Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 31.10.2020: Ozil, Guardiola Alaba, Garcia, Kean, Bale, Kondogbia


Mesut Ozil

Maelezo ya picha,

Ozil alijiunga na Gunners mwaka 2013

Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta amesema kuwa amempatia mchezaji nyota wa zamani wa klabu hiyo Mesut Ozil ,32, “nafasi nyingi” kadri y auwezo wake kabla ya ya kumuacha nje ya kikosi cha Ligi ya Primia na Ligi ya Europa. (Sky Sports)

Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola, amabye kandarasi yake katika klabu hiyo inamalizika msimu ujao amepuuzilia mbali tetesi zinazomhusisha na kurejea Barcelona. (Manchester Evening News)

Barcelona inatarajiwa kurejelea tena jitihada za kumsajili mlinzi wa miaka 19 wa Manchester City Eric Garcia mwezi Januari dirisha la uhamisho litakapofunguliwa. (ESPN)

Maelezo ya picha,

Bacelona inamtaka mlinzi wa Manchester City Eric Garcia,19.

Carlo Ancelotti anasisitiza kuwa mshambuliaji Moise Kean,20 atarejea msimu ujao kujiunga na Everton mkataba wake wa mkopo Paris St-Germain utakapokamilika. (Liverpool Echo)

Mkufunzi wa Bayern Munich Hansi Flick ana matumaini kuwa mlinzi wake David Alaba, 28, raia wa Austria atakubali kutia saini kandarasi mpya ya kusalia katika klabu hiyo. (Goal)

Kocha wa England Gareth Southgate anajiandaa kumjumuisha beki wa kulia na nyuma wa Manchester Luke Shaw, 25, katika kikosi cha kimataifa, baada ya kumteua tangu mwezi Machi mwaka 2019. (Star)

Nyota wa Wales na Spurs Gareth Bale ametoa msaada wa £15,000 kufadhi 300 zawadi za Krismasi zitakazopewa wato walio na uhitaji zaidi Wales. (Wales Online)

Mkurugenzi wa soka wa Arsenal Huss Fahmy anatarajiwa kuondoka klabu baada ya kujiunga na Gunners miaka mitatiu iliyopita. (Standard)

Leading agent Mino Raiola has arrived at AC Milan to begin talks to extend the contracts of goalkeeper Gianluigi Donnarumma, 21, and defender Alessio Romagnoli, 25. (Gazzetta dello Sport, in Italian)

Atletico Madrid wanajiandaa kumsajili kiungio wa kati wa Valencia na Jamhuri ya Afrika ya Kati Geoffrey Kondogbia, 27. (Le10Sport, in French)Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *