Salah, 28, amesema anataka kusalia kwenye klabu hiyo ”kwa muda mrefu”. (Bein Sports, via Express)

Maelezo ya picha,

Winga wa Liverpool Mohamed Salah, 28, anataka kusalia kwenye klabu hiyo

Kinda wa Manchester United Mbelgiji Largie Ramazani, 19, amekataa kusalia Old Trafford akiwa tayari kuhamia Almeria ya Uhispania. (Manchaster Evening News)

Mkurugenzi wa michezo wa klabu ya Rennes Florian Maurice amesema kuwa klabu hiyo haina mpango wa kumuuza kiungo Eduardo Camavinga, 17 anayecheza timu ya vijana wa chini ya miaka 21. (AS)

Tetesi bora Jumatano tarehe 02.06.2020

Maelezo ya picha,

Jadon Sancho hatagaraniwa zaidi ya pauni milioni 50

Manchester United haitalipa zaidi ya pauni milioni 50 kwa winga wa Borussia Dortmund Jadon Sancho.

Hatahivyo, klabu hiyo ya Bundesliga inataka ongezeko la pauni milioni 100 kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20. (Sky Sports)

Maelezo ya picha,

Arsenal wanafikiria kumtumia Matteo Guendouzi kama sehemu ya mpango wowote wa kubadilishana msimu huu

Arsenal wanafikiria kumtumia kiungo wa kati Matteo Guendouzi, 21, kama sehemu ya mpango wowote wa kubadilishana msimu huu. (Mail)

Tottenham wanaamini kuwa watampata kiungo wa Southampton Pierre-Emile Hojbjerg,24, msimu huu lakini watapaswa kuwauza wachezaji kwanza. (Telegraph)Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *