Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 23.05.2020: Coutinho, Willian, Haaland, Sancho, Pochettino, Kavertz


Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Kiungo wa kati wa Barcelona na Brazil Philippe Coutinho, anataka kurejea katika Ligi ya Premia

Chelsea, Manchester United na Leicester City zimewasiliana na ajenti wa kiungo wa Barcelona Philippe Coutinho katika majadiliano ya uhamisho wa msimu ujao lakini The Blues ndio chaguo la kwanza la mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil, 27. (Sun)

Kiungo wa kati wa Brazil na Chelsea Willian, 31, amedokeza kwamba huenda akatia saini mkataba wa muda mfupi hadi mwisho wa msimu huu wakati ambapo kampeni ya Ligi ya Primia huenda ikaendelea hadi Juni 30. (Mail)

Leicester City wanaongoza katika kinyang’anyiro cha kumsajili kiungo wa kati wa Liverpool Adam Lallana, ambaye mkataba wake unamalizika msimu huu, lakini Arsenal, Crystal Palace, Everton na West Ham pia wameonesha nia ya kumsajili mchezaji huyo, 32. (Star)

Haki miliki ya picha
BBC Sport

Image caption

Aliyekuwa winga wa Uingereza John Barnes

Aliyekuwa kiungo wa kati wa Liverpool John Barnes anasema mshambuliaji raia wa Norway wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland, 19, ana uwezo unaohitajika kuchukua nafasi ya Roberto Firmino at Anfield. (Express)

Kocha Ole Gunnar Solskjaer amehakikishiwa kuwa Manchester United itakuwa na ushindani kipindi cha usajili msimu huu baada ya kuweka wazi kuwa janga la corona limewagharimu £28m. (Express)

Bayern Munich ilionesha nia yake kwa mchezaji Jadon Sancho kabla ya msimu kusitishwa kwasababu ya virusi vya corona lakini Borussia Dortmund, ambayo ina imani kuwa inaweza kupata kiasi cha £100m kwa ajili ya kiungo huyo wa kati wa Uingereza, haiwezi kumuuza kwa mahasimu wake wa Bundeslig. (Metro)

Haki miliki ya picha
EPA

Image caption

Mauricio Pochettino aliwahi kushinda mara katika mechi 293 kipindi chake Tottenham

Muda wa kupunga upepo kwa aliyekuwa kocha wa Tottenham Mauricio Pochettino umekwisha na sasa ni wakati wa kuchapa kazi huku kukiwa na tetesi zinazomhusisha na uhamiaji wa Newcastle United. (Express)Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *