

Chanzo cha picha, EPA
Polisi waliyojihami wamekuwa wakipiga doria katika barabara za Kampala
Mwanamuziki nyota wa pop aliye na umri wa mika 38- anachuana kisiasa na mmoja wa viongozi wa Afrika aliyehudumu muda mrefu madarakani katika uchaguzi wa Uganda unaokabiliwa na ushindani mkali
Robert Kyagulanyi, maarufu Bobi Wine, anasema kuwa anawakilisha kizazi kipya cha vijana wa nchini humo, huku Yoweri Museveni, 76, akisema kuwa anasimamia ustawi.
Kampeni zilikumbwa na vurugu ambazo zilisababisha vifo vya watu kadha.
Serikali imeagiza kufungwa kwa mitandao yote ya kijamii.
Rais Museveni anasema hii ni kwa sababu Facebook ilipiga marufuku akaunti kadhaa zinazounga mkono chama tawala.
Sera ya polisi nchini Uganda inasema maafisa watapanda juu ya majengo marefu mjini Kampala siku ya uchaguzi, baaada ya magari yaliyo na silaha kuanza kuzunguka katika mitaa ya jiji hilo.
Vituo vya kupiga kura vitafunguliwa saa moja kwa saa za Afrika Mashariki (04:00 GMT), lakini matokeo ya uchaguzi haitarajii kutangazwa kabla ya Jumamosi.
Rais Museveni anagombea muhula wa sita baada ya kuwa madarakani kwa miaka 35.
Kampeni zilikuwa zimepigwa marufuku katika mji mkuu wa Kampala na katika baadhi ya wilaya.
Upinzani unasema hatua hiyo ilichukuliwa kwasababu ya umaarufu wake lakini serikali inasema ilifikia uamuzi huo ili kudhibiti msambao wa ugonjwa wa Covid-19.
Uchaguzi wa Uganda 2021:Mambo matano unapaswa kufahamu kuhusu uchaguzi huu
Wagombea wa upinzani akiwemo – Bobi Wine – wafuasi wao na wafanyakazi wa kampeni wamekamatwa mara kadhaa.
Polisi imesema imewapeleka maafisa wake katika maduka makubwa na majengo mengine marefu baada ya wanaharakati wa upinzani kuwaelekeza waandamanaji kutoka juu ya majengo hayo mwezi Novemba, ambapo zaidi ya watu 50 waliuawa baada ya Bobi Wine kukamatwa.
Waangalizi kutoka Afrika na wala sio wa Marekani
Siku ya Jumatano Marekani ilitangaza kuowaondoa waangalizi wake baada ya wengi wao kukosa idhini ya kufuatilia mchakato wa uchaguzi huo.
Balozi wa Marekani nchini Uganda Natalie Brown alisema katika taarifa yake kwamba bila kuwa na waangalizi, uchaguzi wa urais na wa ubunge huenda ukakosa “uwajibikaji, uwazi na ujasiri”.
Aliongeza kuwa waangalizi kadhaa wa Uganda pia hawajapewa idhini ya mwangalizi.
Pendekezo la Muungano wa Ulaya kuwatuma wataalamu wa uchaguzi pia halikuitikiwa.
Kujibu ukosoaji huu, msemaji wa Bw. Museveni Don Wanyama aliandika taikia Twitter ya yake kwamba kuna waangalizi kutoka Mungano wa Afrika na Jamuiya ya frika Mashariki.
“Sikumbuki ni lini Uganda iliwapeleka waangalizi wake nchini Marekani,” aliongeza kusema.
Serikali imesisitiz kuwa uchaguzi utakuwa huru na wa haki.
Bobi Wine ametoa wito kwa wapigakura kusalia katika vito vya kupiga kura siku ya Alhamisi na kutumia kamera ya simu zao kurekodi mchakato wa kujumuisha kura ili kuzuia wizi wa kura.
Siku ya Jumatano, mashirika ya simu yaliawafahamisha wateja wao kwamba wamefungia mitandao yote ya kijamii na programu tumishi za kutuma ujumbe, kufuatia agizo la Tume ya Mawasiliano ya Uganda.