Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 12.10.2019: Eriksen, Haland, Aurier, Dier, Parkinson, Lacazette


Kungo wa kati wa Tottenham Christian Ericksen

Real Madrid itataka kumsaini kiungo wa kati wa Denmark Christian Eriksen mwezi Januari.(Marca)

Real Madrid pia wanaisaka saini ya mshambuliaji wa Red Bull Salzburg, 19 raia wa Norway Erling Haaland, ambaye amehusishwa na uhamisho wa kuelekea Manchester United. (AS)

Beki wa kulia wa Tottenham na Ivory Coast Serge Aurier, 26, amefichua kwamba alitaka kuondoka mjini London mwisho wa msimu uliopita na amekiri kwamba hajui hatma yake iko vipi katika klabu hiyo. (Football.London)

Aston Villa imehusishwa na kiungo wa kati wa Tottenham na Uingereza Eric Dier, 25. (Birmingham Mail)

Kazi ya Unai Emery kama mkufunzi Arsenal huenda ipo hatarani iwapo kikosi chake kitashindwa kufuzu katika kombe la klabu bingwa Ulaya msimu huu . (Times – subscription required)

Mchezaji wa zamani wa Uingereza na nahodha David Beckham anamlenga mshambuliaji wa Paris St-Germain na Ufaransa Kylian Mbappe, 20, kama mteja wake wa kwanza katika kazi yake mpya kama ajenti . (Mail)Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *