Tetesi za soka Ulaya Jumatatu tarehe 11.11.2019: Ibrahimovic, Emery, Neymar, Kante, Drinkwater


Manchester united wanaweza kushawishika kumrejesha Zlatan Ibrahimovic kikosini

Image caption

Manchester united wanaweza kushawishika kumrejesha Zlatan Ibrahimovic kikosini

Manchester United inaweza kushawishika kujarbu kumrejesha tena mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic katika Old Trafford.

Ibrahimovic mwenye umri wa miaka 38- -mchezaji wa kimataifa wa Sweden atakuwa huru kutokana na kwamba mkataba wake na klabu ya ligi ya MLS – LA Galaxy unakaribia kumalizika.

(TuttoMercatoWeb, via Mail)

Uongozi wa Arsenal uko nyuma kwa “100%” ya meneja Unai Emery na mpango wa kusubiri hadi ufike msimu mwingine kabla ya kufanya maamuzi kuhusu hali ya baadae ya Muhispani huyo. (Athletic – subscription required)

Unaweza pi akusoma:

Meneja wa zamani wa Spain Luis Enrique, ambaye amekuwa akihusishwa na tetesi za kuwa meneja mbadala atakayechukua nafasi ya Emery katika klabu ya Arsenal, hatafikiria kurejea kwenye utawala kwa sasa . (ESPN)

Image caption

Aliyefikiriwa kuchukua nafasi ya Emery katika Arsenal hafikirii kurejea katika nafasi ya utawala wa klabu hiyo

Tottenham watamuhamisha winga wa Ajax na Morocco, Hakim Ziyech, mwenye umri wa miaka 26, wakati ambao Mchezaji wa kimataifa wa Denmark Christian Eriksen, mwenye umri wa miaka 27, ataondoka katika klabu hiyo. (90min)

Baba yake mchezaji wa kimataifa wa Brazil Neymar anasema kuwa hatafanya mazungumzo na Barcelona juu ya kurejea kwa mwanae katika klabu ya Nou Camp na kwamba mchezaji huyo wa safu ya mashambulizi mwenye umri wa miaka 27 atabaki katika klabu ya Ufaransa ya Paris St-Germain. (ESPN Brazil, via Mail)

Haki miliki ya picha
Reuters

Image caption

Baba yake Neymar anasema kijana wake ataendelea kubakia Paris St-Germain

Kiungo wa kati wa Chelsea na Ufaransa N’Golo Kante, mwenye umri wa miaka 28, amekana taarifa zinanazomuhusisha na kuhamia katika klabu ya Real Madrid na anasema kuwa anaweza kumalizia taaluma yake ya soka katika Stamford Bridge. (Sun)

Burnley wamekamilisha mipango ya kumaliza mkopo wa kiungo wa kati wa Chelsea mwenye umri wa miaka 29 Dann Danny Drinkwater katika klabu hiyo ifikapo mwezi Januari. (Sun)

Image caption

Ufaransa N’Golo Kante amekana taarifa zinazosema anahamia Real Madrid

Inter Milan wana nia ya kumchukua kiungo wa mashambulizi wa Ubelgiji Dries Mertens, mwenye umri wa miaka 32, ambaye mkataba wake na Napoli unafikia ukingoni msimu ujao.

Klabu San Siro pia iko makini na mchezaji wa Paris St-Germain mwenye umri 28- -Thomas Meunier wa Ubelgiji na mchezaji mwenzake katika safu ya ulinzi Layvin Kurzawa, mwenye umri wa miaka 27, wa Ufaransa. (Calciomercato)

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Mshambuliaji wa Wolves (Mbwa mwitu) Adama Traore ni mchezaji anayepiganiwa

Mshambuliaji wa Wolves (Mbwa mwitu) Adama Traore ni mchezaji anayepiganiwa baada ya kijana huyo mwenye umri wa miaka 23 kuitwa kuchezea timu zote Spain pamoja na Mali. Traore alizawa Spain na wazazi wenye uraia wa Mali. (Sun)

Meneja wa Leicester City Brendan Rodgers amehoji ikiwa aliungwa mkono ipasavyo na wamiliki wa klabu ya Liverpool alipokuwa akishikilia wadhifa huuo katika Anfield. (Liverpool Echo)

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Kalvin Phillips anafuatiliwa kwa karibu na Manchester United

Meneja wa Middlesbrough Jonathan Woodgate amesema kuwa ukosoaji unaomlenga kwenye mitandao ya kijamii unaweza kuwa unatoka kwa mashabiki wa Newcastle United na Sunderland. (Evening Gazette)

Kiungo wa kati wa Leeds United Muingereza Kalvin Phillips, mwenye umri wa miaka 23, na mshirika wa Ben White, na mchezaji wa safu ya ulinzi ya Elland Road mwenye umri wa miaka 22 kutoka Brighton ambaye anacheza kwa mkopo wanafuatiliwa kwa karibu na Manchester United. (Football Insider)

Image caption

Manchester United inajipanga kumsajili tena Wilfried Zaha

Klabu ya Arsenal imefanya mazungumzo na meneja wa zamani wa Uhispania na Barcelona, Luis Enrique kuhusu mpango kuchukua nafasi ya Unai Emery. (El Confidencial, kupitia Metro)

Klabu ya Tottenham wapo tayari kutoa ofa ya pauni 50m kwa Memphis Depay mshambuliaji wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 25, ambaye alihamia Klabu ya Ufaransa Lyon kutoka Manchester United mnamo Januari 2017.(Sunday Mirror)

Image caption

Je Paris St-Germain itamuongezea mkataba Mbappe?

Paris St-Germain kwa mara ya kwanza wamefanya majadilano ya kuongeza mkataba na mshambuliaji wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 20 Kylian Mbappé lakini hakuna ofa yoyote iliyotolewa. (L’Equipe, via Marca)

Meneja wa Liverpool Jürgen Klopp hayupo tayari kumuachia Dejan Lovren, mwenye umri wa miaka 30, aondoke klabuni hapo kwenye dirisha dogo la uhamisho Januari.(Football Insider)Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *