Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 26.11.2021: Sterling, Vlahovic, Zidane, Pochettino, Rangnick, Milinkovic-Savic, Perisic,


Raheem Sterling

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Raheem Sterling

Manchester City itapaswa kuongeza juhudi kumpa mkataba wa muda mrefu winga wa England Raheem Sterling, 26 ambaye anahusishwa na Barcelona, ili aweze kusalia klabuni hapo. (Telegraph – subscription required)

Manchester United imeungana na vilabu vingine, vikiwemo Tottenham na Newcastle United, kutaka saini ya mshambuliaji Mserbia Dusan Vlahovic, 21 kutoka Fiorentina. (Mail)

Paris St-Germain imefanya mazungumzo na Zinedine Zidane wakijiweka sawa na uwezekano wa kocha wao Mauricio Pochettino kuondoka na kujiunga na Manchester United. (Le Parisien, via Metro)

Ralf Rangnick anatarajiwa kuwa kocha wa muda wa Manchester United lakini awali alikataa ofa kutoka klabu hiyo ya Old Trafford kabla ya kukubali masharti mapya ya mkataba huo. (Manchester Evening News)Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *