Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 21.11.2020: Szoboszlai, Sanchez, Messi, Willian, Isco, Khedira


Mess

Mkufunzi wa Barcelona Ronald Koeman bado ana matumaini kwamba Lionel Messi atasalia katika klabu hiyo na kukataa kuingizwa katik amjadala kuhusu hatma ya baadae ya nyota huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 33. (Goal)

Tottenham huenda ikawasajili wachezaji zaidi mwezi Januari na inatarajiwa kumtafuta mlinzi mpya wa safu ya kati, huku mchezaji wa kimataifa wa Colombia Davinson Sanchez, 24, akitarajiwa kuondoka. (Football Insider)

Kiungo wa kati wa Mbrazil Willian, 32, ‘amechukuliwa hatua’ na Arsenal baada ya kwenda Dubai wiki kadhaa zilizopita – huku Mikel Arteta akisisitiza suala hilo ‘limesuluhishwa’. (Sun)

Jurgen Klopp anasisitiza kuwa hana habari kuwa mabingwa wa Ligi ya Premia Liverpool, wanapania kumnunua mlinzi mpya mwezi Januari dirisha la uhamisho litakapofunguliwa. (Goal)

Maelezo ya picha,

Mkufunzi Jurgen Klopp na Sadio Mane katika kambi ya mazoezi ya Liverpool,Austria

Liverpool wamefahamishwa kuwa watalazimika kulipa £26.7m ikiwa wanamtaka mlinzi wa Ajax Perr Schuurs, 20, huku AC Milan pia wakionesha nia ya kutaka kumnunua mholanzi huyo anayecheza safu ya kati na nyuma. (Sempre Milan via Liverpool Echo)

Mkufunzi wa Everton Carlo Ancelotti amepuuzilia mbali tetesi zinazoashiria anawataka wachezaji wake wawili wa zamani; kiungo wa kati wa Real Madrid na Uhispania Isco, 28, na kiungo wa kati wa Juventus na Ujerumani Sami Khedira, 33. (Liverpool Echo)

West Ham pia wamehusishwa na mshindi wa zamani wa Kombe la Dunia Khedira. (Sport Mediaset, via Team Talk)

Maelezo ya picha,

Isco, kiungo wa kati wa Real Madrid na Uhispania

Khedira hatarajiwi kuhamia ligi ya MLS ya Amerika. (Bild)

Kiungo wa kati wa Uswizi Granit Xhaka, 28, hana mpango wa kuondoka Arsenal kuelekea Inter Milan mwezi Januari. (Calciomercato via Mirror)

Kiungo wa kati wa Colombia James Rodriguez amepiga ripoti kwamba alihusika katika ugomvi alipokuwa katika shughuli ya kimataifa katika chumba cha kubadilisha nguo. Mchezaji huyo wa Everton aliripotiwa kugombana na wachezaji wenzake wa kimataifa Jefferson Lerma, 26, wa Bournemouth na Davinson Sanchez, 24 wa Tottenham. (Star)

Maelezo ya picha,

Erling Braut Haaland, mshambuliaji wa Borussia Dortmund

Baba yake Erling Haaland, Alf-Inge, kiungo wa kati wa Nottingham Forest, Leeds na Manchester City, amekiri kuwa mwanawe ambaye ni mshambuliaji wa kimataifa wa Norway, 20, anatamani kujiunga Ligi ya Premier lakini kwanza anataka kushinda taji na klabu yake ya sasa, Borussia Dortmund. (Sport 1, via Mirror)

Kiungio wa kati wa zamani wa Manchester City Trevor Sinclair, anaamini kuwasilia kwa mchezaji nyota wa Barcelona Lionel Messi, 33, ‘hakutaepuki’ baada ya mkataba wa mkufunzi wa City Pep Guardiola kurefushwa. (Talksport)

Chris Smalling,30, ameilaumu Manchester United kwa kutompatia maelezo dhahiri kuhusu hatma yake kabla ya kumwachilia kwenda Roma mwaka jana, lakini mlinzi huyo wa zamani wa old former England anasema kuwa anafurahia muda Italia. (Telegraph – subscription required)Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *