Uganda kuidhinisha baraza la kitaifa la Kiswahili wakati ikielekea kuwa lugha rasmi ya pili nchini


Kiswahili Uganda

Haki miliki ya picha
AFP

Serikali ya Uganda imeidhinisha kuundwa kwa baraza la kitaifa la Kiswahili litakaloongoza kuidhinishwa kwa kiswahili kuwa lugha rasmi ya pili nchini.

Waziri wa jinsia kazi na maendeleo ya Jamii Peace Mutuzo ameieleza BBC kwamba Kiswahili ni lugha iliyokubalika katika katiba ya Uganda.

“Katika siku za nyuma kiswahili kilikuwa kikitumiwa na majeshi, wezi, waliokuwa wakikitumia vibaya na kufanya vurugu kwa watu na (watu) hawakukipenda kiswahili sana. Lakini leo, tumekuwa watu wamoja katika Afrika mashariki na tungependa kuendeleza kiswahili”.

Mutuzo amebaini kwamba kamati hiyo mpya inayoidhinishwa itapitia taratibu mbalimbali za kiserikali kabla ya kuanza kufanya kazi ya kueneza lugha ya kiswahili na ‘kukuza jumuiya yetu na utamaduni kwani mambo mengi yanayozungumza kwa kiswahili ni mambo yanayojulikana na lugha nyingine za hapa Uganda’.

Waziri huyo ameongeza kusema kuwa kuna imani kwamba watafanikiwa kukieneza kiswahili.

Haki miliki ya picha
AFP

Image caption

Msemaji wa serikali ya Uganda Ofwono Opondo

“Tuna walimu wengi ambao wamefunzwa kiswahili na wana vyeti lakini hawajapata kazi, na tutazungumza na wizara ya elimu kuwapatia kazi waweze kufundisha kiswahili shuleni na kwenye redio, na televisheni”.

Baraza hilo linatarajiwa kusimamia kuidhinishwa kwa sera, na muongozo wa kisheria na kitaasisi kwa kuweka viwango vya kuhimizwa ipasavyo na kuendelezwa kwa lugha ya kiswahili katika nyanja zote.

Katika mkutano na waandishi habari msemajiwa serikali ya Uganda, Ofwono Opondo ameeleza kwamba kuidhinishwa baraza hilo kunaambatana na katiba na litakuwa na jukumu la kuhakikisha kuwa Kiswahili kinaidhinishwa kama lugha ya pili rasmi nchini, Daily Monitor linaripoti.

Historia ya Kiswahili nchini Uganda

Mwaka 1960, Serikali ya Uganda iliruhusu na kulazimisha Kiswahili kitumike nchini humo; Kiingereza na lugha za kikabila zilikuwa tayari zinatawala mawasiliano Uganda nzima.

Lugha ya maandishi ya Kiswahili yalianza kutumika katika Baraza la Kifalme la Buganda na Bunyoro, hata kabla ya ukoloni (1862). Kiswahili hutumika katika shughuli za biashara, dini na mila.

Nchini Uganda Kiswahili kilifikiriwa kwamba ni lugha ya watumwa. Lakini Kiswahili kilitumiwa zaidi na Polisi na Wanajeshi.

Katibu mtendaji wa Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki, Keneth Cimara ameipongeza serikali ya Uganda kwa juhudi ya kuendeleza Kiswahili tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Kiswahili ni lugha rasmi ya muungano wa Afrika.

KENYA

Kiswahili nchini Kenya ni lugha rasmi na pia ni lugha ya Taifa. Rais wa kwanza wa taifa la Kenya hayati Mzee Jomo Kenyatta alitoa kauli kwamba Kiswahili kinafaa kutumika kama lugha rasmi ya Kenya mwaka 1969.Mwaka 1975 kiswahili kilianza kutumika bungeni.

  1. Maneno ya Kiswahili yaongezwa kamusi ya Kiingereza

Serikali ya Kenya ilianzisha somo la Kiswahili katika Idara ya Lugha za Kiafrika na Isimu ya Chuo Kikuu cha Nairobi.

Haki miliki ya picha
YASUYOSHI CHIBA

Kuanzia miaka ya themanini mwishoni, takriban vyuo vikuu vyote vilivyoanzishwa na Serikali vilifundisha masomo ya Kiswahili kwa lugha ya Kiswahili.

TANZANIA

Kiswahili nchini Tanzania ni lugha rasmi na lugha ya Taifa. Ni lugha ya utambulisho kwa Mtanzania na inatumika kama lugha ya kuimarisha uelewano, ushirikiano na umoja wa kitaifa.

Katika kuiendeleza, juhudi za usanifishaji zimefanyika kwa kuwatumia wataalamu wa fasihi na isimu, wadau wengine na wachapishaji vitabu.

Vyombo mbalimbali vimeubuniwa kama Bakita, Bakiza, Takiluki, Taasisi ya Elimu, Uwavita na Ukuta. Pia vyuo vikuu mbalimbali vya Bara na Visiwani vilianza kusomesha Kiswahili kuanzia shahada ya kwanza, ya uzamili na uzamivu.

Huwezi kusikiliza tena

Kiswahili chakaribia kuwa lugha rasmi Rwanda

RWANDA

Kiswahili ni lugha rasmi nchini Rwanda. Kabla mwaka 1994 , wakati wa mauaji ya kimbari lugha ya kiswahili ilizungumzwa kwenye mji tofauti .

Lugha ya Kiswahili ilisambaa baada ya Wanyarwanda kuwaruhusu Wajerumani nchini mwao kama watawala karne ya 19.

Mwaka wa 1976 -1977 lugha ya Kiswahili ilianza kufundishwa katika shule za upili na chuo Kikuu Cha Rwanda.

Haki miliki ya picha
FREDERIC DE LA MURE

UGANDA

Mwaka 1960, Serikali ya Uganda iliruhusu na kulazimisha Kiswahili kitumike nchini humo; Kiingereza na lugha za kikabila zilikuwa tayari zinatawala mawasiliano Uganda nzima.

Lugha ya maandishi ya Kiswahili yalianza kutumika katika Baraza la Kifalme la Buganda na Bunyoro, hata kabla ya ukoloni (1862). Kiswahili hutumika katika shughuli za biashara, dini na mila.

Nchini Uganda Kiswahili kilifikiriwa kwamba ni lugha ya watumwa. Lakini Kiswahili kilitumiwa zaidi na Polisi na Wanajeshi

Wikendi hii Katibu mtendaji wa Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki, Keneth Cimara imeipongeza serikali ya Uganda kwa juhudi ya kuendeleza Kiswahili tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Huwezi kusikiliza tena

Mwanamuziki anayevumisha Reggae ya Kiswahili

Katika warsha ya siku mbili iliyokamilika mwishoni mwa juma katika hoteli ya Imperial Royal mjini Kamapla iliyowajumuisha walimu wa vyuo vikuu, shule za upili na taasisi mbalimbali nchini Uganda.

Keneth Cimara amesema miaka ya themani raia wengi wa Uganda walikiona Kiswahili kama lugha ya wahalifu ikitumiwa na askari kuwanyanganya mali zao, aidha kuwatendea uhalifu.

Cimara ameongeza kwamba sasa Serikali ya Uganda ni miongoni mwa mataifa ya Jumuia ya Afrika mashariki ambayo yameweka mikakati ya kuendeleza matumizi ya lugha ya Kiswahi kama anavyosema tena Katibu mtendaji.

JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO

Kiswahili kiliingia nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo kuanzia karne ya 19. Kiswahili kilianza kuenea kutoka Mashariki mwa nchi hiyo ,kuelekea kandokando ya mto Kongo.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *