Ujerumani kukutanisha pande zinazohasimiana Libya katika juhudi za kutafuta amani


Fighters loyal to the internationally recognised Libyan Government of National Accord (GNA) rest in an area south of the Libyan capital Tripoli on 12 January 2020.

Haki miliki ya picha
AFP

Makundi ya wapiganaji nchini Libya wameungana na mataifa yenye nguvu nchini Ujerumani kushinikiza kusitisha mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.

Mazungumzo hayo yamekuja mara baada ya utekelezaji wa maubaliano ya awali ambayo hayakuwa yameafikiwa na upande wa pili kutibuka.

Mgogoro huo ambao uliongozwa na Jenerali Khalifa Haftar dhidi ya serikali ambayo ilikuwa inafadhiliwa na Umoja wa mataifa ,katika mji mkuu wa Tripoli.

Mkutano wa jumapili ulikuwa umelenga pia kupata ahadi kutoka kwa mataifa ya kigeni kutaka Umoja wa mataifa kusitisha matumizi ya silaha zao na kutoingilia mgogoro huo.

Siku ya jumamosi Jenerali Haftar alisitisha usafirishaji wa mafuta kutoka katika bandari kuu kadhaa – na kufanya taifa kuwa katika wakati mgumu kwa sababu mafuta ndio kipato kikuu cha mapato katika nchi hiyo.

Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson alisema kuwa lengo la mkutano huo ni kumaliza mgogoro huu.

“Watu wa Libya wameteseka vya kutosha,” Alisema alipowaasili siku ya jumapili.

“Huu ni wakati ambao taifa linapaswa kusonga mbele na kujiletea maendeleo.”

Mkutano huo unaleta pande zote mbili nchini Ujerumani katika mji mkuu wa Berlin, yakiwemo mataifa ambayo yamekuwa yakifadhili mapigano hao, Umoja wa mataifa na viongozi wa mataifa mengine yenye nguvu duniani kama vile rais Vladimir Putin wa Urusi na rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan.

Haki miliki ya picha
AFP

Image caption

Waziri mkuu wa Tripoli Fayez al-Serraj (kushoto) na Jenerali Khalifa Haftar walijumuika katika mkutano huo pia

“Hatujapoteza matumaini katika mdahalo huu na tutaendela kutatua tatizo hili,” bwana Putin alisema siku ya jumapili kabla ya kukutana na rais wa Uturuki katika mkutano huo.

Bwana Erdogan, ambaye hivi karibuni aituma silaha kali kuisaidia serikali ya Tripoli, alisema kabla ya mkutano kuwa Jenerali Haftar “Lazima tuwe na msimamo mkali wa kusitisha mapigano haya”.

Nini kimetokea Libya?

Haki miliki ya picha
Reuters

Kama ilivyotokea kwa Syria, ilianza tu kwa maandamano ya wakati wa vuguvugu la mapinduzi ya Arabuni 2011.

Vikosi vinavyoungwa mkono na Nato vilipindua utawala wa muda mrefu wa Muammar Gaddafimwaka huo, huku raia wakiwa na matumaini mengi tu si raia wa Libya pekee badi hata jamii ya kimataifa.

Tangu wakati huo, nchi hiyo imekuwa katika vita vya wenywe kwa wenyewe.

Baada ya miaka kadhaa ya mapigano, Umoja wa Mataifa ilisaidia kuanzishwa kwa utawala ulioongozwa na waziri mkuu Serraj.

Serikali yake ya Muungano wa Kitaifa ilikuwa mjini Tripoli na ilitarajiwa kuunganisha nchi hiyo.

Japo siyo kila mmoja aliyeunga mkono makubaliano hayo na Jenerali Haftar alitaka kuwa nguvu zaidi ya madaraka.

Aliunda jeshi lake la taifa mashariki mwa nchi hiyo kwa kuzingatia miji ya Tobruk na Benghazi.

Pia alidai kwamba anaweza kurejesha usalama na kupiga vita kile alichokiita ugaidi wa makundi ya kiislamu.

Vikosi vya Jenerali Haftar vimekuwa vikiingia kuelekea mji mkuu wa Tripoli tangu April 2019. Mwezi huu, vilifanikiwa kuteka mji wa kimkakati wa pwani wa Sirte.

Lakini ili kuchanganya mambo zaidi, wanamgambo wapo katika miji mbalimbali, wakipigana vita vyao na wakati hayo yakiendelea, kundi linalojiita Islamic State limejitokeza na kuendeleza shughuli zake katika maeneo mbalimbali ya jagwani.

Mataifa ya kigeni yanahusikaje katika mgogoro huo?

Mataifa ya kigeni katika mgogoro huu yameanza kuhusishwa katika miezi ya hivi karibuni, haswa Uturuki ambayo ikidaiwa kusaidia kwa kutoa silaha ili kusidia serikali ya Libya kuendelea na mapigano.

Huku Jenerali Haftar wa kikosi cha wapiganaji kikiungwa mkono na Urusi, Misri, Saudi Arabia, Jumuiya ya Mataifa ya kiarabu na Jordan.

Haki miliki ya picha
AFP

Image caption

Bwana Salamé alisema kuwa mataifa ya kigeni yamechochea mapigano ya Libya kuendelea kukua

Siku ya jumamosi, kikosi maalum cha Umoja wa mataifa kilitaka mataifa makubwa duniani kuacha kuvisaidia vikosi vya wapiganaji kwa kuwapa silaha, fedha na msaada wa kijeshi.

Aliiambia BBC kuwa hatua zinapaswa kuchukuliwa ili kusitisha mapigano hayo ambayo yanawagawa Libya.

Bwana Salamé aliiambia BBC kuwa suluhisho la kisiasa katika mgogoro huu lilikuwa muhimu kwa pande zote kushiriki katika mkutano huo ili wapate suluhisho la pamoja, kutokana na ukanda waliotoka, nguvu wanayotumia, madhara yanayosababishwa kwa wananchi wa Libya, uharibifu wa miudombinu na ugumu wa taifa hilo kuendelea.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *