Tetesi za soka Ulaya Jumapili tarehe 18.10.2020: Depay, Wijnaldum, Valverde, Pogba, Garcia


Memphis Depay

Maelezo ya picha,

Memphis Depay (kushoto)

Kocha wa Barcelona Ronald Koeman anataka kumuongeza mshambuliaji wa Lyon na uholanzi Memphis Depay, 26, katika kikosi chake Januari. (AD, via Goal)

kiungo wa kati wa Liverpool na Uholanzi Georginio Wijnaldum, pia analengwa na Barcelona. Mchezaji huyo, 29, yuko mwaka wa mwisho wa mkataba wake na msimu ujao atakuwa huru. (AD, via Sky Sports)

Manchester United ina nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Real Madrid na Uruguay Federico Valverde, 22, na inaweza kutumia kiungo wao wa kati mshindi wa kombe la dunia kwa Ufaransa, Paul Pogba, 27, katika makubaliano ya mabadilishano. (Sun)

Ronald Koeman pia ameisihi bodi ya Barcelona kukamilisha uhamisho wa mlinzi wa Manchester City na Uhispania Eric Garcia, 19, Januari. (Mirror)

Maelezo ya picha,

Hivi karibuni Gareth Bale alirejea Spurs kwa mkopo

Kocha wa West Ham David Moyes anasema alikuwa na helikopta tayari kumchukua juu kwa juu Gareth Bale aliyetoka Tottenham na kuelekea Real Madrid mwaka 2013 wakati huo akiwa kocha wa Manchester United. Mshambuliaji huyo wa Wales, 31, hivi karibuni alirejea Spurs kwa mkopo. (Mail)

Msambuliaji wa Manchester United na England Marcus Rashford, 22, amesema siku ya mwisho ya kuwasili kwa mshambuliaji wa Uruguay Edinson Cavani, 33, kutasidia klabu hiyo kushindania kombe. (Sky Sports)

Maelezo ya picha,

Federico Chiesa mchezaji wa Fiorentina

Juventus ilichagua kumsajili winga wa Italia Federico Chiesa, 22, kutoka Fiorentina, badala ya kiungo wa kati wa Lyon na Ufaransa Houssem Aouar, 22, kipindi cha dirisha la usajili. (Sky Sport Italia, via Mail)

Kocha wa Middlesbrough Neil Warnock anasema Yannick Bolasie, 31, alistahili kulaumiwa kiasi fulani kwa kwa uhamisho uliofeli kwenye klabu hiyo. Winga hiyo alipangiwa kuhamia Boro kutoka Everton siku ya mwisho ya uhamisho. (Teesside Gazette)

Maelezo ya picha,

Ozil atakiwa kuthibitisha uwepo wake Arsenal

Meneja wa Arsenal Mikel Arteta amemuambia Mesut Ozil, 32, kuwa ana miezi miwili tu ya kuthibitisha uwepo wake ndani ya klabu.

Maelezo ya picha,

Winga Msenegali Ismaila

Watford ilikataa dau la siku ya makataa ya pauni milioni 25 lililotolewa na timu ya Primia Ligi Crystal Palace kwa ajili ya winga Msenegali Ismaila Sarr, 22. (Mail)

Maelezo ya picha,

William Saliba alikuwa na hamu ya kurejea St Etienne

Meneja wa St Etienne Claude Puel anasema mchezaji wa Arsenal mwenye umri wa miaka 19 anayecheza safu ya ulinzi ya Ufaransa William Saliba “alikuwa na hamu kubwa ya kurejea ” katika blabu kwa mkataba wa mkopo kabla ya hatua hiyo kukwama msimu huu . (L’Equipe, via Mail)Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *