Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 20.08.2019: Neymar, Eriksen, Varane, Vorm, Mustafi, Ibe, Bravo


Neymar

Barcelona inatarajiwa kuwasilisha ombi la kumsaini Neymar, 27, kwa mkopo kutoka Paris St-Germain wiki hii kukiwa na fursa ya kufanya makubalaiono hayo kuwa ya kudumu.. (ESPN)

Juventus imeanza mazungumzo na PSG katika harakati za kutaka kumsaini mshambuliaji wa klabu hiyo Neymar, ambaye alijiunga na klabu hyo ya Ufraansa kwa dau la £200m mwaka 2017. (AS)

Barcelona haijajiandaa kuachilia ndoto yao ya kumrudisha Nou Camp mchezaji huyo wa Brazil . (Marca)

PSG iko tayari kuipatia Real madrid mshambuliaji wake neymar iwapo klabu hiyo itawapatia beki wake wa kati Raphael Varane, 26, na winga mwenye umri wa miaka 19 Vinicius Jr. (Telefoot, via Sun)

Kiungo wa kati wa Tottenham na Denmark Christian Eriksen, 27, ana hamu ya kujiunga na klabu kubwa Ulaya ikiwemo , Barcelona, Real Madrid au Juventus. (ESPN)

Liverpool huenda ikamsaini kipa wa Tottenham Michel Vorm, 35, ambaye amesalia bila klabu baada ya kuachiliwa msimu uliopita. (Caught Offside)

Arsenal imejiandaa kumwachilia beki wa Ujerumani Shkodran Mustafi, 27, kuelekea Roma kwa mkopo wa msimu huu kwa lengo kusajili kwa mkataba wa kudumu wa dau la £23m . (Forza Roma, via Sun)

Haki miliki ya picha
Getty Images

Celtic imejiandaa kumchukua mchezaji wa Bournemouth’s Jordan Ibe, 23, kabla ya dirisha la uhamisho la Uskochi kufungwa tarehe 2 September. (Express)

Manchester City, Arsenal na Tottenham wote walituma maskauti kumchunguza kinda wa klabu ya Rennes Eduardo Camavinga katika mechi ya ushindi wa klabu hiyo dhidi ya Paris St-Germain. (mail)

Kipa wa Chile Claudio Bravo, 36, anatarajiwa kuondoka Manchester City mwisho wa msimu huu katika uhamisho wa bila malipo.. (Sun)

Mchezaji wa zamnai wa Tottenham Fernando Llorente, 34, anakaribia kujiunga na Lazio kwa uhamisho wa bila malipo baada ya kuachiliwa na Spurs msimu huu. (Corriere dello Sport)

Monaco inamlenga kiungo wa kati asiyetakikana Chelsea Tiemoue Bakayoko, 25, kiungo wa kati wa Southampton na Gabon Mario Lemina, 25, kabla ya kukamilika kwa before the end of the European transfer deadline. (L’Equipe, via Talksport)Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *