Uchaguzi wa Uganda 2020: Bobi Wine asema 'Museveni anakabiliwa na kizazi chenye hasira na njaa'


Wafuasi wa mwanamuziki aliyegeuka mwanasiasa Robert Kyagulanyi, maarufu Bobi Wine, walibeba mabango na kuandamana katika maeneo tofauti ya Uganda kupinga hatua ya kukamatwa kwake mapema wiki hii

Maelezo ya picha,

Waandamanaji walikusanya na kuchoma tairi za magari katika mji mkuu wa Kampala, mapema wiki hii

Mgombea urais wa upinzani nchini Uganda Robert Kyagulanyi, maarufu Bobi Wine, amesema Rais wa Yoweri Museveni anakabiliana na kizazi ambacho kitafanya kila iwezelo kupigania uhuru.

Alisema hayo katika hafla ya maombi iliyoandaliwa katika makao makuu ya chama chake kuwaomea watu waliouawa katika maandamano ya siku mbili yaliyokumba nchi, siku moja baada ya kuachiwa kutoka kizuizini.

Akimlenga moja kwa moja kiongozi wa nchi moja kwa moja Bobi Wine alisema Bwana Museveni anakabiliwa na kizazi ambacho kina njaa na hasira kwa wakati mmoja.

Hakuna kiwango chochote cha mabomu ya machozi au mateso ambacho kitawaogopesha, aliongeza.

Mgombea huyo wa urais amesema mashambulio yaliyofanywa dhidi ya raia wiki hii yameweka wazi udhalimu wa serikali ya sasa iliyo madarani.

Akiwahutubia wafuasi na maafisa wa chama, alisisitaiza kwamba damu ya raia wasiokuwa na hatia iliyomwagika wiki hii haitaenda bure, na kuongeza kuwa haki itatekelezwa.

Maelezo ya picha,

Supporters of presidential candidate Bobi Wine were detained on Wednesday and Thursday

Jumamosi asubuhi, magari ya vikosi vya usalama yaliegeshwa katika maeneo tofauti mjini Kampala huku askari wakishika doria katika maeneo karibu na makao makuu ya chama cha upinzani cha People’s Power.

Polisi imetangaza kuwa ni watu 28 waliofarika katika maandamano ya siku ya Jumatano na Alhamisi, japo vyombo vya habari nchini vinanukuu vyanzo vya hospitali kuu kwamba idadi ya waliofariki ni watu 37.

Bobi Wine aliachiwa kwa dhamana siku ya Ijumaa, baada ya kushtakiwa kwa kukiuka kanuni za kudhibiti kusabaa kwa virusi vya corona. Anakabili wa kifungo cha hadi miaka saba gerezani akipatikana na makosa.

Lakini kwa sasa, mwanamuziki huyo na mwanasiasa amesema yuko tayari kurejelea kampeni zake kuanzia Magharibi mwa Uganda.

Maelezo ya video,

Kura za vijana zinaweza kumpa ushindi Bobi Wine?

Mnamo mwezi Juni Bobi Wine aliapa kukiuka marufuku ya mikutano ya kampeni wakati wa janga la corona. Alimshtumu Rais Museveni kwa “kuogopa watu”.

Msmaji wa serikali ya Uganda Don Wanyama ameambia BBC kuwa maafisa “hawengeweza kutualia na kuangalia ghasia kufanyika j”.

Pia amesema RaiS Museveni “ametii marufuku iliyowekwa na Tume ya Uchaguzi na Wizara ya Afya”.

Human Rights Watch linasema ni wazi kwamba mamlaka za Ugandan zinatumia mwongozo wakuzuia Covid-19 kukandamiza upinzani na kuongeza kuwa chama tawala kimefanya kampeni kubwa.

Bobi Wine ni nani?

Nyota huyo wa mtindo wa Afrobeats aliingia katika taaluma ya muziki katika miaka ya 2000, hna anaelezea kipaji chake kuwa ni cha kuelimisha na kuburudisha. Mojawapo ya vibao vyake vya awali Kadingo, inahusu usafi wa mwili.

Jina lake rasmi Wine, ni Robert Kyagulanyi Ssentamu, alichaguliwa kuwa mbunge katika uchaguzi mdogo baada ya kusimama kama mgombea huru mwaka jana wilayani Kyadondo mashariki, Uganda ya kati.

Aliwashinda wagombea kutoka chama tawala National Resistance Movement (NRM) na chama kikuu cha upinzani Democratic Change (FDC).

Baada ya kutangazwa mshindi, aliahidi kuangazia zaidi kuwaunganisha raia.

“Jambo langu la kwanza ninalotaka kufanya ni kufanikisha maridhiano kati ya viongozi wa Kyadondo Mashariki…Ninataka siasa zitulete pamoja… jinsi muziki ufanyavyo.”Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *