Tetesi za soka Ulaya Jumamosi tarehe 09.11.2019:Pogba, Rodriguez, Promes, Rojo, Xhaka, Soares


Paul Pogba

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Kiungo wa Manchester United Paul Pogba

Real Madrid watakuwa tayari kutoa ofa ya kiungo wa Colombia James Rodriguez, 28, kubadilishana na kiungo wa timu ya taifa ya Ufaransa na Manchester United Paul Pogba,26. (El Desmarque, via Metro)

Inter Milan wanamtolea macho mshambuliaji wa Chelsea Olivier Giroud. (Gazzetta dello Sport – via Sun)

Mshambuliaji wa Ajax Quincy Promes, 27, amesema yuko tayari kwa uhamisho kuelekea ligi ya Primia siku za usoni,kauli hiyo ameitoa wakati ambapo Arsenal na Liverpool wakiwa na nia ya kumnyakua mchezaji huyo. (Mail)

Kocha wa timu ya taifa Uingereza Gareth Southgate amesema vikwazo vinavyotolewa kutokana na vitendo vya ubaguzi wa rangi vinapaswa kuwa vikali. (Express)

Manchester United itaweka mezani pauni milioni 42 kwa ajili ya kiungo wa Tottenham na timu ya taifa ya Denmark Christian Eriksen, 27, ifikapo mwezi Januari.(El Desmarque – via Express)

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

mchezaji wa nafasi ya ulinzi klabu ya Southampton, Cedric Soares

Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amesema mchezaji wa nafasi ya ulinzi ya Argentina Marcos Rojo anajiandaa kuendelea kubaki na klabu hiyo. Mchezaji huyo, 29 alifanya mazungumzo na Everton kuhusu uhamisho. (Manchester Evening News)

Kiungo wa Paris St-Germainm Ander Herrera, 30, amesema alifikiri mpira wa miguu ”haukuwa muhimu zaidi” kwa Manchester United alipokuwa akiichezea klabu hiyo.(Metro)

Kocha wa Southampton Ralph Hasenhuttl amesisitiza kuwa hana tatizo na kumchezesha mchezaji wa nafasi ya ulinzi Cedric Soares, 28, au kiungo Pierre-Emile Hojbjerg, 24, pamoja na ukweli kuwa mikataba yao inaelekea ukingoni.(Southern Daily Echo)

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema ”hakuna nafasi kabisa ” ya klabu hiyo kumsajili Kylian Mbappe, ingawa kumekuwa na kampeni za mitandao ya kijamii kuhusu tetesi za kuwa mshambuliaji huyo wa Paris St-Germain ,20 atatua kwenye klabu hiyo.(Sun)

Mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa klabu ya Arsenal Lucas Torreira, 23, atafanya mazungumzo na kocha Unai Emery. (Mirror)

Haki miliki ya picha
Reuters

Image caption

Kiungo wa timu ya taifa ya Colombia, James Rodriguez

Mshambuliaji wa Real Madrid Rodrygo, 18, aliyefuga kwa hat-trick kwenye ligi ya mabingwa wiki hii, alikataa kuhamia Liverpool kabla ya kujiunga na Real.(ESPN, via Marca)

Winga wa timu ya taifa ya Uhispania na Leicester Ayoze Perez, 26, amesema ilibaki kidogo tu ajiunga na Valencia wakati wa majira ya joto kabla ya kuamua kujiunga na mbwa mwitu’.(ABC, via Leicester Mercury)

Kocha wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kocha Unai Emery alitenda haki kumvua unahodha mchezaji wa nafasi ya ulinzi Granit Xhaka, 27. (Evening Standard)

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Granit Xhaka alivuliwa unahodha wa kikosi cha Arsenal

Nahodha na beki wa kati wa Newcastle Jamaal Lascelles, 25, amesema wachezaji wa klabu hiyo wana ari ya kutomuagusha kocha wao Steve Bruce msimu huu.(Chronicle)

Quique Sanchez Flores, 54, amesema hajutii kukubali kazi ya ukocha kwa klabu ya Watford ingawa timu yake imekuwa kwenye nafasi za mwisho miezi miwili baada ya kuchukua nafasi hizo.(Watford Observer)

Kiungo wa Sheffield United John Lundstram anajiandaa kwa mazungumzo ya mkataba. Mkataba wa mchezaji huyo, 25, utakwisha mwishoni mwa msimu. (Sheffield Star)Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *