Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 15.01.2020:Eriksen, Cavani, Lacazette, Guardiola, Solskjaer


Eriksen

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Christian Eriksen

Paris St-Germain ipo tiyari kupambana na Inter Milan kumuwania kiungo wa Tottenham Christian Eriksen, 27. (Mirror)

Mkurugenzi mtendaji wa Atletico Madrid Maguel Angel Gil Marin, alikuwa jijini Paris kufanya mazungumzo na PSG kuhusu mshambuliaji wao Edinson Cavani, 32. (Marca)

Mshambuliaji wa Arsenal Alexanndre Lacazette, 28, ni pendekezo la Atletico Madrid iwapo hawatampata Cavani. (Sky Sports)

Manchester City imeondoa uwezewekano wa mlinzi wake wa kati Muingereza John Stones, 25, kujiunga na miamba ya London Arsenal katika dirisha hili la usajili. (Manchester Evening News)

Kocha Pep Guardiola hana nia ya kuondoka Manchester City mwishoni mwa msimu. (Telegraph)

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Edinson Cavani

Chelsea haina uhakika wa kutoa paundi milioni 40 kumnunua mlinzi wake wa zamani Muholanzi Nathan Ake,24 na pia hawatamsajili mchezaji mwenzake wa Bournemouth raia wa Uingereza Callum Wilson, 27. (Sky Sports)

Mkurugenzi mtendaji wa klabu ya Manchester United Ed Woodward ameonekana akisafiri kuelekea Ufaransa kwa kutumia treni ya Eurostar, United inapania kumsajili kiungo wa Lile mfaransa Boubakary Soumare, 20. (Star)

United itatakiwa kulipa pauni milioni tano kumfuta kazi Ole Gunnar Solskjaer. (Sun)

Wakala wa winga wa United Mholanzi Tahith Chong, 20, ameonekana Inter Milan huku mchezaji huyo akitarajia kuondoka Old Trafford. (Mirror)

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Pep Guardiola

Mlinzi wa Ranger raia wa Ireland ya Kaskazini Danny Finlayson, 18, na mlinzi wa kushoto wa Uskochi Matthew Shiels, 19, wanatarajiwa kupelekwa kwa mkopo katika klabu ya Marekani ya Orange County. (Daily Record)

Mashambuliaji wa Los Angeles FC Carlos Vela atamkaribisha mshambuliaji wa Sevilla Javier Hernandez , hata kama mchezaji huyo mwenye miaka 31 atacheza na wapinzani wao LA Galaxy. (ESPN)

Mlinda mlango raia wa Ufilipino Neil Etheridge, 29, hatokuwemo katika kikosi cha Cardiff City kitakachoumana na Carlisle katika mzunguko wa tatu wa kombe la FA huku tetesi za yeye kuhamia Westham zikiendelea kushika kasi.(Wales Online)

Inter Milan inamuwinda mlinzi wa Parma Matteo Darmian, 30 .(Tuttomercatoweb – in Italian)

Mshambuliaji wa zamani Darren Bent ametaka kujumuishwa kwa mlinzi wa kushoto wa Manchester United Brandon Williams, 19 katika michuano Euro 2020. (Talksport)Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *