Trump: Hatutafunga shughuli za kawaida tenaTrump alisema hayo wakati wa ziara yake katika kiwanda cha kutengeneza magari cha Ford, katika jimbo la Michigan, ambacho sasa kinatengeneza vifaa maalum vinavyowasaidia wagonjwa kupumua.

Amesema kwamba magavana wataendelea kufungua majimbo kutokana na shinikizo kutoka kwa raia.

“Nadhani idadi kubwa ya majimbo ambayo bado yana masharti magumu ya kutofungua shughuli za kawaida, yataondoa masharti hayo. Sidhani kwamba watu wataendelea kuvumilia. Hii ni nchi ambayo ni lazima ifungue shughuli za kawaida na tumefanya jambo lililo sawa. Tumeokoa Maisha ya mamilioni ya watu” amesema rais Trump

Rais Trump aliulizwa kuhusu uwezekano wa kutokea maambukizi mapya ya virusi vya Corona baada ya kufungua shughuli za kawaida.

Amesema kwamba hilo linaweza kutokea lakini hiyo sio sababu ya kufunga shughuli za kawaida kwa mara ya pili.

Imetayarsihwa na Mwandishi wetu Kennes Bwire, Washington DCSource link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *