Tetesi za soka Ulaya Jumanne 30.06.2020: Grealish, Sane, Gomes, Weghorst, Robert, Onan


Manchester City itafikiria kumsajili kiungo wa kati Jack Grealish

Maelezo ya picha,

Manchester City itafikiria kumsajili kiungo wa kati Jack Grealish

Manchester City itafikiria kumsajili kiungo wa kati Jack Grealish , 24 , ikiwa Bayern itamnunua winga wa Kijerumani Leroy Snae,24. Manchester United pia wamehusishwa na habari ya kumsajili Muingereza huyo. (Telegraph)

Chelsea wako tayari kumsajili kiungo Angel Gomes. Muingereza huyo, 19 , pia ananyemelewa na klabu kadhaa za nje. (Independent)

Na Manchester United pia inamtaka Grealish kujaza nafasi ya Gomes. (Express)

Maelezo ya picha,

New Castle na Arsenal zinamtaka Wolfsburg Wout Weghorst

New Castle na Arsenal ni miongoni mwa klabu za primia ambazo zinapenda kumsajili mshambuliaji wa Kiholanzi anayekipiga Wolfsburg Wout Weghorst,27 kwa kitita cha pauni milioni 35 (Bild-in German)

Southampton wanamhitaji mshambuliaji wa Arsenal Florian Balogun, 28. (Mail)

Magpies pia wanafikiria kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Thomas Robert- mchezaji mwenye miaka 19 mtoto wa mchezaji wa zamani wa Necastle Laurent Robert- kutoka Montpellier kwa uhamisho huru. (Mail)

Maelezo ya picha,

Andre Onana ni miongoni mwa wachezaji wanaolengwa na Chelsea

Wachezaji wanaolengwa na Chelsea, mlinda mlango wa Cameroon, Andre Onana 24, na beki wa kushoto Nicolas Tagliafico,27 wameambiwa wanaweza kuondoka Ajax. (Sun)

Kocha wa klabu ya kiholanzi Erik ten Hag amesema kiungo ambaye pia ananyemelewa na Mancehster United Donny van de Beek ,23, anaweza kuondoka mara dirisha la usajili litakapofunguliwa tena .(Mirror)

Maelezo ya picha,

kocha Jurgen Klopp anasema Liverpool hawatatumia ‘mamilioni ‘ kwenye soko la uhamisho

Mchezaji wa nafasi ya ulinzi ndani ya Paris St-Germain Layvin Kurzawa amesaini mkataba wa miaka mine na klabu hiyo . Mfaransa huyo ,27, alihusishwa na taarifa za kuchukuliwa na Arsenal na Liverpool. (Goal)

Mabingwa wa ligi ya Primia, Liverpool hawatatumia ‘mamilioni ‘ kwenye soko la uhamisho, amesema kocha Jurgen Klopp. (Mirror)

Maelezo ya picha,

kocha Jurgen Klopp anasema Liverpool hawatatumia ‘mamilioni ‘ kwenye soko la uhamisho

Wachezaji kadhaa wa Barcelona wamekuwa na mvutano na kocha Quique Setien kutokana na kuonesha kiwango duni cha uchezaji. (ESPN)

Mchezaji wa nafasi ya ulinzi katika klabu ya Leicester City Dennis Gyamfi, 18 ataondoka kwenye klabu hiyo kwa kuwa mkataba wake unakwisha hii leo. Mchezaji huyo wa timu ya vijana ya Uholanzi amekataa maombi kadhaa kutoka kwa mbwa mwitu hao. (Leicester Mercury)

Maelezo ya picha,

Layvin Kurzawa haendi Arsenal wala Liverpool

Mchezaji ambaye yupo Arsenal kwa mkopo Dani Ceballos amesema kwamba huenda akajiunga na klabu yake ya zamani Real Betis baada ya kiungo huyo wa Uhispania, 23, kusema kwamba atarudi katika klabu yake ya Real Madrid mwisho wa msimu huu. (Marca)

Mkufunzi wa klabu ya Gimnasia y Esgrima La Plata Diego Maradona anatumai mchezaji wa Brazil Ronaldinho, 40, atarudi katika ulingo wa soka ili kuichezea klabu hiyo ya Argentina. (Marca)Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *