Trump apiga marufuku mahusiano na wamiliki wa Tik Tok


Hatua hiyo  hata  hivyo  haijajulikana  iwapo  rais wa Marekani  ana mamlaka ya kisheria kupiga marufuku app hiyo nchini Marekani.

Amri hizo mbili za utendaji, moja kwa kila  app, inaanza  kutumika katika  muda wa  siku 45 zijazo. Zinamtaka waziri  wa  biashara kufafanua  utendaji wa  marufuku  hizo kwa wakati huo. Wakati maelezo  ya amri hizo  hayaeleweki, baadhi  ya  wataalamu wamesema  inaonekana zina lenga  kuzuwia  app  hizo  maarufu kuwekwa  katika app  inayohifadhi  app  kama  hizo  katika  Apple  na Google,  hali  ambayo  inaweza  kuziondoa  kabisa  katika usambazaji  wa  app  hizo   nchini  Marekani.

USA I Donald Trump in Clyde I Ohio (picture-alliance/AP/S. Walsh)

Rais wa Marekani Donald Trump

“Haya ni matumizi yasiyo kifani  ya mamlaka ya rais,” Mchambuzi wa kundi  la Eurasia Paul Triolo alisema  katika  barua  pepe. Kw uchache  amesema, amri hiyo inaonekana, kuweka  marufuku juu  ya uwezo wa hifadhi ya app  nchini  Marekani inayoendeshwa  na kampuni  ya  Apple  na  Google na kujumuisha  app  ya  simu  za mkononi  baada  ya  siku  45.

Triolo  alisema  amri  hiyo  huenda  ikakumbana  na  vipingamizi vya kisheria  na  kuonya  kuwa  China  huenda , ikachukua  hatua  kali, takriban kwa matamshi  makali.

USA | US-Präsident Donald Trump will App Tiktok verbieten (picture-alliance/NurPhoto/J. Porzycki)

Kampuni ya ByteDance ya China inayomiliki app ya Tik Tok imepigwa marufuku shughuli zake nchini Marekani

Sheria ya dharura

Amri  ya  Trump  inaelezea  kuhusu mamlaka ya  sheria, ya  sheria ya  kimataifa  ya  dharura  ya uwezo wa kiuchumi  na  sheria ya dharura ya  taifa.

Utawala  wa  Trump imekuwa  ikipambana  na  kitisho  kutoka  China , na  wabunge  wote  wa  chama  cha  Republican na  Democrats pia wameonesha  wasi  wasi  juu  ya  Tik Tok, ikiwa  ni  pamoja  na uchujaji  taarifa, kampeni zinazotoa taarifa  zisizo  sahihi, usalama wa data za  watumiaji  na faragha kwa watoto. Lakini  utawala  huo haujatoa ushahidi mahsusi  kwamba  Tik Tok imetoa data za watuamiaji  nchini  Marekani  kwa  serikali  ya  China. Badala  yake , maafisa  wanaelekeza  katika  kitisho  cha  kufikirika  ambacho kinatokana na  uwezo  wa  serikali  ya  China  kudai ushirikiano kutoka  kwa  makampuni  ya  China.

USA Mike Pompeo (picture-alliance/ZUMAPRESS.com/R. Chiu)

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Mike Pompeo

Mapewa  wiki  hii, Trump  alitoa  kitisho cha  muda  wa  mwisho  wa Septemba 15 kufunga shughuli  za  Tik Tok  hadi  pale  kampuni  ya Microsoft  ama  kampuni  nyingine  itakapoinunua  kampuni  hiyo. Siku  ya  Jumatano , waziri wa  mambo  ya  kigeni  wa  Marekani Mike Pompeo  alitangaza  upanuzi wa mapambano  ya Marekani dhidi  ya  teknolojia  ya  China  ikiwa  ni  pamoja  na  kuzipiga marufuku app za China katika  hifadhi  ya makampuni  ya  Marekani ya app  hizo, akielezea  madai  ya  kitisho  cha  usalama  na  kuzitaja kwa  majina  Tik Tok  na  WeChat.

 Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *