Ubaguzi kwenye soka: ‘Huwezi kujua kile anachohisi muhusika wakati huo


Haki miliki ya picha
Reuters

Image caption

Mshambuliaji wa Mario Balotelli aliwahi kuwa mwathirika wa ubaguzi wa rangi

“Walikuwa wananiita tumbili mweusi, na kuonyesha ishara za tumbili” – Inih Effiong, mchezaji wa timu ya Dover Athletic.

“‘Kwanini mtu mweusi anataka kufunga bao?’, ‘Mwangalie vile, tumbili wewe” – Nathan Ashmore, mlinda lango wa timu ya Boreham Wood FC.

“Ananuka kama mchuzi wa curry” – Imrul Gazi, mchezaji wa timu ya Sporting Bengal.

Ni kile kilichowatokea baadhi ya wachezaji wa soka ya kulipwa, walisema hayo walipoongea na BBC Three kwenye filamu ya Shame in The Game, ambayo inaangazia ubaguzi unaoendelea katika soka ya Uingereza kuanzia ligi ya Premier, ligi ndogo ndogo hadi michezo ya wanawake. Filamu hiyo itaanza kuonekana kwenye iPlayer kuanzia Jumatano, Februari 12.

Haki miliki ya picha
BBC THREE

Image caption

Mchezaji Imrul Gazi, wa Sporting Bengal

Wachezaji na mameneja wanaozungumza katika filamu hiyo hawaoni kama hatua zinazofaa zimekuwa zikichukuliwa na mamlaka husika za kandanda.

Imrul Gazi – kocha wa timu ya Sporting Bengal ya Asia inayoshiriki ligi ndogo ambayo makao yake ni Uingereza – anaaminika kwamba hakuna kitakachobadilika hadi kuwe na wawakilishi wa waliowachache katika mamlaka za kandanda.

“Hakuwezi kufanyika maamuzi yoyote yenye tija ikiwa wanaoketi kwenye meza ya mazungumzo ni wazungu wa daraja la kati,”amesema. “Hauwezi kujua mtu anapoitwa tumbili au nyani anahisi vipi. Ama kuambiwa nenda kwenu’.

“Usiniambia kwamba unaelewa kwasababu huna ufahamu wa kinachoendelea .”

Mshambuliaji wa timu ya Dover Athletic, Inih Effiong, 28, pia naye ana maoni sawa na hayo. Aliwahi kurushiwa maneno ya kibaguzi wakati timu yake inacheza ugenini na Hartlepool United Septemba mwaka jana.

Haki miliki ya picha
BBC THREE

Image caption

Inih Effiong, mchezaji wa Dover Athletic

Ikiwa jambo kama hili litatokea refa awe ni mweusi,” aliiambia BBC Three, “bila shaka hatua ambayo ingechukuliwa ingekuwa tofauti.” Aliongeza: “Refa wakizungu hawaelewi.”

Baada ya kufunga kupitia mkwaju wa penalti, Effiong alianza kusherehekea mbele ya mashabiki wa timu ya Hartlepool ambapo moja kwa moja alipewa kadi ya njano, uamuzi ambao bado unaungwa mkono na FA

“Niliwakunjia masikio yangu,” Effiong anasema, “Huo ndio wakati wachezaji walianza kubaguliwa.

“Refa alikuwa anasema kwamba mimi ndio chanzo kwasababu ya kusherehekea,” Effiong anaelezea kwenye filamu, na kuongezea: “Kama refa, haustahili kusema… maneno kama hayo, eti kwasababu nilisherehekea mbele yao nilistahili kubaguliwa.”

Alirushiwa mkate wa nyama na kuambiwa maneno ya kibaguzi na ishara zinazoashiria kwamba ni tumbili.

Baada ya refa aliyempa kadi ya njano kuulizwa kuhusu tukio hilo, alisema kwamba matamshi ya ubaguzi wa rangi aliorushiwa Effiong ni jambo lisilokubalika kabisa, lakini huenda hangefanyiwa vitendo vya ubaguzi iwapo hangesherehekea mbele ya mashabiki wa Hartlepool.

”Ubaguzi wa rangi ni jambo ambalo linaendelea kujitokeza katika soka ya Uingereza kila uchao. ”

Shirikisho la soka nchini Uingereza FA lilitoa amri kwamba Hartlepool ilipe faini ya £7,500 kwa makosa ya ubaguzi wa rangi dhidi ya Effiong, huku wakiitajika tena kutoa £5,000 na kupigwa marufuku kucheza kwa miezi 18.

Effiong amekatishwa tamaa na haoni kwamba faini waliopewa inatosha kama adhabu.

Anasema: “Ni hatua hafifu sana ukilinganisha na uovu uliotendwa – hakuna hatua yoyote ya msingi inayoendelea.”

Takwimu rasmi kutoka ofisi ya masuala ya ndani inasema kwamba hili ni tatizo linaloendelea. Vitendo vya uhalifu unaochochea chuki vilivyoripotiwa vimeongezeka kwa asilimia 66 katika michezo ya soka ya kulipwa Uingereza na Wales msimu uliopita. Kati ya visa 323 vilivyorekodiwa misimu miwili iliyopita, visa 230 vina uhusiano na ubaguzi wa rangi.

Haki miliki ya picha
BBC THREE

Image caption

Marvin Sordell

“Ubaguzi wa rangi ni kitu ambacho kinaendelea kuongezeka kila uchao katika soka ya Uingereza. Mwanahabari Jonathan Liew amesema hivyo katika filamu. Na wachezaji wengi niliozungumza nao hawaoni kama hatua stahiki zinachukuliwa.

Marvin Sordell – aliyekuwa mchezaji wa Watford na Fulham, anasema kwamba miongoni mwa vilivyochangia kwa kiasi kikubwa yeye kustaafu soka akiwa na umri wa miaka 28 pekee, ilikuwa ni kiasi kikubwa cha ubaguzi uliokuwa ukishuhudiwa katika mchezo huo – na anaamini kwamba mamlaka za mchezo wa soka kama vile FA na FIFA, “zinastahili kuchukua hatua zaidi”.

Kituo cha BBC Three kiliwasiliana na timu zote 20 katika ligi ya Premier wakati wanatengeneza filamu hii. Lakini ni klabu moja pekee iliyowezesha wachezaji wao kuzungumza na timu ya BBC Three kuhusu suala la ubaguzi wa rangi katika mpira wa kandanda – Watford.

Katika filamu hiyo, Andre Gray na Tom Cleverley wote walizungumza kuhusu ubaguzi wa rangi ambao wachezaji wa Watford wamewahi kupitia wakati wanacheza mechi ya nusu fainali ya kombe la FA dhidi ya Wolves Aprili mwaka jana.

Haki miliki ya picha
BBC THREE

Image caption

Andre Gray, Watford

“Hakuna hatua yoyote ambayo imechukuliwa, polisi haikufanya lolote, shirikisho la FA…wale walio katika ngazi ya juu hata hawakuchukua hatua yoyote,” Gray amesem

Wakati huo, nahodha wa Watford Troy Deeney alizuia watu kutoa maoni yao kwenye akaunti yake ya Instagram baada ya kurushiwa maneno ya ubaguzi wa rangi.

Kick It Out ni kampeni iliyojibu madai ya ubaguzi wa rangi na kutaka Twitter, Instagram na Facebook kuchukua hatua stahiki dhidi ya wale wanaotumia mitandao yao kutoa matamshi ya chuki.

Kuna wakati ambao nilikuwa ninaenda nyumbani baada ya mazoezi, na nikaanza kulia nikiwa njiani.

Wakati ambao Inih Effiong alikuwa anabaguliwa, wachezaji wa Dover Athletic na meneja wao walitaka kuondoka uwanjani na kusitisha mechi waliokuwa wanacheza. Effiong alikieleza kituo cha BBC Three kwanini hawakuendelea na mpango huo.

“Kocha aliniambia kwamba anaweza kutoka uwanjani iwapo nitakuwa tayari afanye hivyo,” Effiong anaelezea: “Tukafanya mazungumzo mafupi na kukubaliana kwamba badala ya kuondoka uwanjani, tuhakikishe tumechukua ushindi katika mechi hiyo. Tulikuwa tunacheza ugenini na hatukutaka kurejea tena huko.”

Effiong alituambia kwamba, ikiwa jambo kama hili litatokea tena, atatoka uwanjani.

“Ni vigumu sana kuendelea kucheza baada ya kutokea kwa tukio kama hilo. Haswa ikiwa kila wakati unaposhika mpira unazomewa.”

Effiong pia anasema kwamba baada ya tuki hilo aliwaza kuachana na fani ya uchezaji mpira wa soka.

“Wakati huo kilikuwa ni ktiu kinachoumiza moyo sana,” alituambia, na kuongeza kwamba: “Umefanya bidii katika kipindi chote cha maisha yako lakini matoke yake ni kwamba watu wanakubagua kwa kukurushia maneno ya chuki.”

Hata hivyo msemaji wa FA amesema: “Shirikisho la FA limepiga hatua kubwa katika miaka ya hivi karibuni kuhakikisha kwamba soka ya Uingereza inajumuisha kila mmoja na mchezo huo kuwa wa kipekee zaidi.

“Mwaka 2018, shirikisho la FA lilianzisha mpango maalum wenye malengo ya kuhakikisha kwamba mchezo wetu unaakisi jamii ya kisasa. Hilo ni pamoja na kuunda fursa ya katika soka na siyo tu uwanjani pekee na kwa kila mtu bila kujali asili yake.

“Tunalaani vitendo vyote vya ubaguzi wa rangi na kuhamasisha mashabiki wote na washiriki wanaoamini wamepitia ubaguzi wa rangi waripoti visa hivyo kwa kutumia njia stahiki. Kupitia shirikisho la FA, kwenye mtandao wa FA au kupitia washirika wetu katika kampeni ya Kick It Out.”

Kumbuka kwamba unaweza kutazama filamu ya Shame in The Game iliyoandaliwa na BBC Three kupitia iPlayer kuanzia Jumatano, 12 Februari.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *