Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 22.11.2020: Sterling, Jesus, Nunez, Ronaldo, Romero, Giroud


Raheem Sterling

Maelezo ya picha,

Raheem Sterling

Manchester City iko tayari kutoa ofa ya mkataba mpya kwa mshambuliaji wa England Raheem Sterling, 25. (Sunday Mirror)

United iko katika hatari ya kumkosa kiungo wa kati wa Iceland Isak Bergmann Johannesson huku Juventus ikiimarisha mipango yake ya kumsaka mchezaji huyo wa timu ya IFK Norrkoping, 17. (Sunday Mirror)

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amelipa kipau mbele suala la mrithi wa mshambuliaji wa Argentina Sergio Aguero, 32, na mshambuliaji wa Benfica raia wa Uruguay Darwin Nunez, 21, yuko kwenye orodha hiyo. (Sunday Telegraph – subscription required)

Manchester City, pia ina uhakika wa kutoa ofa kwa mshambuliaji wa Brazil Gabriel Jesus, 23, na kuongeza kima chake cha mshahara hadi pauni 150,000 kwa wiki. (Star on Sunday)

Mshambuliaji wa Juventus na Ureno Cristiano Ronaldo, 35, anafuatilia kwa karibu kurejea Real Madrid. (Marca)

Manchester United iko tayari kumuuza mlinda lango wa Argentine Sergio Romero, 33, mnamo mwezi Januari dirisha la usajili litakapofunguliwa kwa kima cha chini cha pauni milioni 2.5. (Star on Sunday)

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa na Chelsea Olivier Giroud

Mshambuliaji wa Chelsea raia wa Ufaransa Olivier Giroud, 34, amejitokeza kuwa mlengwa wa David Beckham kwa timu ya Inter Miami wakati wa dirisha la usajili litakapofunguliwa Januari mwakani. (Sunday Mirror)

Inter Milan pia inamfuatilia kiungo wa kati wa Giroud, pamoja na Georginio Wijnaldum, 30 wa Liverpool na uholanzi. (Corriere dello Sport)

Kiungo wa kati wa Uhispania Isco ameifahamisha Real Madrid nia yake ya kutaka kuondoka huku Madrid ikiwa tayari kumuuza kwa karibu pauni milioni 45, Arsenal na Manchester City zinasemekana kumwinda mchezaji huyo, 28. (Marca)

Maelezo ya picha,

Christian Eriksen ameichezea Denmark mara 95

Inter Milan itafurahia makubaliano ya mabadilishano na kiungo wa kati wa Denmark Christian Eriksen, 28, na kiungo wa kati wa Manchester United raia wa Brazil Fred, 27. (Football Italia)

Kocha wa Inter Antonio Conte anashikilia kuwa Eriksen ameshapewa fursa nyingi tu za kujiimarisha na haiwezi kukubali makubaliano ya mabadilishano katika nafasi hiyo. (Goal)

Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane anasisitiza kuwa mlinzi wa Ufaransa Raphael Varane, 27, hauzwi, baada ya kuhusishwa na Manchester United. (Goal)

Maelezo ya picha,

Ansu Fati wa Barcelona

Manchester United ilikubali kumsajili winga wa Uhispania Ansu Fati kwa Euro milioni 150 sawa na pauni (milioni 133) msimu uliopita, lakini mwisho wa siku ilichofanya Barcelona ilikuwa ni kupiga simu na kusitisha mazungumzo juu ya mchezaji huyo, 18. (Sport)

Mlinzi raia wa Ufaransa wa timu ya RB Leipzig Dayot Upamecano, 22, amependa ujumbe uliotumwa kwa mtandao wa Instagram unaomuhusishwa na kuhamia Manchester United. (Manchester Evening News)Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *