Umoja wa Mataifa waonya kuhusu mgogoro wa Fizi jimbo la Kivu Kusini


Kwenye mkutano na wandishi habari hapa mjini Kinshasa,kiongozi wa tume ya haki za dinadamu ya umoja wa mataifa nchini Kongo, Abdoulaziz Thioye amesema kwamba hali ya kiusalama kwenye mtaa wa Fizi, huko Kivu ya kusini, nilazima iboreshwe haraka iwezekanavyo.

Thioye amesema kwamba miito kwa ajili ya kuchochea chuki za kikabila inahatarisha amani kwenye eneo hilo

“Machafuko hayo ambayo yametokea huko Minembwe toka mwezi wa machi, kuna mameno ya uchochezi wa chuki yanano ripotiwa baina ya jamii zinazohasimia. Tumeshuhudia pia chuki za kikabila na hata uraia wa Kongo, hali hiyo inaleta tatizo.Kunaumuhimu wa kurejesha kila mutu kwenye jia ya busara,wakiwemo wale wanaochochea kisisisiri machafuko hayo,na mabao ni watu wanaoshikilia madaraka kwa ngazi ya juu,” alisema Abdoulaziz Thioye.

Umoja wa mataifa unaelezea kwamba zaidi ya vijiji 73 vimechomwa moto na makundi ya wapiganaji wa kikabila. Huku vijiji 4 ambavyo ni vya jamii ya kabila la Benyamulenge.

Juhudi za upatanishi zaanzishwa kukabiliana na mizozo

UNHCR Südsudan Flüchtlinge (Getty Images/AFP/I. Kasamani)

Wakimbizi kutoka Congo waliokimbia makaazi yao kwasababu ya machafuko

“Tumewakumbusha wote kwamba uchochezi wa chuki za kikabila ni makosa ambayo mahakama ya kimataifa yanaweza kuhukumu, na wale wanaohusika na machafuko hayo watafuatiliwa na mahakama ya kitaiafa ama kimataifa. Tunauwezo wa kuchunguza vyanzo vya machafuko hayo na vilevile kubainisha wale wanaotawanya ujumbe wa chuki za kikabila. “

Vijiji kadhaa vya mtaa wa Fizi, vikiwemo Minembwe, Bijombo,Lulenge, na Itombwe vinakabiliwa na machafuko hayo ambayo umoja wa mataifa unaelezea kwamba ni kutokana na misingi ya kikabila.

Kila jamii inawanamgambo wake. Na makabila yanayoishi kwenye maeneo hayo ni pamoja na wa Babembe, benyamulenge, Banyindu,bafuliru,Bavira na Banyindu.

Wazalia wa Kivu ya kusini wanaoishi hapa mjini Kinshasa,wameanzisha juhudi za upatinishi ilikumalizisha machakufuko hayo. Norbert Basengezi, alienazisha mazungumzo ya makundi ya kikabila kutoka mtaa wa Fizi.

Lakini amesema juhudi za mazungumzo zimekwama kutokana na misimamo mikali ya baadhi ya viongozi wa makabila hayo. Umoja wa mataifa umesema kwamba mbali na juhudi za mazungumzo nilazima jeshi kuingilia kati na kurejesha mamlaka ya kitaifa.

Saleh Mwanamilongo-DW Kinshasa.

 Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *