Tetesi zasoka Ulaya Jumamosi tarehe 17.10.2020: Ozil, Fernandes, Sarr, Keane, Barcelona, Primia Ligi


Ozil atakiwa kuthibitisha uwepo wake Arsenal

Maelezo ya picha,

Ozil atakiwa kuthibitisha uwepo wake Arsenal

Meneja wa Arsenal Mikel Arteta amemuambia Mesut Ozil, 32, kuawa na miezi miwli tu ya kuthibitisha uwepo wake ndani ya klabu. Mjerumani huyo maarufu aliyeishindio Ujeruamani katika kombe la dunia hajaanda kuwacvhezea Gunners tangu tarehe 7 Machi (Express)

Barcelona na Real Madrid wanafuatilia kwa karibu hali ya kiungo wa kati wa Ureno Bruno Fernandes mwenye umri wa miaka 26 katika Manchester United wakiwa na nia ya kujaribu kusaini nae mkataba . (Sun)

Maelezo ya picha,

Barcelona na Real Madrid wanamtaka Bruno Fernandes

Wachezaji wa Barcelona amekataa pendekezo la kukatwa malipo lililotolewa na rais wa klabu hiyo Josep Maria Bartomeu. (Marca)

Maelezo ya picha,

Winga Msenegali Ismaila

Watford ilikataa dau la siku ya makataa ya pauni milioni 25 lililotolewa na timu ya Primia Ligi Crystal Palace kwa ajili ya winga Msenegali Ismaila Sarr, 22. (Mail)

Meneja wa Leicester City Brendan Rodgers anasema Islam Slimani, mwenye umri wa miaka 32, bado ni sehemu ya mipango yao. Mshambuliaji huyo wa timu ya Algeria hajawachezea Foxes tangu Januari 2018. (Telegraph – subscription required)

Maelezo ya picha,

Islam Slimani bado ni sehemu ya mpango Leicester City

Muda wa mwisho wa winga wa Newcastle United Rolando Aaron wa kuhamia katika klabu ya Huddersfield Town hakuweza kuuheshimu baada ya kushindwa kuwasilisha nyaraka muhimu kwa EFL katika muda unaotakikana (Shields Gazette)

Maelezo ya picha,

William Saliba alikuwa na hamu ya kurejea St Etienne

Meneja wa St Etienne Claude Puel anasema mchezaji wa Arsenal mwenye umri wa miaka 19 anayecheza safu ya ulinzi ya Ufaransa William Saliba “alikuwa na hamu kubwa ya kurejea ” katika blabu kwa mkataba wa mkopo kabla ya hatua hiyo kukwama katika msimu huu . (L’Equipe, via Mail)

Primia Ligi imetahadharisha kuwa inaweza kukabiliwa na garama ya serikali juu ya mikataba ya matangazo kama itashindwa kuongezea fedha inazozitoa kwa Ligi ya soka ya England. (Telegraph – subscription required)

Maelezo ya picha,

Robbie Keane, atarudi upande wa MLS

Mshambuliaji wa zamani wa primia Ligi na Jamuhuri ya Ireland Robbie Keane, mwenye umri wa miaka 40, atarudi upande wa MLS – LA Galaxy kama meneja mpya wa klabu hiyo . (Sun)

Juventus wanapanga uhamisho wa £360m kumnasa mshambuliaji wa Paris St-Germain Kylian Mbappe, 21, klabu hiyo ya Serie A inaweza kumpeleka Cristiano Ronaldo upande wa pili. (Mirror).

Maelezo ya picha,

Abbie McManus anasema sasa baba yake anavaa fulana yenye jina lake

Difenda wa timu ya wanawake ya Manchester United Abbie McManus, mwenye umri wa miaka 27, ametoa matamshi ya utani kuwa shabiki wa timu yake ya United ambaye ni baba yake hatimaye amevalia fulana yenye jina lake baada ya kuhamia kwa mahasiwa wake Manchester City. (Sun)

Kuingo wa Manchester United Bruno Fernandes, 26, amekataa kumnyooshea kidole Ole Gunnar Solskjaer na wachezaji wenzake baada ya kipigo cha 6-1 kutoka kwa Tottenham kabla ya mapumziko ya kupisha mechi za kimataifa. (Sport TV, via Metro)

Maelezo ya picha,

Manchester United katika kumsajili Pau Torres

Arsenal inataka kuipiku Manchester United katika kumsajili mlinzi wa Villarreal, Pau Torres, 23, kwa kitita cha £35m mwezi January. (Express)

Middlesbrough inajaribu kukamilisha usajili wa winga Yannick Bolasie, 31, kwa mkopo kutoka Everton. (Sky Sports)

Mmiliki wa Derby County Mel Morris anasema meneja Phillip Cocu hatafukuzwa kama timu hiyo itafungwa ijumaa hii dhidi ya Watford, na kukataa pia taarifa kwamba mshambuliaji wa zamani wa England Wayne Rooney, 34, atambadili mdachi huyo.(Talksport)Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *