Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 08.04.2021: Lingard, Zaha, Sterling, Messi, Lukaku, Haaland, Konate, Vestergaard


Jesse Lingard

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kiungo wa kati wa Manchester United, Jesse Lingard

West Ham itafanya vyovyote vile ili kumnasa kiungo wa kati Jesse Lingard, 28, anayekipiga Manchester United. (Sky Sports)

Thamani ya Lingard kwa mujibu wa Manchester United ni pauni milioni 30. (Mirror)

Arsenal imerejesha nia yao tena kwa mshambuliaji wa Crystal Palace Wilfried Zaha,28. (90min)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Arsenal wameanza tena kumsaka mshambuliaji wa Crystal Palace Wilfried Zaha

Manchester City wanalenga kukubaliana kuingia mkataba mpya nawashambuliaji wa England Phil Foden,20, na Raheem Sterling,26, kabla ya mwishoni mwa msimu, baada ya kiungo wa kati wa Ubelgiji Kevin de Bruyne,29, kuongeza mkataba wake wa mpaka mwaka 2025. (Eurosport)Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *