Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 15.02.2020: Isco, Pogba, Aubameyang, Giroud, Maddison, Traore


Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Kiungo huyo wa Ufaransa anataka kuondoka Man United

Paul Pogba anataka kuondoka Man United mwisho wa msimu huu lakini fursa ya mchezaji huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 26 kuweza kuondoka vizuri katika klabu hiyo huenda zikaathiriwa na hatua ya klabu hiyo kuomba kulipwa £83m ili kumuuza nyota huyo (Guardian)

Manchester United imeajiandaa kuwanunua wachezaji watatu wa England iwapo itafanikiwa kumuuza Pogba – kiungo wa kati wa Leicester James Madison, kiungo wa kati wa Aston Villa Jack Grealish, 24, na mshambuliaji wa Borussia Dortmund Jadon Sancho, 19. (Star)

Maddison anataka kujiunga na Manchester United. (Manchester Evening News)

Klabu za Arsenal na Chelsea zinafikiria kuwasilisha ombi la kumsajili kiungo wa kati wa Uhispania mwenye thamani ya £63m Isco, 27, huku klabu ya Real Madrid ikitafuta kuchangisha fedha kujiandaa kwa dirisha la uhamisho la mwisho wa msimu huu. (Sun)

Kiungo wa kati wa Real madrid Isco

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Kiungo wa kati wa Real madrid Isco

Ligi ya Premier League itaendeleza uchunguzi wake dhidi ya Manchester kufuatia hatua ya shirikisho la soka Ulaya Uefa kuwapiga marufuku kushiriki katika mechi za ligi ya mabingwa kwa misimu miwili mfululizo. (Mirror)

Manchester City huenda ikapunguziwa pointi moja katika ligi ya England na huenda pia ikalazimishwa kucheza katika ligi ya pili kufuatia hatua yake ya kupigwa marufuku, wataalama wameonya. (Star)

Arsenal na mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 30, watelengwa na Inter Milan iwapo klabu hiyo itampoteza mshambuliaji wake wa Argentina mwenye umri wa miaka 22 Lautaro Martinez in the summer. (Star)

Aubameyang

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Mshambuliaji wa Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang

Mchezaji huyo wa Inter analengwa na Barcelona pamoja na Real Madrid. (Mundo Deportivo – in Spanish.

Mshambuliaji wa Chelsea na Ufaransa Olivier Giroud, 33, amepewa kandarasi na klabu ya Lazio lakini watasubiri kufanya uamuzi huo msimu ujao kufuatia ombi kutoka kwa Tottenham katika dirisha la uhamisho la mwezi januari. (Telegraph)

Winga wa uholanzi na Manchester United Tahith Chong, 20, anafikiria ombi la kujiunga na Inter Milan mwisho wa msimu huu . (Guardian)

Manchester United inapima uhamisho wa mwisho wa msimu huu wa kumsajili kiungo wa kati wa Tottenham Eric Dier 26- r. (Star)

Eric Dier

Image caption

Kiungo wa Tottenham Eric Dier

Crystal Palace inalenga kumsajili Joakim Maehle, 22 ambaye ni beki wa kulia wa Denmark, ambaye amesema kwamba yuko tayari kuchukua uhamisho wa kucheza katika ligi ya Premier League. (Standard)

Arsenal wako hatarini ya kumpoteza winga wa Bukayo Saka, 18, katika uhamisho wa bila malipo mwisho wa msimu huu huku wakishindwa kukubaliana kuhusu kandarasi. (Metro)

Kipa wa Everton Maarten Stekelenburg, 37, ambaye alikua anelengwa na Real Madrid mwezi Agosti bado hajaanza mazungumzo mapya kuhusu kandarasi mpya huku kandarsi ya mchezaji huyo wa Uholanzi ikitarajiwa kukamilika mwisho wa msimu huu. (Liverpool Echo)

Barcelona inafikiria kumnunua winga wa Uhispania Adama Traore, 24, kutoka Wolverhampton Wanderers mwisho wa msimu huu. (Birmingham Mail)

TETESI ZA SOKA IJUMAA

Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola

Image caption

Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola

Pep Guardiola amedai kwamba Manchester City huenda ikamfuta kazi iwapo watashindwa kuilaza Real Madrid katika kombe la mabingwa Ulaya. (Guardian)

Hatahivyo kufutwa kazi kwa Guradiola sio kitu rahisi kutokana na rekodi yake bora alioiweka baada ya kushinda mataji matano muhimu licha ya kushindwa kuiepeleka mbele ya robo fainali ya kombe la klabu bingwa katika majaribio matatu.

Manchester United imeruhusiwa kumsaini mshambuliaji wa Lyon na Ufaransa Moussa Dembele, 23, kwa dau la £60m deal. (Star)

Chelsea pia imepatiwa motisha wa kumsaka Dembele huku rais wa Lyon Jean-Michel Aulas akikiri watamuuza mchezaji anayetaka kuondoka “. (Mail)

Moussa Dembele

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Manchester United imeruhusiwa kumsaini mshambuliaji wa Lyon na Ufaransa Moussa Dembele, 23, kwa dau la £60m deal. (Star)

Tottenham inafikiria kumsaini beki wa Norwich na England mwenye thamani £50m Ben Godfrey, 22. (Express)

Paris St-Germain imejianda kumpatia mshambuliaji wake Kylian Mbappe kandarasi ya malipo ya £41m kila mwaka ili kuzuia kumpoteza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 kwenda Real Madrid 2021. (Mirror)

PSG ina mpango wa kumsaini kipa wa Man United mwenye umri wa miaka 22 Dean Henderson, ambaye kwa sasa yupo kwa mkopo katika klabu ya Sheffield United. (Mail)

Kylian Mbappe

Image caption

Mshambuliaji wa Uafransa na PSG Kylian Mbappe

Aliyekuwa beki wa England Joleon Lescott amemuonya kiungo wa kati wa England na Aston Villa Jack Grealish, 24, kutojiunga na Manchester United mwisho wa msimu huu kwa kuwa huenda wasifuzu kushiriki katika kombe la vilabu bingwa Ulaya msimu ujao.. (Standard)

Real Madrid iko tayari kuilipa Inter Milan £120m zinazohitajika kumuachilia mshambuliaji wa Argentina Lautaro Martinez, 22, kutoka katika kandarasi (TyC Sports)

Lautaro Martinez

Image caption

Real Madrid iko tayari kuilipa Inter Milan £120m zinazohitajika kumuachilia mshambuliaji wa Argentina Lautaro Martinez, 22, kutoka katika kandarasi (TyC Sports)

Tottenham inapanga kumsherehekea mfungaji wa magoli mengi zaidi katika klabu hiyo ambaye amefikisha umri wa miaka 80 Jimmy Greaves kabla ya mechi yake ya ligi ya mabingwa kati yake RB Leipzig wiki ijayo. (Standard)

TETESI ZA SOKA ULAYA ALHAMISI

Odion Ighalo

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Amepigwa marufuku katika uwanja wa mazoezi wa man United kutokana na hatari ya

Mshambuliaji wa Manchester United Odion Ighalo, 30, amepigwa marufuku katika uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo kutokana na hofu ya hatari ya maambukizi ya virusi vya corona.

Ighalo ambaye yuko kwa mkopo katika klabu ya United kutoka klabu ya Shanghai Shenhua hadi mwisho wa msimu amekuwa akifanya mazoezi na mkufunzi wa kibinafsi katika eneo tofauti mjini Manchester.

Mshambuliaji huyo alitakiwa kufanya mazoezi mbali na uwanja wa mazoezi wa Man United kutokana na maswala ya usalama wa kiafya kutokana na mlipuko wa virusi vya corona nchini China ambao umewaua zaidi ya watu 1100.(Mirror)

Liverpool inapanga kumnunua mshambuliaji wa RB Leipzig Timo Werner, 23, mwisho wa msimu huu huku dau la £46m likitosha kumsaini . (Bild)

Mshambuliaji wa Barcelona Philippe Coutinho, 27, amekataa uwezekano wa kurudi katika klabu ya Liverpool akidai kwamba yuko katika safari. (Sun)

Haki miliki ya picha
BBC/Twitter

Image caption

Mshambuliaji wa Barcelona Philippe Coutinho, 27, amekataa uwezekano wa kurudi katika klabu ya Liverpool akidai kwamba yuko katika safari. (Sun)

Huwezi kusikiliza tena

Pele ‘aibika’ kutokana na hali yake ya kiafya

Manchester United inachunguza hali ya kandarasi ya kinda wa Arsenal Bukayo Saka katika klabu hiyo. (Mail)

Mkufunzi wa Everton Carlo Ancelotti, 60, tayari ana matumaini kwamba kandarasi yake itaongezwa katika uwanja wa Goodison Park baada ya kutia saini kandarasi mnamo mwezi Disemba. (Mail)

Image caption

Mkufunzi wa klabu ya Everton ana matumaini ya kuongozewa mkataba

Real Madrid imemuorodhesha mshambuliaji wa Everton Moise Kean, 19, katika rada yake ya kutaka kumsajili. (Teamtalk)

Borussia Dortmund itamruhusu mshambuliaji wa England Jadon Sancho, 19, kuondoka mwisho wa kandarsi yake na tayari wameanza kutafuta mchezaji atakayechukua nafasi yake. (Telegraph)

Manchester United ndio wanaopigiwa upatu kumsaini Sancho huku Chelsea ikitarajiwa kukamilisha uhaimsho wa kiungo mshambuliji wa Ajax Hakim Ziyech, 26.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Chelsea inakaribia kukamilisha uhamisho wa dau la $38m

Liverpool itakabiliana na Real Madrid katika kuwania saini ya kiungo a kati wa Inter Milan Marcelo Brozovic, 27, mwisho wa msimu huu . (Star)

Mkufunzi wa klabu ya Chelsea Frank Lampard analenga kuwasajili wachezaji wane mwisho wa msimu huu utakaoigharimu Chelsesa £150m. (Metro)

Mkufunzi wa Juventus Maurizio Sarri amekiri kwamba Aaron Ramsey, 29, hajapata mambo kuwa rahisi wakati wa kipindi chake cha jeraha nchini Itali , na kuzua uvumi kwamba anapanga kurudi katika ligi ya England huku Arsenal, Manchester United, Liverpool na Chelsea zikihusishwa na uhamisho wake.. (Mirror)

Image caption

Kiungo wa kati wa Juventus Aaron Ramsey

Mshambuliaji wa Former Juventus na AC Milan Massimiliano Allegri ameripotiwa kufanya makubaliano na klabu ya England huku uvumi ukisema kwamba huenda akajiunga na Manchester United . (Corriere dello Sport, via Mail)

Arsenal inatarajiwa kuanzisha mazungumzo ya kandarasi mpya na Matteo Guendouzi, 20, ambayo yataongeza malipo ya mchezaji huyo. (Football.London)

Aston Villa ilishinda kumsaini Islam Slimani, 31, katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari kwa kuwa mchezaji huyo wa Leicester hakutaka kucheza katika timu iiopo eneo la kushushwa daraja.. (Birmingham Mail)

Image caption

Kiungo wa kati wa Arsenal Matteo Guendouzi

Chelsea inpanga ya kumsaini upya Jeremie Boga, 23, kutoka klabu ya Sassuolo miaka miwili tu baada ya kumuuza winga huyo.. (Star)Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *