Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 14.02.2020: Dembele, Henderson, Mbappe, Messi, Grealish, Martinez, Carroll


Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola

Image caption

Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola

Pep Guardiola amedai kwamba Manchester City huenda ikamfuta kazi iwapo watashindwa kuilaza Real Madrid katika kombe la mabingwa Ulaya. (Guardian)

Manchester United imeruhusiwa kumsaini mshambuliaji wa Lyon na Ufaransa Moussa Dembele, 23, kwa dau la £60m deal. (Star)

Chelsea pia imepatiwa motisha wa kumsaka Dembele huku rais wa Lyon Jean-Michel Aulas akikiri watamuuza mchezaji anayetaka kuondoka “. (Mail)

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Manchester United imeruhusiwa kumsaini mshambuliaji wa Lyon na Ufaransa Moussa Dembele, 23, kwa dau la £60m deal. (Star)

Tottenham inafikiria kumsaini beki wa Norwich na England mwenye thamani £50m Ben Godfrey, 22. (Express)

Paris St-Germain imejianda kumpatia mshambuliaji wake Kylian Mbappe kandarasi ya malipo ya £41m kila mwaka ili kuzuia kumpoteza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 kwenda Real Madrid 2021. (Mirror)

PSG ina mpango wa kumsaini kipa wa Man United mwenye umri wa miaka 22 Dean Henderson, ambaye kwa sasa yupo kwa mkopo katika klabu ya Sheffield United. (Mail)

Aliyekuwa beki wa England Joleon Lescott amemuonya kiungo wa kati wa England na Aston Villa Jack Grealish, 24, kutojiunga na Manchester United mwisho wa msimu huu kwa kuwa huenda wasifuzu kushiriki katika kombe la vilabu bingwa Ulaya msimu ujao.. (Standard)Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *