

Chanzo cha picha, Getty Images
Kiungo wa kati wa Manchester United na England Jesse Lingard
Wawakilishi wa kiungo wa kati wa Manchester United na England Jesse Lingard, 28, wamefanya mazungumzo ya awali kuhusu uhamisho wake wa mkopo kwenda Nice, huku mazungumzo rasmi yakitarajiwa katika wiki ijayo. (Sky Sports)
Meneja wa Newcastle Steve Bruce anauungwaji mkono wa mmiliki wa klabu hiyo Mike Ashley, licha ya shinikizo kutoka kwa mashabiki wanaotaka afutwe kazi baada ya kushindwa despite na Sheffield United kati kati ya wiki. (Sky Sports)
Manchester United wamesitisha mpango wa kumnunua mchezaji wa Atletico Madrid wa safu ya kulia na kushoto Muingereza Kieran Trippier, 30, mwezi huu huku kukiwa na wasiwasi kuhusu matokeo ya marufuku ya kimataifa dhidi yake kwa kukiuka sharia ya kucheza kamari. (Manchester Evening News)
Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United yamesitisha mpango wa kumnunua Kieran Trippier kutoka Atletico Madrid
Tottenham huenda ikafutilia mbali mkataba wa Danny Rose katika dirisha la uhamisho wa Januari, huku West Brom ikionesha azama ya kutaka kumnunua beki huyo aliye na umri wa miaka 30. (Talksport)
Kiungo wa kati wa zamani wa Arsenal Mjerumani Mesut Ozil, 32, ameamua kuacha £7m alizotarajiwa kupokea kabla ya mwisho wa msimu huu ili afanikiwe kukatiza mkataba wake na kuondoka mwezi huu. (The Athletic)
Chanzo cha picha, Getty Images
Beki wa Tottenham Danny Rose
Mlinzi wa Manchester City ana Uhispania Eric Garcia, 20, amefikia makubaliano ya kibinafsi na Barcelona, lakini uhamisho wake haujakaribia kukamilika. (Goal)
Meneja wa Barcelona Ronald Koeman ana imani ya kuwasajili kiungo wa kati wa Liverpool na Uholanzi Georginio Wijnaldum, 30, na mshambuliaji wa Lyon na Uholanzi Memphis Depay, 26 kwa mkopo msimu huu. (Mundo Deportivo – in Spanish)
Chanzo cha picha, Getty Images
Kiungo wa kati wa Liverpool Georginio Wijnaldum
Mshambuliaji wa Arsenal Muingereza Folarin Balogun, 19, amekubali kujiunga na RB Leipzig. (Football Insider)
Liverpool wanajiandaa kumnunua mlinzi wa Brighton Muingereza Ben White, 23. (Liverpool Echo)