Trump hatahudhuria kikao cha kusikiliza tuhuma dhidi yake, White House imesema


President Trump leaning on his hand with the American flag in the background

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Bwana Trump na mawakili wake wamepewa nafasi ya kuuliza maswali katia kikao cha kusikiliza mahsitaka dhidi yake

Ikulu ya White House imesema rais wa Marekani Donald Trump na mawakili wake hawatahudhuria kikao cha jumatano cha kusikiliza tuhuma dhidi yake ikidai ukosefu wa “haki”.

Kikao hicho kinachoendeshwana kamati ya bunge la uwakilishi la kushughulikia masuala ya haki kimefikia awamu nyingine ya uchunguzi huku wataalamu wa sherua wakitoa ushahidi ambao unaweza kufikia uamuzi wa kura ya kutokuwa na imani.

Ilidai kuwa rais iliishinikiza Ukraine kufanya uchungu mara mbili kwa maslahi yake binafsi ya kisiasa.

Bwana Trump amekanusha madai hayo.

Baada ya wiki kadhaa ya mashahidi kuhojiwa faraghani na hadharani, mchakato huo sasa utangazi uwezekano wa mashtaka ya misconduct, ambayo huenda ikachangia kupigwa kwa kura ya kutokuwa na imani bungeni na kufunguliwa kwa mashataka na kamati ya seneti inayoongozwa na Republican.

Uchunguzi Democratic ulitokana na mazungumzo ya njia ya simu ya Mwezi Julai baina ya Bwana Trump na rais wa Ukrain Volodymyr Zelensky.

Bwana Trump amepuuzilia mbali mchakato huo akiutaja kama wa “hila”.

Jumatano iliyopita, Jerrold Nadler, mwenyekiti wa kamati ya sheria ya bunge alimualika Bwana Trump ahudhurie kikao cha wiki hii , “moja kwa moja au kupitia mshauri “, akisema itakuwa ni fursa ya kujadili misingi ya kihistoria na kikatiba ya mashtaka yanayomkabili.

Unaweza pia kusoma:

Lakini katika barua kwa kamati, mshauri wa White Hous Pat Cipollone ameishutumu kamati kwa ” Kutofahamu kanuni za mchakato na usawa wa kimsingi”, akisema mwaliko ungeshindwa kuipatia ikulu ya White House muda wa kutosha kujiandaa na haukutoa taarifa zozote kuhusu mahahidi.

Taarifa zilisema kuwa mwaliko huo “ulikuwa ni nyaraka za kisomi” na kwamba ”usingejumuisha mahshahidi “, alisema Bwana . Waraka wa shahidi unaelezea ushahidi juu ya uelewa wa mtu binafsi wa matukio huku ushahidi wa kitaalamu ukisisitizia hukumu kwa kutoa maoni.

Haki miliki ya picha
Reuters

Image caption

Jerrold Nadler alisema Bwana Trump anafaa kuhudhuria kikao au “akome kulalamika”

Trump anashutumiwa nini?

Katika mawasiliano ya simu hiyo Trump alimtaka Bwana Zelensky amchunguze Joe Biden, ambaye kwa sasa ndie mgombea aliye mstari wa mbele kuwania kiti cha urais kwa tiketi ya chama cha Democratic katika uchaguzi wa urais mwaka ujao, na mtoto wake wa kiume Hunter Biden, ambaye awali alifanyia kazi kampuni ya nishati ya Ukraine Burisma.

Uchunguzi unataka kubaini juu ya ikiwa Bwana Trump alitumia tisho la kuzuwia msaada wa jeshi la Marekani kwa Ukraine ili kuifanya imchunguze Biden na mwanae. Rais Trump amekana kufanya kosa lolote na ameutaja uchunguzi kuwa ni ” hila”.

Wiki iliyopita, Kamati ya masuala ya ujasusi ilikamilisha wiki mbili za kusikiliza , kufuatia wiki kadhaa za vikao vya faragha ambapo waliwahoji mashahidi.

Adam Schiff, mwenyekiti wa kamati ya ujasusi, anayeongoza uchunguzi huo alisema kamati za masuala ya kigeni na intelijensia – sasa zinaifanyia kazi ripoti yao, ambayo itatolewa tarehe 3 Disemba. m

Ni nini kitakachofuata?

Kamati ya masuala ya sheria ya bunge inatarajiwa kuanza kuandika miswada ya tuhuma – ambazo ni mashtaka ya kufanya makosa dhidi ya rais- mapema mwezi Disemba.

Baada ya kura, bunge linalodhibitiwa na Democratic , kesi itaendeshwa katika bunge la seneti linalodhibitiwa na Republican.

Kama Bwana Trump atapatikana na hatia kwa theluthi mbili ya wabunge- matokeo ambayo yanaonekana huenda kutopatikane- atakuwa ni rais wa kwanza wa Marekani kung’olewa madarakani kupitia mashtaka ya aina hii

Ikulu ya White House na baadhi ya Warepublican wanataka kesi iendeshwe kwa wiki mbili tu.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *